Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Nadhani hivi karibuni kila Mtanzania na ulimwengu mzima kwa ujumla, wameshangazwa na kufadhaishwa na kauli ya Raisi Samia kutoa agizo kwamba madini yaliyoko Serengeti yachimbwe, kwa sababu simba na tembo hawali madini.
Tangazo la raisi Samia
Sasa labda watu wengi wasichoelewa ni kwamba, kwa miaka kadhaa, UAE wamefanya jitihada kubwa ya kutengeneza mazingira ya "Serengeti" huko Dubai, kwa lengo la kukuza utalii wa wanyama pori huko Dubai. Na kila mtu anajua kwamba wengi wa wanyama waliopelekwa Dubai Safari Park wametoka Tanzania, na bado hadi leo wanapelekwa. Hii ni kutia ndani na tembo, simba, viboko, vifaru, nyoka, vinyonga, fisi, ndege, swala, duma, nyani, twiga, kenge, mamba, sokwe, chui, nk. Dubai walichofanya ni kutengeneza kwa gharama kubwa mazingira kama ya Serengeti huko Dubai, kutia ndani na mito, misitu, miamba nk, na kuingiza wanyama kwenye mbuga hii "artificial savanna".
Baadhi ya picha katika Dubai Safari Park ni hizi
Lengo la UAE ni kuteka biashara ya utalii wa wanyama pori, hasa kutoka Afrika, ambayo ndio mshindani mkubwa wa Dubai Safari Park. Hivyo, kwa namna moja au nyingine, Serengeti ikifa, basi Dubai Safari Park itakuwa mdadala mkubwa wa Serengeti.
Athari ya kuchimba madini ndani ya Serengeti ni kuiua Serengeti, na siyo Serengeti tu, bali pia Masai Mara ya Kenya, kwa sababu Masai Mara ni sehemu ya Serengeti. Hivyo hili ni jambo ambalo litaathiri sana utalii wa wanyama pori Tanzania na Kenya, na atakaefaidika ni UAE na Dubai. Kwa hiyo basi, ni jukumu la Watanzania na ndugu zetu Wakenya kuungana na kukosoa na kupinga kwa nguvu zote uamuzi huu wa raisi Samia, kwamba hauna manufaa ya muda mrefu ya nchi zetu, bali manufaa ya muda mrefu ya Dubai. Madini yeyote katika Serengeti yakichimbwa, sana sana yatadumu kwa mika 20-30, na yatakapoisha hakutakuwa tena na Serengeti wala Masai Mara.
Kumbuka, mazingira ya utalii katika Dubai Safari Park ni ya kisasa sana, luxury, lakini bado hawajaweza kutoa ushindani mkubwa kwa Serengeti na Masai Mara. Sasa je, kuna mbinu za makusudi za kuziua Serengeti na Masai mara ili kusiwe na ushindani mkubwa kwa Dubai Safari Park?
Sasa ndio maana tunajiuliza, hili wazo la kuchimba madini katika mbuga ya Serengeti, ambalo kwa muda mrefu TANAPA wamelipinga kwa nguvu zote, ni la raisi Samia mwenyewe, au ushauri kutoka Dubai? Na mnafikiri nani atapewa mikataba ya kuchimba madini ndani ya Serengeti, kampuni toka Dubai? Je atachimba madini hayo kwa lengo la kutoathiri wanyama wa Serengeti?
Jambo hili kwa sasa linahusishwa pia na mabadiliko ya baraza la mawaziri la hivi karibuni, hususa kumuondoa Jerry Slaa katika wizara ya ardhi ambako ameonekana kama kero kwa baadhi ya watu kutia ndani "wawekezaji" toka nchi fulani fulani ambazo sitaki kuzitaja. Pia limemgusa Makamba wizara ya mambo ya nje. Je, wamekuwa kikwazo katika mipango kama hii ambayo inahusishwa na kuiua Serengeti na Masai Mara kwa manufaa ya Dubai?
Tukumbuke documentary ya TANAPA - Serengeti Shall Never Die, chini ya raisi yeyote wa Tanzania.
Kwa wale msioijua Dubai Safari Park bofya hapa
View: https://www.youtube.com/watch?v=us8Sl-w9n20