Kuna mdada ni mzuri sana, ila najishangaa sana kwanini sivutiwi nae kimapenzi

Kuna mdada ni mzuri sana, ila najishangaa sana kwanini sivutiwi nae kimapenzi

Balqior

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2021
Posts
2,406
Reaction score
8,039
Kuna mdada hapa mtaani kwetu, mimi namuona ana sura nzuri, Ana ngozi nzuri, mweupe, ana chura, halafu umri wake mdogo, tena hajaolewa, mpole, hana nyodo wala maringo, alikuwa anauza mgahawa wa mama yake, nilikuwa nikienda pale mara nyingi tu kunywa chai, namwona binti ni mzuri lakini hata sishtuki, wala hata nikilala usiku simwazagi, wala mara nyingi hayuko kwenye mawazo yangu, hata sipatagi hamu ya kumtongoza Au kumshobokea. Wakati vigezo vyote vya kimwili navyotaka toka kwa mwanamke huyo mdada anavyo, ni ajabu sana.

Cha kushangaza kuna baadhi wadada hapa mtaani wananivutia sana, Nawashobokea mno, nikiwaona roho yangu inafanya paah, ila kiuhalisia hawamfikii huyu binti mweupe kwa uzuri wa mwili hata nusu, sasa najishangaa ni uchawi au, it doesn't make sense kabisa

Kuna mtu asha experience jambo hili?
 
Haya mambo huwa hayalazimishwi japo nadhani binti tayari keshakukaa akilini ndo maana umekuja kufungua uzi. Kwa sasa waachie wenzio mpaka wewe na halmashauri ya kichwa chako mtakapokaa kikao na kufanya maamuzi yenu...[emoji16][emoji16]
 
Mkuu umelogwa mwamba umelogwa macho ya rohoni huna mkuu woooiiii do something
 
Huyo ndo unavutiwa nae sanaaa sasa sema huna tu ujasiri wa kumtongoza,,sidhan kuna mtu kamili anatoa sifa kibao kwa mwnaamke then anasema izo blah blah
 
Huvutiwi nae na Bado umeandika Uzi kumuhusu yeye..jipe muda
Hujanielewa, Sina haja ya kudanganya, au labda hii hali haijawahi kukutokea, unamuona mkaka mzuri ila hakushtui, ila akija Kaka mwingine Ana muonekano wa kawaida ila ukimuona roho inafanya paah, Kiukweli Sijavutiwa nae, nimeandika uzi kwasababu hio hali inanishangaza Yna2
 
Huyo ndo unavutiwa nae sanaaa sasa sema huna tu ujasiri wa kumtongoza,,sidhan kuna mtu kamili anatoa sifa kibao kwa mwnaamke then anasema izo blah blah
Sio kwamba sina ujasiri wa kumtongoza, hio hali haijawahi kukutokea ndo maana hunielewi brobiz
 
Hujanielewa, Sina haja ya kudanganya, au labda hii hali haijawahi kukutokea, unamuona mkaka mzuri ila hakushtui, ila akija Kaka mwingine Ana muonekano wa kawaida ila ukimuona roho inafanya paah, Kiukweli Sijavutiwa nae, nimeandika uzi kwasababu hio hali inanishangaza Yna2
Sio lazima kila kitu ule wewe mkuu, vingine waachie mafisi wasiochagua mfupa
 
Back
Top Bottom