KERO Kuna Mgao wa Maji maeneo ya Shekilango Dar? Kama Ndio, Tuambiwe Ukweli

KERO Kuna Mgao wa Maji maeneo ya Shekilango Dar? Kama Ndio, Tuambiwe Ukweli

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Wakazi wa NHC Shekilango, Ubungo, na maeneo mengine mengi tumekuwa tukikumbwa na tatizo kubwa la upatikanaji wa maji tangu mgao wa mwezi Desemba.

Kinachoshangaza ni kwamba zamani eneo la NHC Shekilango lilikuwa linapata maji kwa uhakika karibu kila siku. Leo hii maji yanaweza yasionekane kwa wiki moja au hata mbili bila maelezo yoyote kutoka DAWASA.

Tumewasiliana na huduma kwa wateja, tumefikisha malalamiko kwa viongozi mbalimbali, lakini majibu yanayopatikana ni ya jumla na hayaelezi kinachoendelea wala lini hali itaimarika.

Swali la wananchi ni rahisi: Je, kuna mgao wa maji? Kama upo, semeni wazi. Wananchi tunaweza kuvumilia changamoto za kiufundi au upungufu wa maji, lakini hatupaswi kuishi kwenye sintofahamu.

Tunachohitaji si ahadi zisizo na mwisho, bali uwazi. Tuambieni tatizo ni nini, linaathiri maeneo gani, na ni lini linatarajiwa kutatuliwa.

Mawasiliano ya wazi hujenga imani; ukimya hujenga malalamiko.

Wananchi tuna haki ya kupata huduma, na pale huduma inaposhindikana, tuna haki ya kupewa taarifa za kweli.
 
Back
Top Bottom