Tetesi: Kuna mgawanyiko mkubwa ndani ya CHADEMA kuhusu kuacha kuhudhuria vikao vya Bunge. Kuna fukuto la chini kwa chini

Hapo ndio namshangaa Mbowe anadai demokrasia wakati yeye ni dikteta

Watanzania tumuogope Mbowe
Hakuna wa kumpangia DJ chama ni mali yake ni Kama Sacco's tu yake hakuna wakuhoji ukienda kinyume na matakwa yake kufukuzwa uwanachama Kuna kuhusu ukiwa na bahati anakutenga Kama selasini
 
Bia yetu kada mtiifu alielisi mikoba ya Ritz na Lizabon kwa vyovyote mshahara wako utakua tofauti na kina magonjwa mtambuka.
 

Ni kweli Mbowe ni mbaya sana, kwanza yupo upinzzani, pili anatumiwa na mabeberu, hapaswi kumshirikisha kwa kuwa hataki kukubaliana na chama dola, ni mpinzani ni hatari kwa taifa kama usemavyo.

Kuna msemo ya kiingereza usemao, if you can help, don't hurt. Ukishindwa kuwasaidia usowadhuru....... Kiongozi yyt ana maswali ya kujibu kwa mungu wake, kuwa ulipotaka uongozi uliwsaidiaje watu uliowaongoza?!?!. Kwa alichokifanya Mbowe naamini atakuwa na jibu hata kwa mungu...
 
Mimi ni mleta Habari
Usihangaike kujieleza. Kuna watu wanadhani Mbowe ni mpigania uhuru na haki, bila kujua kwamba naye anaigiza kuwa ni rais wa nchi isiyojulikana. Hajitofautishi na rais wa nchi.

Sifahamu undani wa maelezo yako lakini kwa kuangalia tabia ya Mbowe, siyo ajabu kwamba anaamua bila kuwashirikisha wenzake. Tatizo anajiona kama anawamiliki watu ndani ya chama, wakati chama kimeishiwa pull. Hata Katibu wake simsikii tena kelele zake kama alivyokuwa anabwabwaja kabla ya kuteuliwa. Ni ishara ya kujionea ukatibu bandia.
 
Umemaliza
 
Hizo pesa wanazong'ang'ania za Vikao vya BUNGE watakufa wataziacha. Tulikuja duniani bila kitu hivi vitu tutaviacha hapahapa duniani. Mbaya zaidi, kwa hali ya sasa ukifa hata watoto wako watapata tabu sana kupata stahiki zako. UROHO WA PESA UTAWATOKEA PUANI.
 
Km bungeni hawazidi 500 wako hatarini vipi wanaopambana kariakoo

Acheni kudeka nyie Chadema
 

Huu muda wako ambao huwa unaupoteza mara kwa mara Kuijadili CHADEMA ungeutumia Kumshauri Mwenyekiti wako Taifa atoke upesi huko Mafichoni aje katika Mapambano ya wazi dhidi ya Janga hili HATARI la COVID-19 ningekuona wa maana mno. Na kuhusu Mgawanyiko kwa taarifa yako tu tokea Historia ya CCM hakuna Kipindi ambacho CCM imegawanyika Vipande Vipande huku Wanachama hasa Waandamizi wakihujumiana na Mwenyekiti wake Taifa akichukiwa na Wanachama wake kama hii CCM iliyo chini yake hasa ya kuanzia mwaka 2016 hadi sasa na pengine hata ile ya 2020 hadi 2025. Fanya Utafiti uamini.
 
Hata Katibu wake simsikii tena kelele zake kama alivyokuwa anabwabwaja kabla ya kuteuliwa. Ni ishara ya kujionea ukatibu bandia.
Kelele au hoja? Unataka kusema Mnyika anafanana na Kibajaji? Ukatibu Bandia kivipi?
 
Hayo ni mawazo ya kimasikini, yaani tusitafute kisa tutakufa?
 
Chadema wao wamezaliwa kubisha na kupinga
 
Wewe huijui Ccm au labda ni mtoto wa juzi
 
Wewe huijui Ccm au labda ni mtoto wa juzi

Uko sahihi na ni kweli kwamba CCM ya Magufuli si tu siijui bali siielewi ila nashukuru CCM ya Hayati Mwalimu naijua na ilinilea!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…