Gamba la Nyoka
JF-Expert Member
- May 1, 2007
- 7,036
- 9,331
Kwa sasa inaonekana kama kila kitu kiko shwari katika muungano wetu lakini Ukweli ni kuwa kuna ufa mkubwa sana ambao ni hatari kwa muungano na nchi kiujumla.
Ukweli wenyewe ni kwamba Katiba mbili, yaani ya Muungano na ya Zanzibar (toleo la mwaka 2010)vinakinzana na hivyo kupelekea mkanganyiko ambao hauna afya kwa nchi na hivyo ili kuondoa jambo hili ambalo ni serious lazima mabadiriko katika Katiba ya Zanzibar au ya Muungano lazima yafanywe ili kurekebisha hili tatizo
Vifuatavyo ni vifungu katika katiba ya Zanzibar ambavyo vinapingana waziwazi na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
1. Kipengele cha kwanza ni kuhusu Zanzibar kuwa ni nchi
Katiba ya Zanzibar ibara ya 1 imetamka kwa sauti kubwa kuwa ni NCHI na Imeainisha mipaka yake waziwazi
Ibara hiyo inasema hivi:
Kujitangaza huku kwa Zanzibar kuwa ni nchi haukuwemo kwenye toleo la kwanza la katiba ya mwaka 1984, Je ni kwa nini basi katika mabadiriko ya katiba hiyo toleo la 2010 Wazanzibar wakaamua kuiita Zanzibar kuwa ni nchi?
Wakati wazanzibar wakiutangaza Unchi wao na mipaka yao waziwazi kwenye katiba yao bado Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaendelea kutambua uwepo wa nchi moja tu iitwayo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mipaka ya hiyo Tanzania.
2. Ibara ya pili nayo ina contradiction, Katiba ya Zanzibar toleo la mwaka 2010 imetwaa Madaraka ambayo awali yalikuwa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kumpa rais wa Zanzibar. Awali kabisa, katiba ya JMT ilikuwa ikimpa rais wa JMT uwezo wa kuigawa Zanzibar katika mikoa na Wilaya kwa "kushauriana" na Rais wa Zanzibar lakini kwenye katiba ya Zanzibar, nguvu hizo kapewa rais wa Zanzibar kwa kufuata sheria zitakazotungwa na baraza la wawakilishi.
Ibara ya 2A ya Katiba ya Zanzibar toleo la 2010 inasema:
3. Katiba ya Sasa ya Muungano ibara ya 105(1)(b), Inatambua Muundo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wa Zamani, ambapo kuna cheo cha Waziri kiongozi na siyo muundo wa sasa wenye vyeo vya Makamu wa Kwanza na wa pili wa rais.
Hili siyo jambo dogo, maana ni ajabu uwe na kifungu cha katiba chenye kuelezea cheo ambacho hakipo!!. Kuacha ibara hii iendelee hivihivi kuwemo ndani ya katiba ja JMT wakati tayari Wazanzibar walisharekebisha muundo wa serikali yao maana yake inaweka hata question mark kwenye uhalali wa muundo mpya. Kunahitajika mabadiliko ya katiba ili kuweka jambo hili sawa!
4. Katiba ya Zanzibar ya toleo la 2010 inataka baraza la wawakilishi litunge sheria ya namna Wazanzibar watakavyoshiriki katika majeshi kwa ajili ya ulinzi wa Taifa
Kwanza tunajua kuwa kwa mujibu wa Katiba ya JMT, Suala la Majeshi ya Ulinzi wa Taifa ni suala la Muungano, Kwa muktadha huo, Sheria za Ulinzi wa JMT zapaswa kutungwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ninatambua wazi kuwa katiba ya Zanzibar haitumii neno Majeshi kuhusu vikosi vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, bali inatumia neno "Idara Maalumu". Wakati huohuo Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haitambui Mahali popote kuwa hizo Idara maalumu ni Majeshi ya Ulinzi wa Taifa!
Na Katiba ya nchi, yaani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepiga Marufuku kuanzisha Jeshi la Ulinzi kinyume cha Sheria ya bunge
Sasa swali la Msingi ni je?
(a). Hiyo katiba ya Zanzibar ilipotamka neno Majeshi ilimaanisha Majeshi gani?, kwa nguvu gani ambazo baraza la wawakilishi linazo juu ya majeshi hayo?
(b). Kama Kwa kutamka hilo neno "Majeshi" ilimaanisha idara Maalumu au vikosi Maalumu vya SMZ, Je Kamanda mkuu wa Vikosi hivyo ambaye kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ni rais wa Zanzibar sasa anaweza kuamuru vikosi hivyo kuingia vitani kuilinda Zanzibar?
Maana kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar toleo la 2010 rais wa Zanzibar ana mamlaka ya kuviagiza vikosi ya SMZ (idara maalum) kufanya shughuli(mission) yoyote atakayoona inafaa kwa ajili ya Maslahi ya Taifa (Zanzibar), pigia Msitari maneno SHUGHULI YOYOTE ATAKAYOONA INAFAA!
5. Katiba ya Zanzibar Imepoka Mamlaka ya Amiri Jeshi Mkuu.
Katiba Ya Zanzibar toleo la mwaka 2010 inatamka Vikosi Maalum ya SMZ kwa kutumia jina (Idara Maalum) na Imetaja Idara hizo kuwa Ni Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) na Jeshi la KMKM (Jeshi la Kuzuia Magendo) ba Idara ya Chuo cha Mafunzo(Magereza).
Na imetamka kwenye Ibara ya 123(1)Kuwa Rais wa Zanzibar atakuwa KAMANDA MKUU WA IDARA HIZO na Anaweza KUFANYA CHOCHOTE, pigia Msitari naneno KUFANYA CHOCHOTE kwa Ajili ya Maslahi ya Zanzibar, Sasa kama huu Siyo Uamiri jeshi mkuu ni nini?
Katiba hiyohiyo ibara ya 123(2) inasema kuwa Rais wa Zanzibar anaweza kuunda Idara nyingine yoyote atakayoona Inafaa na ANAWEZA KUIPA SHUGHULI YOYOTE ATAKAYOONA INAFAA KWA MANUFAA YA TAIFA. Pigia Msitari maneno "Shuguli yoyote", What if shughuli hiyo ikawa ni kupigana vita?
Sasa kama huu siyo uwezo wa Kuunda Majeshi kwa mgongo wa jina "Idara Maalum ni nini?"
6. Rais Wa Zanzibar akila Kiapo cha Kulinda Katiba ya Muungano (wakati wa kuapa kuwa mjumbe wa baraza la Mawaziri) na Akila Kiapo cha Kulinda Katiba ya Zanzibar anakuwa anaapa kufanya vitu vyenye contradiction
Tumeshaona, mahali ambapo katiba hizi mbili, Ya Zanzibar na ya Muungano zinapingana. Sasa ukiwa Rais wa Zanzibar ukaapa kulinda na kutetea vyote viwili, unakuwa unaapa viapo vyenye utata. Je utatekeleza kiapo gani kwanza pindi maslahi ya pande mbili yakikwaruzana?
7. Katiba ya Zanzibar toleo la mwaka 2010 Imepoka mamlaka ya Mahakama ya Rufaa ya Tanzania kuhusu uwezo wa Mzanzibari kukata rufaa katika mahakama ya Rufaa ya Tanzania kwa makosa yanayohusu uhuru na Haki za binadamu baada ya hukumu kuwa imetolewa na mahakama kuu ya Zanzibar.
Sote tunajua kuwa miongoni mwa mambo ya Muungano ni Mahakama ya Rufaa, hata hivyo katiba ya Zanzibar imemega mamlaka haya ya Mahakama ya Rufaa ya Tanzania kinyume cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Katiba ya Zanzibar inasema kwenye Ibara ya 24(3) kuwa:
Mwisho Kabisa
Wazanzibar Katika katiba yao toleo la 2010 kuna Mambo wameyawekea Kinga yasibadiishwe kirahisi, Mojawapo ni ZANZIBAR KUWA NCHI, Ukitaka Kubadilisha hili ni lazima Uitishe kura ya Maoni ya Wazanzibar, Sasa Jiulize kama hili itawezekana?
Kwanza Kipengele hiki peke yake Kinaua Ndoto hata ya CCM ya Serikali mbili kuelekea kwenye Serikali Moja
Kwa hiyo Ndugu Zangu, ni lazima tukubaliane, Hatuwezi kuwa na katiba mbili nchini zinazokinzana, Hatuwezi kuwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayotambua vyeo ambavyo Havipo, Hatuwezi kuwa na Katiba ya Zanzibar inayompa rais wa "nchi" hiyo uwezo wa kuunda vikosi na akavipa "MISSION YOYOTE" atakayoona Inafaa kwa Masilahi ya sehemu ya Nchi hiyo halafu tusiogope. What If mission hiyo ni kupigana vita dhidi ya "yeyote" anayehatarisha maslahi ya Zanzibar?
Kutokana na Hilo, TUNAHITAJI KATIBA MPYA itakayoondoa Mkanganyiko huu!
Hatuwezi kuendelea Kutegemea GOODWILL YA VIONGOZI kwenye kuudumisha huu Muungano,, Bali tunahitaji Mfumo wa Kikatiba na Kisheria Uliokaa sawa ili hsya mambo yaende vizuri, ili kesho na keshokutwa hata Marais wa Pande hizi mbili wasipotoka Chama Kimoja, Kila Rais ajue mipaka ya Majukumu yake Kikatiba.
KATIBA MPYA HAIEPUKIKI, TUNAWEZA KUJIFICHA KWENYE MCHANGA KAMA MBUNI TUKAJIAMINISHA KUWA KILA KITU KIKO SHWARI LAKINI SIYO KWELI.
TAIFA LINAHITAJI KATIBA MPYA!
Link ya Kupata katiba ya Zanzibar toleo la 2010 ni hii hapa chini:

"1. Zanzibar ni Nchi ambayo eneo la mipaka yake ni eneo lote la
Visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na Visiwa vidogo vilivyoizunguka
na bahari yake ambayo kabla ya Muungano wa Tanganyika na
Zanzibar ikiitwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar."

"2A. Kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli za Serikali, Rais
aweza kuigawa Zanzibar katika Mikoa, Wilaya na maeneo mengineyo
kwa kufuata utaratibu uliowekwa na sheria iliyotungwa na Baraza la
Wawakilishi"

"Rufaa dhidi ya uamuzi wa Mahkama Kuu katika Shauri lililofunguliwa dhidi ya Masharti ya sura hii ya Katiba yatasikilizwa na Mahkama Kuu mbele ya Majaji watatu bila ya kujumuisha Jaji aliyeamua shauri hilo mara ya kwanza. Majaji hao watatu watateuliwa na Jaji Mkuu na uamuzi wao utakuwa ni wa mwisho na hautokatiwa rufaa kwenye Mahkama ya Rufaa ya Tanzania"