Kuna Mgongano wa Katiba ya Zanzibar na ya Muungano, ufumbuzi wake tutake tusitake ni katiba mpya!

Vikosi vyote vya SMZ havina nguvu nje ya visiwa na hata hivyo huko Zanzibar kuna kikosi kamili cha jeshi la wananchi ambalo liko chini ya mabrigedia kutoka bara. Wewe unafikiri kwa hicho unachokiandika kama sio jeshi kuwepo huko pangetulia? Thubutu, haiwezekani.
 
Brother bado huelewi vitu, una think anticlockwise

Sent from my 5023F using JamiiForums mobile app
 
Brother bado huelewi vitu, una think anticlockwise

Sent from my 5023F using JamiiForums mobile app
Wewe ndio huelewi chochote kabisa na utaendelea kubaki na kilema hicho cha kukuelewa lolote asilani.

Kaamurishe basi hivyo vikosi vyako viende kinyume uone watafaywa nini na jeshi; hao ni sawa na Suma JKT au Mgambo, Katiba ya Zanzibar kutamka kwamba ni nchi haiwezi kusababisha wawe 'Soverign State'.

Hebu panuka ubongo
 
Wewe unazungumzia kwamba maadamu JWTZ ipo basi scenario ya Rais wa Zanzibar siku moja kuleta ukorofi kwa kutumia vikosi maalum vya SMZ (ambavyo katiba ya Zenji imempa power ya kuvitumia atakavyo) basi haitokuwepo!

Ukweli ni kwamba usidharau kikundi chenye muundo wa kijeshi, kina silaha za kijeshi, kina komandi za kijeshi na ukiachilia mbali hilo KINA wajibu wa KUFANYA LOLOTE Kitakachitumwa kufanya (Kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar).
Sasa tusingoje siku tuone JWTZ na Vikosi Maalum vya SMZ vinazichapa mchana kweupee kisa tu kuna Mkanganyiko katika katiba hizi mbili ambapo upande Mmoja kuna Mtu ni Amiri jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama kwa mujibu wa Katiba ya JMT na Upande wa Pili kuna Mtu kapewa powers na katiba ya Zanzibar Kuunda vikosi maalum kadri anavyooba inafaa na pia ana Powers za Kuviamrisha vikosi hivyo vifanye lolote!

Ndugu,, Jaribu kufikiria scenario tofauti tofauti ya haya nambo. Hiyo scenario unayoisema wewe ni BEST case Scenario ambapo tuna viongozi wenye busara kutoka pande mbili, na pia wanatoka chama kimoja, wanasikilizana na hivyo kila kitu kiko Shwari.

Sasa hebu fikiria WORST CASE Scenario, ambapo una rais wa Zanzibar aliyeamua kwenda na Katiba ya nchi yake, Akaamua kuunda vikosi maalum vyenye nguvu (katiba ya nchi yake ya Zanzibar inamruhusu), kwa hoja ya kulinda maslahi ya Zanzibar akaanza kupatrol mipaka ya bahari ya Zanzibar, kwa kufanya hivyo akahatarisha Maslahi ya JMT, Akaanza kugoma Mashauriano na Mwenzie wa JMT, Ikaamuliwa Ashughulikiwe Kijeshi na Yeye akaamua kuamuru vikosi vya SMZ vijibu Mapigo, Wakati huohuo kama alivyosema Mchangiaji mmoja huko Juu Wananchi wa Zanzibar wakaamua kusimama na Rais wao, Huoni hapo tayari hii itakuwa Vita ya wenyewe kwa wenyewe?
 
Hatuhitaji katiba mpya kwa sasa iliyopo inatosha,period. Nguvu zetu wote tuzielekeze kwenye kuwa-letea wananchi maendeleo.Tuungane wote katika hili.
After all mwananchi wa kawaida hana habari na katiba mpya,what he/she wants is a better life.
Maneno ya wanafiki.
 

Tujadili huku tuliko toka, ndio msingi wa Muungano wetu. Kumefanyika hadaa nyingi kuidhoofisha Zanzibar nje ya Muungano na Ndani ya muungano huu, huu muungano hakuna alie mkubwa wala mdogo, nchi zote ni Equal, hamtaki basi sisi tutaendelea kuhoji uhalali wake na kumetumika sheria zipi za kimataifa mpaka kubadili jina la Muungano wetu , mpaka kumuondoa Rais wa Zanzibar umakamo wa Rais, mpaka kuifuta Tanganyika.
 
Maneno ya wanafiki.
Wanafiki ni wale wanaotumia siasa ili waonekane wanawajali wananchi,kumbe ni wachumia tumbo fulani tu.

Kwanza Waafrika hatuna asili ya written constitutions,mta-copy na ku-paste mpaka lini? Kama written constitutions zingekuwa muhimu, kwa kiwango
mnnacho-aminishwa na mabeberu,si Britain
wangekuwa na a written constitution, mbona hawana na wao ni mabeberu!Don't you find this queer?Amkeni jamani,mbona mnaingizwa mkenge kirahisi hivyo?

Other countries with unwritten constitutions
are Canada, Israel, Libya, New Zealand, Oman and Saudi Arabia.
 
Hao unaowataja walishakuwa wastaarabu katika mifumo yao ya utawala na uongozi . WaAfrica na especially Tanganyika ustaarabu bado zero. Bila kuwa na muongozo imara tutakuwa na kina Trump wa kiAfrika wa kutaka kufia madarakani.

Tumeona Mugabe akitaka afie madarakani , Ccm wakijinasibu kuongeza muda hata kama kiongozi hataki !!. So Africa na especially Tanganyika inahitaji katiba ya wananchi dhidi ya watawala
 
Tumeanza kuamka baada ya kuona Marais wote ni wazanzibar, Na kutokana na katiba ya 2010 kwamba Zanzibar ni nchi hapa panaleta ukakasi ,
 
Nyerere alikuwa smart sana lakini viongozi waliofuata baada ya Nyerere walikuwa wajinga sana.

Mpaka sasa tungekuwa tumeshafikia serikali moja na hizi chokochoko za uzanzibar na tanganyika zisingekuwepo.

Leo hii mambo vururuvururu tu.

Cha kukurekebisha tu suala la tawala za mikoa na serikali siyo suala la Muungano hivyo ni sahihi katiba ya Zanzibar kumpa mamlaka rais wa Zanzibar kufanya hivyo.
 
Sijui kwa nini mnapenda kunyooshea vidole nchi zenu na ninyi mnakaa humo humo.Kilichotokea Marekani November 2020 katika uchaguzi wa kishenzi kabisa kuwahi kutokea katika historia ya Marekani ulikiona,au kwa kuwa kilitokea Marekani sio shida.

Na yanatokea Canada na Australia unayajua?Na Malkia wa Uingereza je,ana-chaguliwa na nani,si amejipachika tu.Na hapa nimetaja nchi moja tu ya Ulaya yenye Kingship na Queenship,ziko nyingi.Unajua kwa nini system hiyo ipo?Acheni kushabikia vitu ambavyo hata hamvielewi.
 
Ikishindikana hiyo Katiba Mpya, basi wajitenge tu na hivyo kujitegemea kwa kila kitu! Natamani pia kuona siku moja na sisi tukijivunia Utanganyika wetu.
Ni hatari mno kwa Zanzibar kujitenga sana sana urithi pekee tutakaowaachia wajukuu zetu ni kuhakikisha Zanzibar inakaliwa na watanganyika tu.
 
Hao ni wehu wa ccm achana nao sisi tunaitaka Tanganyika na Zanzibar zenye usawa hatutaki Tanganyika ipotee halafu zanzibar iwepo huo sio Muungano
Kinachotakiwa ni kupigania Tanzania moja na siyo kuwa na kakipande sehemu.
 

Nyerere alikuwa Smart lakini Maalim Seif naye alikuwa Smart sana.
Maalim pamoja na kuwekewa Figisu na CCM nyiiiingi na kwa miaka mingi lakini kwa kushirikiana na Karume Jr alifanikiwa kuwabeat CCM at their own game kwa kuja na katiba ya Zanzibar toleo la 2010.

Hii katiba ya Zenji ya 2010 ni bonge la ushindi kwa Wazanzibar katika jitihsda zao za kufungua vifungo vya koti la muungano.

Naamin, CCM walijaribu kumfrustrate Maalim kwenye uchaguzi wa 2020 lengo lao likiwa asuse ili waende wakaibadili hii katiba ya Zanzibar, maana walihakikisha wanajipa Wajumbe wa baraza la wawakilishi wa kutosha kwelikweli, Maalim akaona isiwe tabu ngoja awe sehemu ya serikali!. Siamini kama ni kwa Interest ya Hussein Mwinyi kuitisha mabadiliko ya Katiba ya Zanzibar na kubadili vipengele vya katiba hiyo kwa sasa.

Tukubali tu, The only way ya kucounter move ya Wazanzibar ya mwaka 2010 ni kutengeneza Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kinyume cha hapo mgongano wa katiba hizi mbili zilizopo sasa ni time bomb kwa mustakbali wa muungano
 
Hatuhitaji katiba mpya kwa sasa iliyopo inatosha,period. Nguvu zetu wote tuzielekeze kwenye kuwa-letea wananchi maendeleo.Tuungane wote katika hili.
After all mwananchi wa kawaida hana habari na katiba mpya,what he/she wants is a better life.
Unaletaje maendeleo wakati nikiwa na Bidhaa zangu kutoka zanzibar zikija Bara zinatozwa kodi mara ya pili?
Sukari kutoka Zanzibar kuja bara ni marufuku?

-Eti muungano na maendeleo , Serikali ya Zanzibar hairuhusiwi kuomba misaada ya nje kuijenga Zanzibar, na ikimpata mfadhili ,ni mpaka Muungano waridhie ndio apewe msada huo tena kwa mashartiya Kuigawabara % ya huo msaada,?

-Unasemaje Katiba iliyopo inatosha huku wazanzibari waliokimbizwa na mapinduzi wakitaka kurudi nyumbani hawakubaliwi na Tanganyika hata zanzibar yenyewe inawatamani warejee?

-Suala la Uraia kuwa Moja ni Msiba mkubwa Kwa Znzibar, kwani raia wa Zanzibar si Raia wa Tanganyika, kwa hiyo Tanganyika ndiye anaamua yupi awe raia na yupi asiwe?

TUNAHITAJI KATIBA MPYA ILI TUWE A MUUNDOMPYA WA MUUNGANO.
 

Na chengine anachoshindwa kufahamu, ndani ya hilo jeshi la JWTZ muna wazanzibari wengi tu, kwa Scenario kama hiyo ni wazi kuwa most of them wataliasi JWTZ na kuungana na Raisi wa Zanzibar.
 
Suluhisho la kudumu ni kuanzisha effective assimilation policy ambayo within 50 years itakuwa imeshafuta uzanzibar na kubaki na Tanzania tu.
 
Huyo anavuta bangi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…