Kuna Mgongano wa Katiba ya Zanzibar na ya Muungano, ufumbuzi wake tutake tusitake ni katiba mpya!

Ni hatari mno kwa Zanzibar kujitenga sana sana urithi pekee tutakaowaachia wajukuu zetu ni kuhakikisha Zanzibar inakaliwa na watanganyika tu.

Sasa huo Udikteta ulionao ndani ya nafsi yako utakusaidia nini mkuu? Wewe unataka kuwa huru lakini mwenzio umtawale au sivo?
 
Hadi HII LEO HAKUJA FANYIKA ''CONSTITUTIONAL ASSEMBLY'' yaani Bunge la katiba.
La kwanz ni lile la Kikwete la Katiba ya Warioba ambalo lilikufa kifo cha mende. CCM walilijhodhi na kupindua meza.
 
Kinachotakiwa ni kupigania Tanzania moja na siyo kuwa na kakipande sehemu.

Hilo jambo haliwezekani mkuu, Watanganyika hawataki kutawaliwa na MZanzibari, na Wazanzibari hawataki kutawaliwa na watanganyika. Hiyo moja itapatikanwa vipi?
 
Suluhisho la kudumu ni kuanzisha effective assimilation policy ambayo within 50 years itakuwa imeshafuta uzanzibar na kubaki na Tanzania tu.
Nyerere alichelewa.

Hiyo ilitakiwa pale Mzee Karume aliposema tuwe na nchi moja "wewe rais mimi makamo" palepale Nyerere alitakiwa kuseize moment, sasa yeye akawa na wasiwasi kuwa akikubali idea hiyo ataonekana kaimeza Zanzibar, eti ataonekana mkoloni mpya.
Instead Nyerere akaopt kwenye long game, yaani kuimeza Zanzibar mdogomdogo, Hii plan imefeli baada ya muafaka wa Karume na Seif

Lakini sasa hivi huwezi hata kwa mabomu ya nyuklia kuwafanya Wazanzibar waikane autonomy yao, Never!
 
Katiba hazina mgongano bali kknachopaswa kufanyika Ni UPDATE kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili ku-accomodate maboresho ya liyofanyika kwenye Katiba ya ZNZ ya 2010.
 
Kwani Katiba inasemaje kwenye hiyo Act of Union and Article of Union?
 
Katiba hazina mgongano bali kknachopaswa kufanyika Ni UPDATE kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili ku-accomodate maboresho ya liyofanyika kwenye Katiba ya ZNZ ya 2010.

Duh, Sasa wewe ndo umetuchanganya moja kwa moja.

Sasa kama katiba haijawa updated ili kuendana na mabadiliko ya Zanzibar huko si ndo kugongana kwenyewe?
Au unafikiri hiyo Update itafanyika kwa kutype tu upya hizo updates bila kikao cha bunge cha mabadiliko ya katiba kufanyika na kufuata process yote ya mabadiliko ya katiba?.

Ni mpaka mabadiliko hayo yafanywe kupitia upigaji wa kura bungeni na zipatikane theluthi mbili ya Wabunge wa Tanganyika na Theluthi mbili ya wabunge kutoka Zanzibar wapitishe mabadiliko hayo hapo ndipo mkanganyiko huu utaondoka, bila ya hivyo hizi katiba mbili kwa sasa zinapingana
 
Asante Mkuu kwa maboresho. Tuko pamoja

And kwa maneno yako hayo ndipo Rasimu ya Katiba ya Warioba inapokuwa very RELEVANT at this moment in time
 
Hizi ni choko choko tu zenye nia ovu ya kuleta migongano isiyo ya lazima kwenye nchi yetu.Wananchi wa kawaida wala hawana tatizo na mfumo wa muungano wa sasa.Ninyi mlio kwenye payroll ya mabeberu ninyi,ndio mnaotuletea shida.Mnachofanya ni kuwa-instigate Watanzania:Tanganyika na Visiwani,ili waone kwamba serikali zao haziwatendei haki.This is dissent,which if not properly handled could in collaboration with other issues,lead to revolt by the citizenry.Kuweni makini sana.
 
Mkuu umenifumbua macho sasa nimeamini hatuna muungano Bali tunamgongano
 
Kwa sasa Zanzibar inaendeshwa na aina ya serikali ambayo muundo wake hautambuliki katika katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katiba ya Zanzibar inapubgana na katiba ya JMT

Tunahitaji katiba mpya yenye kuondoa mtanzuko huu!
 
Tunahitaji katiba mpya ili kuondoa mgongano wa katiba ya JMT na SMZ
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…