Kuna movie inayotisha zaidi ya 'The Conjuring'?

Kuna movie inayotisha zaidi ya 'The Conjuring'?

HumbleBoy98

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2020
Posts
387
Reaction score
396
Habari zenu wadau wapenda movies hasa zile za kutisha.

Hivi juzi Kati hapa nilicheki movie inayoitwa 'the conjuring', nilicheki sehemu ya Kwanza na ya pili.

Hii ni baada ya kupata habari zake humu JF kwamba inatisha Sana na kilichonivutia zaidi kutaka kuzicheki hizi movies Ni kwasababu they are based on true story!

Hivyo nikawa curious kujua Nini kilijiri coz ninachoamini Ni kwamba wenzetu wa dunia ya Kwanza Mambo ya uchawi na ushirikina hayapo Sana Kama sisi waafrika.

Mazee hizi movie zinatisha aisee hasa ile sehemu ya pili inayohusisha ule mzimu unaoitwa 'valak' (hii sehemu ya pili nilivyomaliza kuangalia nikawa naogopa hata kwenda toilet kukojoa maana ilikuwa saa nane usiku afu Giza kinoma the conjuring sio mchezo mazee)

Nimevutiwa Sana na jinsi directors wanavyopangilia matukio na kufanya usisimke na kuogopa pia, na hata story yake inasisimua Sana kwani mwisho wameweka Picha za wahusika halisi Kama Ed & Lorraine Warren halisi kabisa waliokuwa wanafanya kazi ya kupeleleza matukio yasiyo ya kawaida (paranormal investigators)

Mpaka saivi najiuliza hivi kweli mtu unaweza ukawa na kipawa Kama Cha bi Lorraine Yani 'clairyvoyant'? Lakini kwa mujibu wa story Ni kwamba alikuwa hivyo kweli.

Sio hivyo tu, mwisho wanaonyesha mpaka Picha ya yule mtoto Janet aliyekuwa possessed na ule mzimu akiwa ana elea hewani (levitate) kiukweli ukweli kabisa yaani tukio lenyewe halisi lilivyonaswa kwenye camera achana na ile Picha ya kwenye movie, nilishangaa Sana!

Sasa nilikuwa nauliza wadau wa hizi makitu Kama kuna movie nyingine yoyote inayotisha zaidi ya hizi za the conjuring nipakue fasta nicheki maana siku hizi sijui nimekuwa na akili gani nimejikuta Napenda tu movie za kutisha.

Horror movies ambazo mpaka Sasa nishazicheki Ni hizi hapa chini:
The Conjuring 1&2
The Nun
IT (hii nimecheki chapter 2 tu)
SAW 3D
Final destination 1-3
Wrong turn 1, 2, 4 &5

Ila Kati ya hizo zoote hakuna niliyotokea kuielewa Kama the conjuring.

Sasa wadau Nani anajua movie nyingine yoyote inayotisha zaidi ya the conjuring na yenye story ya kusisimua zaidi?

Afu Kuna kipindi nilionaga mdau humu jf anasema the conjuring sehemu ya tatu IPO njiani vipi ishatoka?

Karibuni wazee
 
Ni kitu kizuri, tena zima taa, it's exciting alot
Na ndo nilivyofanya mkuu ila nilivyomaliza nilitamani kujuta 😆
Maana mkojo ulikuwa umenibana ila nikifikiria toilet kulivyo Giza saa nane usiku nahisi Kama nitakumbana na valak huko😂😂
Ukitaka upate msisimko wa horror movie cheki usiku na taa uzime ndo utapata ile feeling yenyewe.
 
ni nini nijitese bure niangalie movies za kutisha ili nigundue nini??
Kama unajijua huwezi Bora uachane nazo tu mkuu😀
Maana unaweza hata kuzimia ila kwa sisi wengine ni burudani na Wala sio kujitesa.
Sema jaribu tu mkuu siku Moja ucheki hata SAW 7 hivi utest feeling yake😎
 
Na ndo nilivyofanya mkuu ila nilivyomaliza nilitamani kujuta 😆
Maana mkojo ulikuwa umenibana ila nikifikiria toilet kulivyo Giza saa nane usiku nahisi Kama nitakumbana na valak huko😂😂
Ukitaka upate msisimko wa horror movie cheki usiku na taa uzime ndo utapata ile feeling yenyewe.
afu uweke na sauti kubwa...
maana bila sauti hutaogopa
 
Mie napenda horror film kama izo the conjuring.

Lkn film kama SAW au wrong turn (thriller) zisipendi. Mambo ya kuona scenes za damu damu kama vile sichukui. Na utuuzima huu ndio kabisa
😄😄
Mara watu wanapasuliwa vichwa na na magreda Yale ubongo Unaruka huko na huko wazungu sijui wanafikiriaga Nini kutengeneza muvi Kama hizo mi mwenyewe sivutiwi nazo kivile
 
Hebu jaribu kizitazama hizi hapa:

1) The Amityville Horror
2) Evil Dead (mpya)
3) Dead Silence (2007)
4) Drag Me to Hell
5) The Ring (1,2 na 3)

Pia, ukipata muda usisite kutupatia mrejesho!
Sawa mkuu Asante ngoja ntazipakua zote nijionee😎😎
 
Fanya ucheki “The grudge” bonge ya horror pia hiyo The nun ni nouma mkuu
Asante mkuu nishai add kwenye list.
The Nun nayo Ni noma afu Sasa story yake inahusiana na the conjuring 2 maana mzimu ule ule wa kwenye the conjuring 2 ndo huo huo wa kwenye The Nun.
 
Vipi kuhusu sehemu ya tatu ya the conjuring wadau ishatoka au bado?
 
Back
Top Bottom