Kuna Mtanzania bado anaamini nchi hii ni masikini na inahitaji misaada zaidi kujikwamua?

Sasa kwanini aliuliwa?
Unamuua vipi mtu unaacha kuuwa kitabu chake,hizi dhana za killing ni muendelezo wa propaganda za enzi za vita baridi Mrusi akiwa engineer wa propaganda.
 
Umasikini wa Tanzania unazidi kuongezeka kila siku, hii ni kutokana na wananchi kuendelea kudanganywa kila siku.

Utajiri wa mali asili ni mkubwa rasilimali watu ni nyingi mno, akili kisoda za viongozi wetu ndio tatizo.

Viongozi wetu wanashindwa kutambua au wanaviacha makusudi vipaumbele vinavyoweza kumuinua mwananchi mmoja mmoja na kulifanya taifa liinuke jumla.

Hili linaweza likawa ni mpango wao ili waweze kuendelea kututawala milele maana masikini anatawaliwa kwa urahisi sana.

Viongozi wetu wanaogopa wananchi wanaojitambua.

Jingine ambalo naliona ni la kijinga pia ni kuacha kutatua matatizo ya nchi na kuanza kushindana na mataifa mengine, ili tuonekane nchi tajiri ni upumbavu tu.
 
Msema kweli tume huru ndiyo itakayo amua mbivu na mbichi, achana na hii ya ccm inayojipigia kura vichochoroni, ccm haijawahi kushinda uchaguzi na haitakuja kushinda,
CCM ilishinda kwa kura halali na kwakishindo mwaka 2005 na 2020.
Chaguzi zingine sina hakika sana
 
CCM ilishinda kwa kura halali na kwakishindo mwaka 2005 na 2020.
Chaguzi zingine sina hakika sana

2020 moja kati ya chaguzi za hovyo kuwahi kutokea duniani mpaka Mungu akaamua kuingilia kati
 
Wewe endelea kuwaita watu waenda kuzimu mimi nakwambia nchi hizi za kiafrika zimejaa watu wapumbavu wasio na ujasiri kazi yao kulamba watu makalio.Unafikiri hizo doll milioni 700 ni hela ya kukufanya ujikomboe? Ukombozi unaanzia kwenye fikra! Lazima update umasikini nao utakukimbia! Ila viongozi wote walio ukataa umasikini kama akina na Sankara na watu wengine wazalendo wa kiafrika walionekana hawana maana! Mwisho wa siku kuambulia kupata viongozi wapumbavu na wazurulaji tu!
 
Real,unakuwa na kiongozi anaona sifa kualikwa Ikulu ya America na ulaya
 
Unamuua vipi mtu unaacha kuuwa kitabu chake,hizi dhana za killing ni muendelezo wa propaganda za enzi za vita baridi Mrusi akiwa engineer wa propaganda.
Unahitaji maombi ya kiroho haswa
 
Umsema ukweli,lakini watakuja kukupinga maadui wa ukweli
 
Tanzania sio masikini ila huyo unayejaribu kumpamba ndio masikini pamoja na wewe. Mnaoamnini umasikini unaondoka kwa slogani na maneno matamu matamu. Hebu nikuulize kitu?
1. Anayewaita watu wanyonge huku akisema nchi yao ni tajiri anaelewa anachosema kweli? Toka lini mwenye utajiri akawa mnyonge?
2. Magufuli kafanya lipi la ajabu ambalo watangulizi wake hawakufanya?
3. Kama Magufuli kaacha kutegemea misaada mbona katika kipindi chake deni la nje limekua kwa kasi kuliko watangulizi wake?

Narudia tena Tanzania sio masikini ila wwwe na unayejaribu kumpamba ndio masikini wa kutupwa. Mnachoongea na takwimu haviendani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…