Kuna mtu anaweza kuniambia faida za Wabunge Tanzania?

Tangu mambo yalipopelekea nchi ikawa na bunge la chama kimoja halafu hata hao waliopita wakawa hawana uhakika wa kurudishwa na wengine wakawa na uroho wa kutaka teuzi hali iliyopelekea kutengeneza kila mmoja kuwa chawa kwa malengo yake, kila kitu kimejitenga.

Nakuhakikishia, bila bunge, wakuu wa wilaya, wakuu wa mikoa nchi hii itapata maendeleo makubwa sana

Haya makundi yalipaswa kuisaidia serikali na endapo yangetimiza majukumu yao ipasavyo kama yalivyoandikwa kwenye job description zao, hakika nchi ingepiga hatua. Lakini imekuwa kinyume chake, muda wote, saa zote, miaka yote wanalinda na kuficha uzembe na uozo wa serikali badala ya kuuanika hadharani ili ufanyiwe kazi

Haya makundi ndio yanaongoza kwa uchawa, kujipendekeza na kuipotosha serikali kwa kuficha udhaifu wa serikali

Yakiondolewa haya makundi kwenye mfumo wa nchi yetu, nchi itabaki na wataalamu watakaotenda kwa kuzingatia weledi
 
Inawafanya wahisani waendelee kuipa Serikali hela kwa kuamini kuwa kuna demokrasia.
 
Kumaliza hewa safi Dodoma
 

Kwetu Ngara mbunge anafanya kazi ngumu sana ya kusogeza bajeti kuu karibu na wananchi.

Umeme umefika, barabara zinaendelea kujengwa. Siasa pana za kitaifa zinayo majukumu ambayo ni tofauti na haya mawazo ya kitoto unayojaribu kuyawakilisha humu jamvini.
 
Kugonga meza,uchawa tu
Hawako kwa ajili ya wananchi

Ova
 
wabunge wetu hawawezi kuwa na meno na sababu inafahamika vizuri sana ni katiba ya nchi imewafunga kwani katiba yetu imetamka kuwa ikiwa Mbunge akifukuzwa uanachama na chama chake basi na ubunge wake nao utakoma..isitoshe mkuu wa mhimili wa serikali ndie pia mwenyekiti wa chama chake..ili wabunge wapate mamlaka yao kamili basi iwe chama kikimfukuza hakitaadhiri ubunge wake hapo kidogo watajitutumua kuliko hii ya sasa ubunge kumilikiwa na chama na kinaweza kuuchukua ubunge huo mda wowote...maana inajulikana huku afrika kupata mamlaka,cheo na madaraka sio kwa ajili ya kuwatumikia watu bali ni umepata fursa na ulaji kwahiyo kila mtu anaangalia maslahi hakuna atakaekubali kupoteza ulaji wa maslahi manono..hivyo bila wao kupenda mfumo umewashape wawe hivi tunavyowaona walivyo huko bungeni ni useless kabisa
 
Bunge la sasa halina faida yoyote kwa wananchi ni heri Mungu awapende zaidi
 
Binafsi kwa sasa sioni,hasazaidi ndani ya miaka 10 ,13 ya hivi karibuni hata lisipo kuwepo naamini inaweza kuwa faida zaidi kwani katika mazingira hayo itajitokeza mifumo mingine iliyobora kuliko hii iliyoonyesha kishindwa kulisaidia taifa,hata kama itakuwa ya shida na mateso,ila itawezakusaidia kutoka tulipo kwamishwa.
 
Kuhudhuria mazishi ya viongozi
 
Hakuna faida ya wabunge. Wafutwe tu
 
Kwa huu ulimwengu wa teknolojia hakuna umuhimu wa bunge popote pale duniani. Sio Tanzania tu. Kuhusu bunge kutunga sheria ni uongo mtupu. Mbunge wangu aliyeishia darasa la 7 anatunga sheria gani? Kama ni uwakilishi wa matatizo ya wananchi siku hizi hata mtu aliyeko Mara anaweza jua kinachoendelea Mtwara. Kama ni maoni ya wananchi kuhusu sheria ziwe zinawekwa tu online watu watoe maoni yao.
 
Pale ni kutimiza takwa la Katiba tu, kwa vile imesema tuwe na bunge. Ukiondoa hapo hakuna faida yeyote. Nchi inaingia gharama bure kabisa
Museveni alitokea pahala akoweka rula, Uganda ipo pazuri. Hapa Tz kuna haja aje mnyosha rula, kwa kipindi hicho cha kunyosha rula hakuna bunge na fungu la bunge liende kwenye huduma za kijamii. Kwan kuna siku Museven atashtakiwa kwa kosa la kupindua serikali. Najiuliza hili swali
 
Mkuu uneona nchi za kuiga mfano ukaona Uganda? We utakwa mnyarwanda😅😅
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…