Hivi kama mume wako anakupenda na kukujali kwa kila kitu kisha huko nyuma hukuwa mwaminifu na ukakubali na akakusamehe. ukarudia tena mara 2 au tatu na akakuonya na kukusamehe. Je akikukukuta tena una mahusiano nje ya ndoa akufanye nini?
Mbarikiwe sana.
Nimesahau kuanza na Salamu, ila nina Imani nyote hamjambo. Karibuni kikombe cha chai hapa. Haya tunaomba msaada wa mawazo wapendwa.
Kama hatajua la kufanya atakuwa ni amefikia TBS hadi kufanana na Yesu ambaye alimsamehe Petro hata baada ya kumakana mara 3.
Babu DC, mwenzio anampenda mke wake, lakini ndo hivyo huyo bibie anashindwa kuacha hiyo tabia.
Kwani babu unadhani usingeweza kusamehe mara zote hizo?
Duh We mtakatifu, lakini ninyi mnasamehewa jamani.Ana bahati kusamehewa mara ya kwanza....ilikua ni straight red card.....
Kwa nini unaona hivo Mery, kwani huyu mwanamke hakustahili huo msamaha??
Mara ya 3 bado tu uendelee kusamehe haiwezekani kabisa inahitaji moyo mgumu kama chuma ama uwe umelishwa limbwata. Inaniuma sana nikifikiria...
Mi naona aendelee kumsamehe tu :crazy:..mhh!na ana moyo!!!kama alimsamehe mara zote hizo na wakaendelea vizuri..why not now?
mbona wanawake huwasamehe wanaume mara nyingi tuu.
sasa zamu yao,kibaya ni kwamba huyo ndo amebeba msalaba wa wote.
Amsamehe tena maisha yaendelee