Kuna mtu kaniuliza hili swali jamani, anataka msaada wa Mawazo yenu. Maji yamemfika shingon

LD

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2010
Posts
3,014
Reaction score
578
Hivi kama mume wako anakupenda na kukujali kwa kila kitu kisha huko nyuma hukuwa mwaminifu na ukakubali na akakusamehe. ukarudia tena mara 2 au tatu na akakuonya na kukusamehe. Je akikukukuta tena una mahusiano nje ya ndoa akufanye nini?

Mbarikiwe sana.
Nimesahau kuanza na Salamu, ila nina Imani nyote hamjambo. Karibuni kikombe cha chai hapa. Haya tunaomba msaada wa mawazo wapendwa.
 
  • Thanks
Reactions: RR
Ndo madhara ya huruma hayo mara tatu na bado unaomba msamaha na anakusamehe?????!!!!

Kwa heri mwalimu
 
Dah Desidii, unasema je dada angu, manake hapa, ndo tunavaa uhusika wa mwanamke sasa.
 
Hivi kama mume wako anakupenda na kukujali kwa kila kitu kisha huko nyuma hukuwa mwaminifu na ukakubali na akakusamehe. ukarudia tena mara 2 au tatu na akakuonya na kukusamehe. Je akikukukuta tena una mahusiano nje ya ndoa akufanye nini?

Mbarikiwe sana.
Nimesahau kuanza na Salamu, ila nina Imani nyote hamjambo. Karibuni kikombe cha chai hapa. Haya tunaomba msaada wa mawazo wapendwa.

Kama hatajua la kufanya atakuwa ni amefikia TBS hadi kufanana na Yesu ambaye alimsamehe Petro hata baada ya kumakana mara 3.
 
Ana bahati kusamehewa mara ya kwanza....ilikua ni straight red card.....
 
mara tatu nadhani huyo mwanaume ana mapungufu katika kufanya maamuzi mazito
 
Babu DC, mwenzio anampenda mke wake, lakini ndo hivyo huyo bibie anashindwa kuacha hiyo tabia.
Kwani babu unadhani usingeweza kusamehe mara zote hizo?
 
Hivi LD unamaanisha huyu mke keshafumwa mara ya tatu au ndo anatafuta ushauri ili afumwe mara ya 3?
 
Ana bahati kusamehewa mara ya kwanza....ilikua ni straight red card.....
Duh We mtakatifu, lakini ninyi mnasamehewa jamani.
Hata kosa la kwanza hakutakiwa kusamehewa?
Mi nafikiri tatizo la huyu bibie ni ile tabia ya kurudia rudia hili kosa.
Sasa we mtakatifu, mwenzio hajui aanzie wapi kumuacha mtu anayempenda.
 
Hivi LD unamaanisha huyu mke keshafumwa mara ya tatu au ndo anatafuta ushauri ili afumwe mara ya 3?

Yani huyu bibie kashafumwa kaka angu.
 
Kama amemsamehe mara zote hizo na akarudia nadhani sasa basi. Ukimkamata tena mpe red card. Kinyume na hapo atakuletea gonjwa na kwa Babu loliondo dawa hairudiwi.
 
mara tatu nadhani huyo mwanaume ana mapungufu katika kufanya maamuzi mazito

Kwa nini unaona hivo Mery, kwani huyu mwanamke hakustahili huo msamaha??
 
Mi naona aendelee kumsamehe tu :crazy:..mhh!na ana moyo!!!kama alimsamehe mara zote hizo na wakaendelea vizuri..why not now?
mbona wanawake huwasamehe wanaume mara nyingi tuu.
sasa zamu yao,kibaya ni kwamba huyo ndo amebeba msalaba wa wote.
Amsamehe tena maisha yaendelee
 
Kama amemsamehe mara zote hizo na akarudia nadhani sasa basi. Ukimkamata tena mpe red card. Kinyume na hapo atakuletea gonjwa na kwa Babu loliondo dawa hairudiwi.

Asante Mhache!!!
 
Kusamehe inataka moyo na ni kwa neema ya MUNGU mtu unaweza kusamehe. kwa fikra za kibinadamu ni ngumu hata kama unampenda mke kwa kiasi gani inafika mahali atashindwa kama hatabadili tabia
 
Mara ya 3 bado tu uendelee kusamehe haiwezekani kabisa inahitaji moyo mgumu kama chuma ama uwe umelishwa limbwata. Inaniuma sana nikifikiria...
 
Kwa nini unaona hivo Mery, kwani huyu mwanamke hakustahili huo msamaha??

LD mara tatu?? Huyo mwanamke wa aina gani asokuwa na soni usoni mwake??
Kapata mwanaume mpole lakini aangalie "Ukiona Kobe kainama................................."
Atakuja mfanyia kitu mbaya hakutarajia hivi kwa akili yake kabisa anamuona huyo mwanaume ni mwehu kumsamehe samehe tu
Hapo kuna jambo litampata tena si dogo
 
Mara ya 3 bado tu uendelee kusamehe haiwezekani kabisa inahitaji moyo mgumu kama chuma ama uwe umelishwa limbwata. Inaniuma sana nikifikiria...

Kama wewe hapo swala kama hili ungefanya je AK-47?
Ok huwezi kumsamehe, sasa ungefanya je? Unampa Talaka, Unamfukuza kama Mbwa, unamrudisha kwao au unafanya je?
 
Mi naona aendelee kumsamehe tu :crazy:..mhh!na ana moyo!!!kama alimsamehe mara zote hizo na wakaendelea vizuri..why not now?
mbona wanawake huwasamehe wanaume mara nyingi tuu.
sasa zamu yao,kibaya ni kwamba huyo ndo amebeba msalaba wa wote.
Amsamehe tena maisha yaendelee

Ni kweli aendelee tu kumsamehe tena amake sure account yake ya msamaha bado ina balance ya kutosha kwa ajili ya next msamaha kwani huyu dada anaonekana hiyo ndio tabia yake. Kama amefumaniwa mara 3 imagine sioni sababu kwanini asitende tena huo uharamu wake. Kitu kingine hapa, hizi mara 3 ni fumanizi, yeye anajuwa mara ngapi ametoka nje ya ndoa, mara 3 alizofumaniwa na mara kadhaa ambazo alimaliza salama bila kufumaniwa, this is serious jamani tuacheni masihara. Ila jamaa naye anastahili tuzo kwa kweli mmhh yataka moyo si mchezo.

By the way LD, aliyekuomba ushauri ni mume au mke? Kuna siku humu JF kuna kaka mmoja alijadiliwa tabia zake mbaya watu wakaomba features zake ili wajikinge naye. Natamani tungetajiwa features za huyo dada japo kdg ili sisi tusiooa tukae mbali kabisa na ndugu zake isijekuwa ni tabia ya ukoo maana ni noma kwa kweli.
 
Back
Top Bottom