Kuna mtu kaniuliza hili swali jamani, anataka msaada wa Mawazo yenu. Maji yamemfika shingon

Mbu hata mimi naanza kujiuliza mengi...LD na jamaa wana nini kati yao?
LD wewe ndio sababu ya mke wa jamaa kucheat kila mara!

...mnh, :behindsofa:...mie sasa simo humu! ha ha ha


..unaona sasa? hapo kuna watu watakushangaa kwanini upatwe na hali hiyo. Mwingine ndio kwanza ataanzisha kipondo kwa mwizi wake, kisha huyoo anamchukua mkewe anarudi nae nyumbani.
Viwango vya ustahmilivu huzidiana jinsi experience, imani na mapenzi yalivyojitosheleza kwa mtu na mtu.


...e bana wee, usiombe yakukute. Yapo sana haya bana. Mnaishi dunia gani nyie? Unakuta mume analia hadharani kamfumania mkewe anamtaka mkewe, arejee nyumbani. Mapenzi ni sehemu ya wazimu ati!

Je, mkaka anaumwa kisukari?:crazy:

...aahahhaaahhaaa, mapya haya sasa, aende kwa babu wa Loliondo ee?
"Cobra" hanyanyuki ila kwa kupigiwa filimbi sio?
 
embu nikuulize msamaha wako unaupima kwenye mizani ipi na huwa tunapanga mambo ya kusamehe au maamuzi huja baada ya jambo kutokea embu tuwe wakweli kwenye hili.

Kusamehe naweza kwa sababu siwezi kuishi na kinyongo kwa maisha yangu yote yaliyosalia.

Ila uhusiano wa kimapenzi na huyo mke au mwanamke aliyenichiti hautakuwepo tena.

Kwa hiyo kwa kusamehe namaanisha sitajenga uadui. Nikikutana naye sehemu tutasalimiana, tutajuliana hali na kadhalika! Lakini uhusiano wa kimapenzi kutakuwa hakuna.

Huyo ndiye mimi. Natambua watu tumetofautiana. Kwa mfano, wapo watu walio kwenye ndoa na wacheza filamu za ngono na wala hiyo haiwasumbui. Wewe unaweza kuolewa na mtu kama huyo na bado akaendelea na kazi yake?

Kwa hiyo cha msingi hapa ni kuheshimu tu tofauti tulizonazo sisi binadamu!!!!
 
Kumbe nawe umeliona hili ehhh?



Ulinishushua niliposema juu ya umri!



Mbona ulijipinga mwenyewe tena?

Hapana ndugu yangu Samawati,

Hata siku moja huwa siandiki kumshushua mtu na nadhani umeukubali msamaha wangu. Kama bado nieleze tu nikuombe samahani tena!

Hoja yangu ya umri ni kwamba labda ndio chanzo cha kuwa na ndoa ya kinadharia na ya kufikirika. Ila bado naamini mtu hawezi kuwa serial cheater eti kwa sababu wametofautiana sana kiumri na mwenzake. Na ndiyo maana bado nashauri kuwa hiyo ndoa haina msingi mzuri na kwa hiyo kama inawezekana waachane hata leo!
 
DC mbona unaukana tena ubabu wako
 

Kweli kabisa...ndo maana kuna vitu huwa watu wanafanya huwezi kuwatofautisha na vichaa wanaookota makopo!
 
DC mbona unaukana tena ubabu wako

TF,

Hivi katika mazingira ya hii sintofahamu ya huyo mlozi wa Loliondo mtu unaweza kujisikia amani kuitwa Babu? Mimi naomba kuahirisha hilo jina kwa muda!!
 
TF,

Hivi katika mazingira ya hii sintofahamu ya huyo mlozi wa Loliondo mtu unaweza kujisikia amani kuitwa Babu? Mimi naomba kuahirisha hilo jina kwa muda!!
:lol::lol::lol: Kweli babu wa loliondo kaharibu imeji za watu
 


Daha kweli kabisa, dada angu, haya yote atayapata.
halafu sasa aamue kusuka au kunyoa!!!
 
TF,

Hivi katika mazingira ya hii sintofahamu ya huyo mlozi wa Loliondo mtu unaweza kujisikia amani kuitwa Babu? Mimi naomba kuahirisha hilo jina kwa muda!!
Jana kuna jamaa alikuwa anaongea na simu aliposema shikamoo babu watu waliokuwa wanamzunguka wakashtuka huku wakimtolea macho l.o.l
 
...I hate being judgemental, lakini kuna mengi yanajieleza humu...
Huwezi kumkuta mwanamke ukajiaminisha ukishamuoa atabadilika tabia.
Huyu braza-kaka kuna kila dalili alitumia jeuri ya faranga zake kumkwapua binti kwa mtu.
Sasa ile methali "mla kuku wa mwenzie,..." miguu ndio inamuelea sasa.

Kusema ukweli bado sijaona nia!!
Labda anataka kunitoa likizo nini??
Sijaona Ishara lakini.

...LD, haya yote aliyokwambia ndio ishara za nia yake kwako.
"Wakey, wakey...!!!"
Utakujashtukia unaitafuta shuka ingali kushakucha.

He's 47yrs old, ana enough experience nini analotaka kufanya.
Hana haja ya kuku-consult mambo haya ila kukupima "alliance" yako kwake.
Welcome to the men's world
 
Daha kweli kabisa, dada angu, haya yote atayapata.
halafu sasa aamue kusuka au kunyoa!!!

Hebu mweleze kuwa kwa umri huo anatakiwa kuwa analea wajukuu. Na kama ataendelea kuishi na huyo Serengeti girl basi asubiri kulea watoto wa wenzake.

Ila kubwa zaidi ni kwamba jamaa anaumwa sana tena sana. Vinginevyo hii ndoa ilitakiwa kuwa historia siku nyingi...Wapo wamama wengi wamemalishatinga menopause wanatafuta watu wakuepeana nao faraja. Hiyo nidyo michuma ya kuwahi na si hawa watoto wa viwanja!!
 

LD hizi info za hao wapendanao a.k.a wadanganyanao zilitakiwa ndo zifungue thread maana watu tumezunguka weeeeee....kumbe tatizo liko wazi kabisa!!!!

Babu inabidi kuwe na darasa aisee....hii ndo hasara ya kukimbilia au sijui niseme kukimbiza ndoa kabla ya kufahamu kama kweli mtu unaekimbia nae mtawezana au la!!!Kuna watakaokuja na hoja ya ''hakuna aliyekamilika'' ila ukweli ni kwamba mtu anatakiwa akamilike kaajili yako...sio kwako ila kwaajili yako!!Hapo ina maana kwamba kasoro zake unaweza na uko tayari kuzibeba!!Sasa mzee wetu hapa amechukua mtoto akampa kazi ya kua mke na matokeo ndo hayo!!
 
LD shosti
Kulikoni tena?
NI YUPI NDUGUYO KATI YA HAO WAWILI?

Dah shosti, hebu tuliache kwanza hilo swali!!!
Niambie shostito kaka huyu anamuacha je huyu kipenzi chake jamani.
 
Akeketwe...! Fullstop.
 
hahaaaaaaaaaaaaaa mbu umenifurahisha


 
Reactions: Mbu



kumbuka kuwa katika hivyo viapo pia,
mlisema kuwa mtakuwa pamoja katika,
shida na raha!!!!!!
 
Dah shosti, hebu tuliache kwanza hilo swali!!!
Niambie shostito kaka huyu anamuacha je huyu kipenzi chake jamani.
Mamushka!
Si ampotezeee tu akuchukue wewe jumla kuliko mnavyoibana?
 
Duh hii mada imenipita, ila kuna watu wana moyo jamani huyo kaka pamoja na kufanyiwa hivi bado atamshukia chumvini mkewe :lol::lol::lol::lol::lol: poor him lol
mie mara moja tu ur out mwanzo ni mgumu ila nitaweza tuuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…