Kuna mtu kawauliza swali wanaosema "Mungu hafananishwi na kitu chochote" wameshindwa kujibu wanamtukana na kumpa vitisho. Mpeni majibu tafadhali

Kuna mtu kawauliza swali wanaosema "Mungu hafananishwi na kitu chochote" wameshindwa kujibu wanamtukana na kumpa vitisho. Mpeni majibu tafadhali

LIKUD

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
18,037
Reaction score
33,681
Ilikuwa kwenye mjadala kuhusu maoni ya Harmonize kwamba katika miaka ishirini aliyo ishi duniani amegundua kwamba huenda Mungu ni mwanamke..

Wenye dini zao wanasema Harmonize apigwe mawe kwa sababu amekufuru na kwamba " Mungu hafananishwi na kitu chochote kile"

Swali la jamaa lilikuwa:

1. Mlimuona wapi huyo Mungu hadi mje mtuambie kuwa hafananishwi na kitu chochote.

2. Kama Mungu hafananishwi na kitu chochote then mna tumia vielelezo gani kuthibitisha kwamba hivyo vitabu vyenu vimetoka kwake kwa sababu tayari mmeshasema hafananishwi na kitu chochote. Je hamuoni kwamba mnaji contradict?

Kama Mungu hafananishwi na kitu chochote basi maana yake hata Qur'aan na Bible haviwezi kuwa vitabu vyake kwa sababu ili tuseme kuwa hivyo ni vitabu vyake lazima ndani yake kuwemo na vitu vilivyo andikwa ambavyo tukivisoma ndio tuseme.ama kwa hakika vitu hivi vimetoka kwa Mungu jambo ambalo haliwezekani kwa sababu tayari mmeshasema hafananishwi na kitu chochote
 
... atheism inakuja kwa kasi sana! Ole ni wao 100 yrs later; hawa hawatamjua MUNGU kabisa! Ni hatari sana.
 
... atheism inakuja kwa kasi sana! Ole ni wao 100 yrs later; hawa hawatamjua MUNGU kabisa! Ni hatari sana.
Alieliza swali sio atheist
 
... atheism inakuja kwa kasi sana! Ole ni wao 100 yrs later; hawa hawatamjua MUNGU kabisa! Ni hatari sana.
Mbona miaka ya nyuma awakumjua na walikuwa wanaishi hata hapa Tanzania jamii kama za wa masai na waadzabe wanamjua Mungu kidogo sana wengine hawajui chochote unaona kinawakuta kibaya gani.

Mungu mpaka uambiwe uwepo wake usipo ambiwa kwaiyo Mungu uwezi kumjua kamwe hii inatia kidogo mashaka.
 
Duh hoja yako imenifikirisha sana mkuu hasa paragraph ya mwisho
 
Back
Top Bottom