Mr George Francis
JF-Expert Member
- Jun 27, 2022
- 278
- 512
Kuna watu wanatoka familia ambazo wazazi wao wanawapa kila kitu wanachokitaka na ndugu zao wanawapa support wanazohitaji katika harakati zao.
Lakini kuna sisi tunaotoka familia ambazo wazazi wametupa kile kidogo kilichopatikana. Tumebeba jukumu la ukombozi wa familia katika umri mdogo tukiwa hatuna kazi yoyote ya maana.
Tunapitia changamoto ngumu na nzito sana ambazo sio tu rafiki zetu bali hata wazazi wetu wenyewe hawajui.
Kwa tulio na watoto ndio kabisa tunajitahidi kuficha maumivu yetu kwao na kwa wazazi tuliozaa nao au wenza tunoishi nao.
Lakini sio kwamba wao sio muhimu kwenye maisha yetu au hawapaswi kujua tunayopitia la hasha! Tunaogopa tu kuwatia unyonge kwani kwao sisi ni watu imara na wanapata mahitaji yao kupitia jasho, damu na aibu tunazopitia katika utafutaji wetu.
Sometimes inatulazimu kuishi maisha ya mbali na nyumbani mbali na macho yao kwani kama wangeona hatari tunazopitia kwaajili yao basi naamini wao wangeumia zaidi yetu.
Sometimes wakituomba picha tunawatumia picha nzuri tu, hata mitandaoni tunapost picha za photoshoot sio kwa lengo la kutaka kuvimba hapana! Bali tunaogopa kuwapa unyonge wale wanaotutegemea.
Yaani kwa ufupi tumebeba matumaini ya watu wengi sana nyuma yetu na hatupendi kupoteza furaha zao.
Mafanikio yetu ndio mafanikio yao na anguko letu ni anguko la familia zetu masikini zenye matumaini makubwa kwetu.
Mwenyezi MUNGU ndio tegemeo letu kwani sometimes wanaotupiga vita hawatoki mbali. Wengine ni hawahawa tunaotafuta nao maisha kwa jasho na maumivu makali.
Watu imani imepotea hadi wanaamini tukikosa sisi wao ndio watapata. Kumbe kumfanya mwenzako akose hakuwezi kukufanya wewe upate kwani riziki mafungu na kila mtu ana lake na atapata kwa wakati wake.
Kwa wewe ambaye katika kupambana kwako teyari umejaliwa kupata chochote kitu "MSHUKURU MUNGU" kumbuka pia wengine uliowaacha nyuma yako.
Kuna watu walikushika mkono kabla hujafika hapo ulipo. Kuna watu walikuombea ili ufanikiwe na wengine MUNGU amepitisha tu riziki kwenye mikono yako kwaajili yao.
Furaha ya kweli ni kuwafanya wengine wawe na furaha.
Tumebeba matumaini ya watu wengi sana nyuma yetu. Eeh Mwenyezi MUNGU naomba utusaidie. 🙏🙏🙏
Content By Mr George Francis