Kuna nafasi nzuri zaidi ya kujenga Taifa linalozingatia haki na Rais Samia

Msambichaka Mkinga

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2015
Posts
1,646
Reaction score
2,911
Ukiyatazama yaliyofanyika wakati wa Samia, ukiacha doa kubwa la kesi ya inayoaminika ni ya kumbambikia Mbowe na makomandoo, kuna nafasi nzuri zaidi ya kuijenga Tanzania ya haki na demokrasia, katika utawala huu wa Samia, pengine kuliko utawala wa mwingine yeyote.

Kuna mengi positive yamefanyika katika utawala huu, japo pia yapo mengi yaliyobakia, katika kilinda na kujenga haki na demokrasia kuliko utawala uliopita:

1) Kufuta kesi za kuwabambikia watu (mashekhe, wahujumu uchumi, madawa ya kulevya, n.k.), japo na yeye akaikubali ile ya ugaidi

2) Kukemea matendo maovu dhidi ya Polisi. Alikemea matukio ya mahabusu kufia kwenye mahabusu za polisi, alikemea tabia ya polisi kuwaonea madereva, na hivi karibuni dhidi ya Polisi wanaoaminika umwua mfanyabiashara, na akaagiza kuunda kamati isiyo ya kipolisi kuchunguza tukio hilo. Na sasa hivi kuna mabadiliko ya kiwango fulani juu ya utendaji kazi wa Polisi. Madereva ni mionhoni mwa mashuhuda wa hili. Ule ubabe unapungua kwa kiasi fulani.

3) Kuziagiza mahakama zitende haki.

4) Kuwaambia wananchi wawe na kauli na walalamike inapoonekana viongozi wanafanya mambo ya hovyo kuhusiana na miradi inayojengwa maeneo yao.

5) Kuyafungulia magazeti yaliyofungiwa kidikteta, na kutaka kupitiwa sheria zinazosimamia vyombo vya habari.

Mambo ambayo ni negative:

1) Kuruhusu Polisi kuendesha kesi inayoaminika ni ya kubambikia dhidi ya Mbowe na makomandoo

2) Kutoweka wazi kalenda ya kupata katiba mpya

3) Kutoshughulika na ubadilishaji wa sheria na mifumo inayochochea ugandamizaji wa haki na demokrasia

Pamoja na yote, ni lazima tukiri, kuna hatua, na kuna mwanga wa kujenga Tanzania mpya kwenye utawala huu kuliko utawala uliopiya.

Katika mapambano, kuna hatua, na kila hatua inahitaji mbinu mpya. Vyama vya upinzani, ili kupata matokeo chanya kwa haraka, ni muhimu kwenye utawala huu ulio tofauti na uliotangulia, kubadili mbinu za utendaji kazi ili kufika panapohitajika:

1) Rais, mara kadhaa ametamka kwa kauli na matendo kutaka haki

2) Vyama vya upinzani wakati wote vimekuwa vikipigania uwepo wa haki

Kwa sababu ya hiyo intersection, pande mbili hizi ni muhimu kujenga mazingira wezeshi ili kujenga mstakabali wa pamoja.

Kosa kubwa ni pale kila upande utakapoamua kuwa na msimamo mkali. Gharama yake itakuwa kubwa kuliko faida. Ningekuwa kwenye nafasi ya kushauri ningesema Rais kupitia ofisi ya DPP wafute kesi isiyo na maana yoyote dhidi ya Mbowe. CHADEMA, wayatambue na kuyakubali mambo positive yaliyofanywa na Rais.

Pande zote mbili zitengeneze mazingira wezeshi na rafiki, ya kukutana na kujadili namna bora ya kuendesha shughuli za kisiasa kwa kufuata sheria na katiba, huku lengo kubwa likiwa kuijenga Tanzania yenye maendeleo, inayozingatia misingi ya utawala bora, haki za kidemokrasia, uhuru wa maoni, haki za kiraia; na pia kubunja na kufuta sheria zote na mifumo inayochochea uharibifu wa demokrasia, haki za watu, uhuru wa maoni, na maendeleo ya wananchi.
 
Lakini gharama za maisha hujaongelea hata kidogo
Upo sahihi. Japo hatuna uhakika gharama hizi zimesababishwa na nini hasa. Je, ni tozo kwenye mafuta? Lakini baadaye walipunguza baadhi ya tozo. Je, ni bei ya mafuta kwenye soko la Dunia? Je, ni ujeuri wa wafanyabiashara? Inaonekana, hata wao Serikalini hawajui kwa uhakika. Kama hujui kisababishi, siyo rahisi kumaliza tatizo.
 
mfumo wa HAKI ulichezewa vibaya mno na awamu ya tano chini ya uongozi wa mwendazake, katiba yetu ikakanyagwa bila aibu as of now bado watu wapo mahabusu wengine wamefungwa kwa kesi za kutengeneza kabla na baada ya uchaguzi mkuu.

Wengi wamefilisiwa, kudhalilishwa, kuteswa na kuumizwa au hata kupotezwa kisa kikubwa ni mambo ya siasa au kuikosoa serikali hiyo - ilifikia pahala kuwa katika siasa za upinzani ikawa kama kukata tiketi ya mateso au hata kifo.

Kutoa ahueni ya haya yote basi Taifa likubali kuuangalia mfumo huu wa HAKI kwa jicho la tatu - na dawa ama mzizi wa kuyamaliza haya yote ni kukubali mchakato wa KATIBA MPYA kuhuishwa.

Pamoja na hatua hizi za sasa, mfumo wa utoaji HAKI bado finyu sana sana.
 
Tuendelee kumwombea Mama afanye vizuri zaidi. Huko kwenye chama chake kuna watu waongozwa na pepo wabaya.
 
Jpm aliharibu kiasi kwamba hata yale anayofanya Samia badi yanaonekana ni kiduchu.

Anyways kila mchuma janga hula na wakwao. Wacha Samia ayabebe maana alikuwemo naye pia.
 
Tuendelee kumwombea Mama afanye vizuri zaidi. Huko kwenye chama chake kuna watu waongozwa na pepo wabaya.
Ni lazima kumpa moyo katika haya machache aliyoyafanya vizuri ili afanye zaidi.

Walioguswa na mabadiliko chanya ni lazima watamponda, nasi tunaotaka afanye zaidi tusipompo moyo kuonesha tunafarijika na yale aliyokwishafanya, anaweza kukata tamaa ya kufanya zaidi maana ataona kuwa hakuna kundi linalomwunga mkono katika mabadiliko chanya aliyokwishayafanya.
 
Sahihi kabisa.

Magu aliharibu nchi kiasi kwamba itamchukua Samia kurithisha watanzania kwa madhira waliyopitia
 
Mkuu jambo moja ambalo ni muhimu katika kuleta haki katika taifa letu ni mageuzi makubwa ya kimfumo Jambo ambalo linafanywa Sasa ni kuweka viraka katika nguo ambayo tayali isha kwisha.

Kila siku tutakuwa tunaimba nyimbo hizi hizi hii ni nchi sio Mali ya mtu binafsi,chama,taasisi nk hivyo lazima tuzingatie Sheria tulizo jiwekea wenyewe hi hali ya nchi kuongozwa kwa fikra za mtu na utashi wake binafsi sio afya kwa maenndeleo ya taifa letu.

kiongozi wa kweli anaye penda taifa hili lipate maenndeleo ya kweli lazima Kwanza afanye mageuzi ya kimfumo Kwanza hapa ni hitaji la "katiba mpya"
 
Hakika, katiba mpya iliyo nzuri, na siyo katiba mpya magumashi, ndiyo suluhisho kuu. Samia bila kusimamia hili, hata angefanya mabadiliko makubwa kiasi gani, atakuwa ameyajenga hewani, hayatakuwa na mizizi wala msingi.

KATIBA.
 
Sijaona lolote la maana
Waswahili siku zote mnapenda maneno matamu matamu.
Anyaway, tupunguzieni mfumuko wa Bei na muwasaidie wazaza wa hawa vijana watano waliopotea chini ya polisi
 
Wacha hii pointi ikae hivyo hivyo. Imetulia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…