Naendelea kujifunza mengi, wazazi tuwe makini sana na malezi, mengi yameongelewa lkn kumuandaa mtoto wa kike na kiume kujitegemea ina faida sana kwa maisha yake ya sasa na baadaye.
Personally mm ni mwanaume, lkn nafika std seven najua kupika aina mbalimbali za vyakula na mboga zake (Particularily traditional foods sio bugger sijui) kwahyo mpaka wakat huu nimeoa na nina watoto huwa wananishangaa napoingia jikoni na kumwambia wife hebu kaa pemben nikusaidie kupika, watoto wangu huwa nawaita japo bado wadogo lkn huwa wanaonesha nyuso za kufurahi sana..kumuona Dady anamsaidia mamy kupika.
Mtoto akifika age ya kujitambua, mwambie pamoja na kuwa na dada wa kazi ( dada yao) haina maana kwamba wao wanatakiwa kurelax, wafanyiwe kila kitu, hapana...mtoto asifike wakati akaona yule dada ameajiriwa pale kufanya kila kitu ndani na yeye akae akunje miguu, mzazi ukiona hyo kuwa mkali...hii itamsaidia mwanao.
Unapofanya hvo iendane sambamba na kumueleza kwann unataka yeye ashiriki kikamilifu kujifunza na kufanya vitu personally bila kufanyiwa na mtu mwingine, tell them just be open, kuna siku hutakuwepo tena duniani, au hata kikazi tu, haitampa maswali ya kuumia mwanao, cos he/she is capable kufanya by her/himself.
Jitahid kuficha ule upendo uliopitiliza wa kusema nampenda sana mwanangu na sitaki apate shida...huyu ndo boy peke yake na nitamjengea nyumba yake sijui hapa pembeni ya nyumba yangu[emoji3][emoji3] aisee anasikia unayomwambia.
Wengi hatujasoma Psychology, lkn saikolojia inasema unaweza kumtengeneza mtoto kuwa kitu chochote unachokitaka, tufaham hivi kwamba miaka 6 ya mwanzo ya ukuaji wa mtoto awe wa kike au wakiume anahitaji support ya karibu sana ya wazazi wote wawili, japo sio kwa wote lkn sailolojia inasisitiza malezi ya wazaz wawil pamoja.
Miaka 6 ya mwanzo imejaa stages almost tatu ambazo mtoto anatakiwa kuzipita kwa lazima akiwa chini ya wazaz wake, na akipita stages hzo successful basi ukuaji wake kiakili, kimwili, kihisia, kimahusiano yake na watu wengine, na kitabia unakua kwa kiwango kinachotakiwa and thay why sometimes unakuta kuna mtu hawezi fanya team work na wengine, au mtu akiachiwa kazi peke yake kuifanya ifanikiwe inakuwa shida.
Stages za awali za ukuaji wa mwanadamu ni za msingi sana....sambamba na parenting style ambayo inafaa...sio kila anachotaka kufanya mtoto wew mzaz unasema just do it....hapana...lazima uwe na limitations...na usiliache hilo kwa mama au baba tu...epuka kuwa Neglectiful parent.....utatengeneza mtoto hatari sana.
Leo hii vijana wengi mjini, ukimwachia kazi siku tatu tu hawezi, kila siku naongea na wife na nina ushahidi...kuna kazi tu zinatokea namwambia wife tafuta watu wa kufanya kazi hizo, mtu anaanza fanya kazi siku 3 tu....anaacha maelekezo aliyoelekezwa, anaanza kuleta maelekezo yake, anaambiwa rekebisha anashindwa...anafukuzwa. huyo ni kijana, maana yake hajaandaliwa vizur kujitegemea mwenyewe...imagine kijana kama huyo atafanya kazi gani mjini, na kwa sasa nisimalizie tu...kuna mambo ya ajabu sana yanaendelea.
Issue ya vyuo nje ya nchi, hasa Asia kuna shida, sijawah soma nje ya nchi lkn nimewah kaa miaka kadhaa nje ya nchi particulary Asia na Some Middle Easterns, lkn nina mtu nayemfaham na nashauriana naye mpaka sasa ili awe sawa, alipata changamoto hzo nje ya nchi akihudhuria masomo undergraduate, hakumaliza, aliishia kula madawa ya kulevya.
Kusima nje ya nchi inatekuja kuathiriwa na tunachokipigia kelele sana hapa, malezi...mfano mm niliwah faulu kwenda O level ya serikali miaka hyo na ilikuwa day school, nilimwambia mzaz wangu kama unataka nifanikiwe naomba nikasome Boarding school, baba akanipeleka Private Boarding...lkn mama mkubwa alikataa na kusema huyu mtoto asipelekwe hyo shule ataenda kuharibikiwa na kuvuta bangi[emoji3][emoji3]
Baba akaniuliza kwamba eti vipi, uende au usiende, nikamwambia mm naenda kusoma siendi kufuata bangi, nilienda kibishi form one kweli nilikuta kuna bangi tu tena sana..lkn nilienda nikijua nilikotoka na nilimaliza form 4 nikafaulu nikaendelea Advance, nikapata kazi kabla sijaenda Chuo na Advance nikafaulu vzur...nikiwa kazin nikajipeleka Udsm nikapiga undergraduate nikiwa kazin, lkn unaona kilichonifanya nifanikiwe, ni ile natambua nilikotoka na sio vile tu nakumbuka mzee alikonilea, sitaacha kutoa ushuhuds huu, siku mzee amekuja nitembelea shuleni kwangu nikiwa sina hata tshs 10, nikajua mzee ameniletea hata hela ya matumizi, mzee aliishia kuniletea zawadi ya BIBLIA sitakaa nisahau maishani mwangu[emoji3][emoji3]. Nilijuliza maswali mengi sana kwamba hv hii Biblia vipi hahaa lkn, nilimuelewa huyo mzee, na Mungu ambariki.
All ina all kama una malezi mazuri na pia umekuzwa namna flan pia kuwa na hofu flan hv ya Mungu, this is another case lkn inasaidia sana.
Kwanini wengi wanaharibikiwa nje ya nchi masomoni;
Wengi wanapagawa na homa ya freedom, wanajikuta wanafanya mambo mengi sana kwa wakati mdogo mpaka wanakosa kutambua ni kipi wanatakiwa kukishika na kuendelea nacho, uhuru uliopitiliza wakat na umri wao bado upo under probation period, inawakuta wameanguka bila kujua, na huku ndugu au wazaz wao wanakuwa mbali nao, na most cases ndugu mnakuja kufaham baada ya kwamba wameshaharibikiwa au wapo kwenye earlier stages za kuharibikiwa.
Wawapo huko hakuna anayemmwambia acha hii jambo, unaenda potea, lknangekuwa home unakuta anapata ushauri kwa wengi kwamba unapotea, though it is sometimes exceptional cases lkn maandalizi ya watoto wetu kusimama wao kwa miguu yao ni muhimu sana..
Duu hii ni independent thread sasa....nitaomba kufanya ya kwangu peke yangu......[emoji3]