Kuna nchi ukimpeleka mtoto kusoma chuo utajuta

... wengi walioenda Russia hawajawahi kurudi binadamu kamili; wanarudigi nusu mtu, nusu debris.
Mbona wa kike hawawi walevi?? Nina Daktari wawili wa kike wamesoma Urusi 7+ years wamerudi hata pombe hawagusi.
 
Mbona wa kike hawawi walevi?? Nina Daktari wawili wa kike wamesoma Urusi 7+ years wamerudi hata pombe hawagusi.
Nami namjua dada amesoma computer engineering urusi hanywi pombe
 
Zuu mtoto wa Kiarabu
 
Exposure kitu muhimu sana kwa watoto wetu. Mpe mwanao asilimia fulani ya uhuru hasa anapoanza kujitambua, hii itamjengea kuyajui mazuri na mabaya. Tabia za kulea watoto kishua sio nzuri kabisa. Mtoto hajui kufanya lolote la maana akiwa peke yake.

Nitawapa mfano.
Nilizaliwa mji karibia sana na Dar es Salaam. Nikasoma shule ya msingi huko. Lakini kuanzia form 1 maisha yangu yakawa Dar. Nikirudi likizo nakuwa Dar. Nimetanguliza hivi ili upate picha kwamba sijakulia vijijini kusema kwamba hakukuwa na social amenities. Mpaka nafika chuo, hustles zote nazijua....kupika, kufua, kuosha vyombo, kutwanga, kuchota maji mara nyingi nilitumia mkokoteni ulikuwepo home nafata maji kama mita 700 hivi toka home....maji yakiisha ndani basi ndo kazi yangu. Nimecheza chandimu pekupeku sana tu. In short maisha ya kiugumu nayajua.
Mimi nilikua exposed na uhuni kitambo sana, sema nilikua sijapata starting point.

Mimi nilikua sijawahi kunywa pombe, nilianza kunywa pombe nilipokuwa mwaka wa kwanza chuoni. Kisa nini? Si kingine ni marafiki. Ajabu ni kwamba nimesoma boarding za serikali form 1-6....huko kote sikuwa na marafiki wa hayo mambo. Basi hapo nikajua Gins, vodka, beer, brandy, whisky, wines na kila aina ya unywaji wa kulevya.

Nilikua sijawahi kuingia club, mara ya kwanza kuingia club nilikuwa nikiwa chuo kikuu.

Nilikuwa sijawahi kupiga one night stand....hii nimefanya nikiwa chuo kikuu.

Ni bangi tu ndio sijawahi kuvuta. Na ni kwa sababu kampani yangu yote hakukuwa na mtu hata 1 anakula bangi.

Lakini kwa sababu nilikua najitambua na najua nimetokea familia ya aina gani.....hayo yote hayakunifanya nitoke nje ya reli. Niligraduate na 3.7 GPA ni mtu 1 tu darasani kwetu aliyenizidi, sikuwahi hata kupata supplementary.

Leo hii ukiwaambia wanafamilia home kwamba nakunywa pombe wanakukatalia katu katu. Lakini washkaji, ma x zangu, wanajua napiga ulabu tena mzito. Hata mama mtoto wangu (wife to be bado kidogo sana) hajui kama napiga vyombo ingawa hachukii jambo hilo. Hatukai sote muda mwingi so hajajua hilo.

Mtoto wa kishua umpeleke USA na hapa bongo ulimlea kwa kumlimit, akifika huko akutane na Jorge Martin Vasquez, Alex McLeish, Vladimir Kubertiv, ambao wamelelewa kiulaya ulaya since childhood unatarajia nini?

Kuna mwana kasoma Cuba na USA anatuambia kule hadi Waarabu wanakula kitimoto. Ni ule uhuni unafanya mbali na home.
 
Hii sikatai, kuna mwaka fulani mimi na bro tulikua tunafanya kazi sehem jirani tukapanga nyumba 1 tukawa tunaishi kisela. Kuna jamaa 1 alipata kazi mkoa tuliopo akaja kuanza kazi basi tukampokea na kukaa naye geto....jamaa alikua hajui kupika chochote. Kuna Saturday 1 nimerudi job mchana nimekuta jamaa kaforce kupika ugali, kumbe ni uji mzito una mabonge bonge kibao nilishindwa kula. Nikapika ugali chap akashangaa mbona nimepika fasta....nikamwambia ni gesi hiyo.

Kuna times mdogo wake alikuja wa kiume yule naye alikua hivyo hivyo. Kumbe kwao kuna housegirls 2.....yaani dogo hajui chochote ni mzembe balaa halafu eti anasoma diploma.
 
nchi pekee unaweza peleka mtoto asia ni japan na china, na huko wanaenda ili kufamilialize mazingira ya kibiashara tu. nje na biashara zako, kuna ubaguzi mwingi na ujinga mwingi. hata hivyo, ujinga huo hautafikia USA, ambako mtoto anaweza kurudi shoga. canada ni nchi nzuri sana kusoma, pamoja na UK.
 
Hqta ulichoelezea hakieleweki mambo ya ajabu yepi?? Mbpna hata hapa watoto wanaacha chuo wazazi mikoani wanalalamika watoto zao wakija dar hawasomi,huyo mtoto wako anayeacha chuo marekani elewa hakua na muamko wa kusoma au hana akili wala muamko unamfosi tu kuna watoto wanajitafutia scholarship au wanajisomesha wenyewe nchi hizohizo na wanagraduate bila kushikiwa bango na wazazi
 
Una uhakika? Na mabinti wa kike mtu na nduguye, baba yao nafahamiana naye, wamesoma US hadi degree ya pili wamerudi nyumbani.Usifanye generalization tafadhali.
 
[emoji38][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Wanaopeleka mitoto yao Nje wengi ni mabosi wanadhulumu watu wao wa chini pesa ni mafisadi wakubwa ndio maana mitoto yao ikifika huko mingi Ni laana tupu!! Wengi wanaangukia pua hawasemi tuuu,mitoto mingine ya kiume Inaolewa hukohuko.
 
Malaysia ndio useseme kabisa. Kila Binti aliyepelekwa kule aligeuka muuzaji wa huduma ya maili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…