Kabla ya kwenda WCB ungeanza na Diamond kwanza kisha unganisha dots!naomba kujua pale wcb
kazi ya
sallam
babu talent
mkubwa fella
rommy jones
Tale ndo meneja wa awali kabisa wa Diamond... wa awali kwa maana ya miongoni mwa hao uliowataja!!!
Baada ya Diamond kuzidi kuwa mkubwa, ikamlazimu Tale kusaidiana na Saidi Fella kwa sababu Fella alikuwa na uzoefu zaidi kuliko Tale!!
Ukubwa wa Diamond ulipokuwa mkubwa maradufu, akaingia Sallam na mwanzoni kwa ajili ya kusimamia international level kwa sababu tayari Sallam alishakuwa na access na wasanii wa nje ya Afrika Mashariki kulinganisha na Fella na Tale!
In short, Tale na Fella wali-base sana kwenye local market kwa sababu fitina za Bongo Flavor wanazijua inside out!!!
Undugu wa Rommy Jones na Diamond ndio uliomwingiza kundini! Pamoja na kwamba ndie DJ wa Diamond lakini wote wametoka mbali pamoja; si tu kwa undugu wao bali hata kwenye sanaa hususani wakati Rommy yupo Clouds!!!
Hamisha hayo maelezo kisha yapeleke upande wa WCB ingawaje kuna tofauti za hapa na pale kati ya WCB na Diamond.