Doctor Ngariba
JF-Expert Member
- Jan 28, 2020
- 588
- 951
Habari za asubuhi waungwana na wapendwa wa Jamii Forums.
Bila kupoteza muda, mimi ni mdau na mtumiaji wa barabara ya Mwalimu Nyerere takribani miaka saba sasa.
Kuna jambo ambalo kwa siku za hivi karibuni linanikera na naamini wapo pia wengine ambao linawakera nalo si jingine bali ni foleni nyakati za asubuhi uelekeo wa mjini kuanzia maeneo ya Mchicha hadi unapoanza kupanda fly over ya Mfugale. Ikumbukwe ishu siyo foleni (maana ni kawaida kwa maisha ya mjini) bali sababu ya hii foeni ndiyo tatizo.
Nilikuwa najiuliza kwani shida nini kwa bahati leo nimegundua kwamba tatizo kuna baadhi ya madereva wanaoelekea Buguruni au Mbagala wanalazimisha kupita upande wa kushoto uelekeo wa mjini hadi pale inapoanzia Mfugale Fly Over.
Niwaombe jeshi la Polisi wa usalama barabarani mujaribu kuondoa huu uzembe maana ni kero mno na pia kwa nyie madereva hebu punguzeni hizi tamaa za kuwahi kwa kuwa mnasababisha adha kwa watumiaji wengine wa barabara. Naamini jukwaa hili haliwezi kukosa askari wa usalama barabarani kwa hiyo lichunguzeni na kama kuna ukweli tafuteni mwarobaini wake.
Asubuhi njema.