Kuna nini huko, mbona gunia la viazi Dar es Salaam ni laki 1?

je parle

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2018
Posts
2,022
Reaction score
3,919
Tanzania tunashukuru Mungu kwa kuingia uchumi wa kati mpaka sasa gunia la viazi wanauza kuanzia 98.000 hadi 110.000

Tatizo ni uzalishaji mdogo kila mtu kawa machinga au tatizo ni madalali kujipangia bei zao wenyewe?
 
Hiyo mbona ni shilingi 98 na shilingi 110
Au ulimaanisha 98,000 na 110,000 nasi 98.000 na 110.000
 
Nukta kwenye namba(tarakimu) inakuwa ni desimali endapo kuna tarakimu zisizozidi mbili baada yake(upande wa kulia wa nukta), na kama kuna kuwa na tarakimu tatu basi hiyo nukta inachukuliwa kama mkato na hivyo basi hiyo 98.000 ni elfu tisini na nane na hiyo 110.000 ni laki moja na kumi elfu.
 
Wewe! Acha upotoshaji hapa si French speaking country
 
"kama uwezi amia Burundi"
hayo majibu[emoji121]inawezekana kabisa ukapewa na waziri mwenye dhamana anaeongoza serikali ya kizombi kwenye nchi ya mazombi.
 
Nukta kwenye namba(tarakimu) inakuwa ni desimali endapo kuna tarakimu zisizozidi mbili baada yake(upande wa kulia wa nukta), na kama kuna kuwa na tarakimu tatu basi hiyo nukta inachukuliwa kama mkato na hivyo basi hiyo 98.000 ni elfu tisini na nane na hiyo 110.000 ni laki moja na kumi elfu.
sijabadili ukweli kuwa sisi ni nchi inayozungumza kiingereza.
 
Tanzania tunashukuru Mungu kwa kuingia uchumi wa kati mpaka sasa gunia la viazi wanauza kuanzia 98.000 hadi 110.000

Tatizo ni uzalishaji mdogo kila mtu kawa machinga au tatizo ni madalali kujipangia bei zao wenyewe?
Viazi gani...?
Viazi vitamu ama viazi ulaya(chipsi)... Sasa hvi mambo yamebadilika sana kilimo ndo kinaenda kuwa na hela Vijana wengi wameshika boda boda na bajaji...wako load hawataki tena kulima wanataka kununua...
 
Ukame na Kiangazi cha mda mrefu uliathiri sana uzalishaji wa mazao. Hata kitungu kwa sasa hakishikiki. Mfano mkoa wa Iringa bei ya Gunia inasoma 250000.

Sent from my SM-G955U using JamiiForums mobile app
 
Watanzania bwana unajua kulalamika tu ili uzalishe viazi unahitaji Mbolea , madawa aina mbalimbali sasa before mfuko wa mbolea 50kgs sh, 60,000 to 70,000 but nowadays 50kgs imefika mpaka 110,000 mbolea ileile kuhusu dawa kuna dawa kama za ukungu unatakiwa kunyunyiza kila baada ya siku 10 to 14 depending na ubora hiyo ni mbali na booster sumu za wadudu palizi tena sio moja sasa hivi vyote vimepanda almost two times what do you expect?

NB: Mwache mama paige kazi sote kwa pamoja tuseme kaaazi........................?
 
Kitaalam inaitwa IMFLATION. Pesa zimeumuka kama puto kumbe ndani kumejaa hewa.
 
Back
Top Bottom