kuna nini kichwani mwa mke wangu

kuna nini kichwani mwa mke wangu

VIKWAZO

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2011
Posts
1,900
Reaction score
581
jamani leo nimeona nijisalimishe hapa kwenu jamii labda nitapata maarifa.
mke wangu ana msifia sana mdogo wangu wa kiume, yaani kuna wakati hata hakuna umuhimu wa hizo sifa lakini yeye anamwaga tu sifa kwa bwana mdogo!!!!!!
nimefanya utafiti sijagundua kitu chochote, mimi nampenda sana mdogo wangu nashindwa kumuondoa hapa nyumbani kwa kutumia hisia tu kwamba yawezekana kuna kitu kati yake na mama watoto au mama watoto ana kitu kichwani?

mahusiano yetu yako sawa tu, sijagundua kasoro, lakini sifa na maongezi muda wote kuhusu bwana mdogo sasa yanaanza kunipa ishara mbaya kichwani mwangu

naombeni maarifa sitaka kuchemka nawajali na kuwapenda wote, mmoja kama mke na mwengine kama ndugu
 
Naamini wewe ni mtu mzima huwezi tu ukaibuka na kulalama
kitu ambacho hakipo... bahati mbaya hujaeleza sifa hizo ni zipi
maana yaweza kua sifa za kumsifia kua ana msaada mkubwa hapo
nyumbani i.e kusaidia shughuli za hapa na pale au sifa za maumbile
i.e. ooh mdogo wako ana mvuto, dah sijui kifua kimefanyeje n.k

Kikubwa na kizuri ni kua umetambua hizo sifa na hivyo ni dhahiri
hawajafanya mchezo wowote mchafu (naona ndo hofu yako)
maana angekua amefanya au anafikiria asingedhubutu kumtaja taja
mbele yako...

Mimi nakushauri mwambie kua mbona sifa zimezidi??? Walau apate picha
kua hupendi na pia kua wawafuatilia...

Pole saana kwa tatizo lako. Kila la kheri.....
 
VIKWAZO:
Because you have not found anything suspicious, the easiest thing for you to do I think is to just be open and let your wife know that you do feel uncomfortable na hizo sifa kem kem anazomwagia dogo! She just may not be aware how unconfortable you are, so start by letting her know, ili aache au apunguze.
 
sifa ni nyingi kwa kweli
aliwai kusema anaumbo zuri hatapa usumbufu wa wanawake
ana tabia nzuri mkewe hatapata raha
ana juhudi ya masomo na ana akili darasani
ana upendo
na hii ni kama biashara ya kila siku mimi kusikiliza masifa ya bwana mdogo
mpaka inakera
 
VIKWAZO:
Because you have not found anything suspicious, the easiest thing for you to do I think is to just be open and let your wife know that you do feel uncomfortable na hizo sifa kem kem anazomwagia dogo! She just may not be aware how unconfortable you are, so start by letting her know, ili aache au apunguze.

yawezekana kutoka na ubusy na shughuli zangu wakawa na uwezo wa kunifunika maana ratiba yangu in kama kanuni za wokovu
hiko fix. sana hovyo bado nina mashaka kuna kitu
 
yawezekana kutoka na ubusy na shughuli zangu wakawa na uwezo wa kunifunika maana ratiba yangu in kama kanuni za wokovu
hiko fix. sana hovyo bado nina mashaka kuna kitu

Lakini hata hivyo ni bora umwambie, ukiona hata baada ya kumwambia anashindwa kujisitiri na kuvimilia, then at least utajua ana lake moyoni. Ila pole, lakini pia si vizuri, kuwazia mabaya peke yake. Inawezekana labda anasema hivyo ili na wewe uhamasike na kufuata vitu positive she sees from dogo. Kwa mfano, kama wewe ni mnene na mwenye kitambi, basi upunguze, kama wewe ni mkali, basi uwe mwenye upole and upendo kama dogo etc
 
Katika makosa ambayo unatakiwa kuyaepuka ni kufanya maamuzi kwa kutepemea hisia,utakuja kujilaumu sana,kagua tabia ya mke wako kama alikuwa na historia ya kutokuwa mwaminifu,ila fuatilia piam na uchunguze kinachosababisha anamsifia kisha utoe maamuzi!
 
sina hakika sana kama hajawai huko nyuma lakini kwa ufahamu wangu hapana ,
kutoka na msukumo wa mawazo kama hizo hoja mbili hapo juu ndio maana nimekwama, nikweli sitaki kutumia hisia kufanya mahamuzi ya aina yoyote.
kumwambia nashindwa sitakii kufanya kitu ni kakijutia,
nimekuwa nafikilia kufanya hivyo lakini nakwama kwa kugopa kama nitakuta nilikuwa na hisia mbaya tu.
kuna kijana nilita kujaribu kumtumia kama mpelelezi lakini nasiki ni rafiki sana na mdogo wangu.
kwa sasa mimi nafikiri kumtoa dogo hapa home bila kusema kiti ila kwa kutengeneza story
sijui kama itasaidia
 
Usimtoe mdogo wako kwa kufanya hivyo tayari unakuwa umemuadhibu kwa kufuata hisia zako,kama umefuatilia na hujagundua tatizo fuatilia tema au achana na mawazo hayo!
 
jaribu kuvunja ratiba! uje home muda usiotarajiwa, uone hali ikoje. Ikiwezekana, njoo bila hata usafiri wako wa kawaida!
 
Vikwazo,mimi sijui wewe kabila gani,lakini kwetu sisi wahaya kuna kitu tunaita 'okushanzila' meaning kutania.Kwetu ni ruksa kabisa dogo kumtania mke wa kakake ila ni marufuku kaka kumtania mke wa mdogo wake maana yeye anachukuliwa kama baba.Wewe tuliza ball,endelea kumtunza mdogo wako,achana na insecurity , na kisha shukuru kuwa mkeo na mdogo wako mpendwa wanaishi in harmony maana ziko thread kibao humu MMU ambazo zinahusu nyumba kukosa amani kisa shem na wanandugu ni paka na panya na mme anashindwa aegemee wapi.
 
jamii leo nimeona nijisalimishe haba kwenu labda nitapata maarifa.
mke wangu ana msifia sana mdogo wangu wa kiume, yaani kuna wakati hata hakuna humuhi wa hizo sifa lakini yeye anamwaga tu sifa kwa bwana mdogo!!!!!!
nimefanya utafiti sijagundua kitu chochote mimi nampenda sana mdogo wangu nashindwa kumuondoa hapa nyumbani kwa kutumia hisia tu kwamba yawezekana kuna kitu kati yake na mama watoto au mama watoto anakitu kichwani?

mahusiano yetu yako sawa tu sijagundua kasoro, lakini sifa na maongezi muda wote kuhusu bwana mdogo sasa yanaanza kunipa ishara mbaya kichwani mwangu

naombeni maarifa sitaka kuchemka nawajari na kuwapenda wote, mmoja kama mke na mwengine kama ndugu

kwa pointi yako ya mwisho umesema unawaheshimu wote, pia pamoja na misifa hiyo yote ukafanya uchunguzi lakini hujagundua kibaya chochote, kubwa ambalo naliona kutoka kwako ni wivu wa mapenzi, nakushauri umwambie mke wako kiustaarabu kuwa hiyo mijisifa imezidi na wakati mwingine we hupendezwi nayo. Naamini kama mkeo anakupenda atajirekebisha. Sidhani kama kuna kitu kichwani mwake ila tu we una wivu. Pole kwa mkasa.
 
Usifanye maamuz yoyote ya haraka had uwe na uhakika braza,take time chunguza yaweza kuw hamna kinachoendlea
 
Bro, kwani mdogo wako anafanya nini hapo nyumbani kwako? ana umri gani? yeye anasema nini kuhusu shemeji yake? Na yeye anamwaga sifa? ukimwangalia kwa kumkazia macho usoni yukoje? Just remember the guilt are always afraid!
 
Nahisi ni hisia zako tu, angekuwa na lake jambo asingethubutu hata kumuongelea mbele yako, mshukuru tu Mungu mkeo anampenda ndugu yako na anaishi nae kwa upendo.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Mkuu, kuna member kauliza umri wa mdogo wako! Pamoja na kuwa umekuwa suspicious, jaribu kuficha hisia zako ili usichafue hali ya hewa nyumbani. Kwa mtu mwizi huwa anakuwa na kawaida ya kufuta nyayo ya anapopita. Kama wife na mdogo wako wana uhusiano, basi wangekuwa mbali kiasi, japo dalili nyingine zingejionesha.
Thank God wife anawapenda ndugu zako, kwani wengine huwachukia sana ndugu wa mume. Usivunje trust ya mkeo, japo inabidi uchunguze kwa busara zaidi na bila wao kujua. Na mwambie mkeo, badala ya kumsifu sana mdogo wako, basi akuambie madhaifu yako ili ujirekebishe na akusifie wewe.
 
jamii leo nimeona nijisalimishe haba kwenu labda nitapata maarifa.
mke wangu ana msifia sana mdogo wangu wa kiume, yaani kuna wakati hata hakuna humuhi wa hizo sifa lakini yeye anamwaga tu sifa kwa bwana mdogo!!!!!!
nimefanya utafiti sijagundua kitu chochote mimi nampenda sana mdogo wangu nashindwa kumuondoa hapa nyumbani kwa kutumia hisia tu kwamba yawezekana kuna kitu kati yake na mama watoto au mama watoto anakitu kichwani?

mahusiano yetu yako sawa tu sijagundua kasoro, lakini sifa na maongezi muda wote kuhusu bwana mdogo sasa yanaanza kunipa ishara mbaya kichwani mwangu

naombeni maarifa sitaka kuchemka nawajari na kuwapenda wote, mmoja kama mke na mwengine kama ndugu

Pole sana kaka kwa yanayokukuta,
kiukweli kauli kama hizo zinaleta mashaka kidogo,
na hatimae zinakufanya ujisikie inferior kiasi fulani,

Lakini labda cha msingi zaidi, si vema kumhukumu,
pasipo kuwa na uhakika na hizo investigations zako!
inaweza kuwa kuna kitu huyu mke wako anakimaanisha pindi anapokueleza hilo,
sasa anataka upay aatention kwake na ubadilike, lakini wewe bado hujaonyesha dalili
za mabadiliko!
Lakini inawezekana pia kukawa na kitu kinachoendelea hapo,
kwani hawa dada zetu nao wakishapenda na kunogewa na kitu fulani,
kwakweli huwa wanajisahau na kujikuta hata staha hakuna tena.

Jaribu kufuatilia kwa makini hizo kauli zake, na usifanye maamuzi ya papara!
 
kuna kitu anakiona kwa mdogo wako na kwako hakioni.ndio maana anajaribu kutoa sifa hizo ili na wewe ufuate,mfano anasema ni mpole ina maana wewe sio mpole,anaposema mke wake hatapata shida ina maana yeye anapata shida,jaribu kila anapotoa sifa mwulize je kwangu hupati?usikie maelezo yake.Mfano akisema mdogo wako mpole sana,mwambie ndivyo kwetu tulivyo kwani hunioni hata mimi?hapo utapata jibu maana atakueleza.Usikurupuke,utajutia maamuzi yasiyo sahihi ya hisia kwaajili ya wivu wako.
 
Back
Top Bottom