Kuna nini kimejificha nyuma ya hawa warembo wanaouza karanga mtaani?

Kuna nini kimejificha nyuma ya hawa warembo wanaouza karanga mtaani?

AMANI YA BWANA IWE NANYI, MUNGU AWAPAYE WATU NEEMA NA AWAPE NEEMA.

Kuna jambo nimeliona huku mtaani siku za hivi karibuni sijawahi kulielewa kwa undani wake kuna nini kimejificha huko.

Hivi karibuni kumeibuka kundi kubwa sana la akina dada warembo ambao wanazunguka mtaani hasa majira ya Jioni wanatembeza karanga.

Kwenye mtaa mmoja unaweza kuwakuta wapo hata watano. Mtaa ambao nimewaona sana ni salasala, Mbezi Beach, goba na mbezi ya kimara(ndio nimeishi huko).

Uuzaji wao inaweza isiwe shida sana ila shida kubwa zaidi ni mavazi wanayovaa, wanavaa kama wale wahudumu wa Bara.

Swali langu lipo hapa je shida nini wameongezeka sana? ni ugumu wa maisha, au wamjitambua na kuamua kujiajiri, au kuna uhitaji mkubwa sana wa hizo karanga mtaani, au ni fursa mpya? au kuna nini cha zaidi

Mwenye majibu zaidi atujuze
Uzuri wa maswali yako yote yanashirikiana. Swali la 1 jibu lake lipo swali la 2 na la 3 alkadhalika.
Nadhani majibu ya wengine ni nyongeza tu.
 
Kuna mambo matatu kama si manne ndani yako:
  1. Kuuza karanga ni kwa wanaume Tu.
  2. Wauza karanga wawe wakibosho na Waha na wawe wachafu.
  3. Wauza karanga wawe wachafu, nuka kikwapa, wanaoingia choo cha jiji na kapu la karanga.
  4. Wawe wanajifuta jasho na mkono wanaotumia kukupimia karanga.
JIFUNZE HIVI.
  1. Wanawake wamekataa kuwa magolikipa, sasa nasi tunataka kulea familia.
  2. Single mother kama akina Hamisa Mabeto, Zari, Giggy Money, Christina Shushu, Blandina Chengula na wengine wakilala nani atalisha familia zao?
umeuchambua kama Jaji. hayo mambo manne hayapo ndani yangu mkuu
 
Back
Top Bottom