Kwani graduation ni mojawapo ya vigezo vya kutunukiwa cheti?
Mimi sikuwahi shiriki graduation yoyote ile na nilihitimu na kutunukiwa cheti. Kwenye prospectus ya chuo chochote hakuna sehemu imeandikwa kuwa mahafali ni sehemu ya kukamilisha vigezo vya kutunukiwa cheti, na wala hayana alama, na hayana kufaulu au kufeli, na si lazima.
Chuo kinaweza toa cheti kabla, wakati wa, au baada ya graduation. Na mnaweza kosa graduation kabisa na vyeti mkatunukiwa. Mwaka huu Arusha Technical hawana graduation na vyeti wanapata waliokidhi vigezo.