Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sisi hatuna jambo, tukishindwa jambo tuna singizia mabeberu.Nchi zetu changa zinapelekeshwa kila siku na ubeberu. Ukiwepo mpango wowote wenye maslahi kiuchumi kwa umma ila unakinzana na maslahi ya ubeberu au vikaragosi vyao unakwama.
Ni vigumu mtu kuamini sababu zinazotolewa kila siku kwanini mpango wa Serikali kuwapatia wananchi wake vitambulisho vyenye ubora mkubwa kukwama. NIDA kuna jambo.
Inaelekea kila Mkurugenzi mpya akiwekwa anakutana na jambo. Hebu niambieni mbona vitambulisho vya wapiga kura kwa ubora huo huo vinakamilika lakini vitambulisho vya Taifa vinasuasua. Kuna watu hawataki kila mtanzania atambulike kwa maslahi yao mabaya kwa taifa.
Ni muda sasa wa kutimua panya wanaotafuna mradi wa vitambulisho vya taifa usiende unavyotakiwa. Mabilioni yanapotea bila faida kamili iliyokusudiwa kwa mradi wa vitambulisho vya Taifa.