Kuna nini Nyuma ya FIFA (Blatter) na Marekani?

Kuna nini Nyuma ya FIFA (Blatter) na Marekani?

Barbarosa

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2015
Posts
22,584
Reaction score
27,817
Hili jambo linanitatiza kidogo, Nchi ya Marekani haijulikani kama nchi maarufu kwa mchezo wa huo kipenzi cha wengi hapa Duniani soka ambao unaratibiwa na FIFA yenye makao yake Makuu huko nchini Uswisi chini ya Kiongozi wake wa siku nyingi
Bw.Sepp Blatter!


Sasa ni nini kimeisukuma Marekani kulivalia njuga hili swala la FIFA na viongozi wake? Na Je, ni kwamba imetokea tu sasa hivi au ilipangwa iwe hivyo ukizingatia ya kwamba FIFA wako mbioni kufanya Uchaguzi na Bw.Sepp Blatter mpaka sasa hivi ndio kipenzi cha wengi, sasa Marekani anashinikiza akamatwe, sasa kwa nini hili lihusu Marekani? FIFA haiko ndani ya ardhi ya Marekani, Sepp Blatter ni Raia wa Uswisi na siyo Marekani, na isitoshe Soka siyo mchezo maarufu Marekani kuweza kuifanya nchi hiyo ijiingize kwenye hili!

Je kuna uhusiano labda na FIFA kuipa Urusi nafasi ya kuwa mwenyeji wa Kombe la Dunia mwaka 2018? Ikizingatiwa ya kwamba kama Urusi ikipata hiyo nafasi basi itatumia kuonyesha Dunia mambo mazuri ya Urusi na hatimaye labda kujipatia Umaarufu Duniani kinyume na matakwa ya mayahudi ya Marekani?
 
Tatizo mkuuu mimi nachoona hapa marekani wantaka kujifanya wababe wakilaa kituu
Nilikua naangalia web ya cnn sport makampuni makubwa ya VISA na Hyundai yamejitoaa kama wathamini wakubwa wa FIFA…
 
Tatizo kubwa hapo ni urusi tuu sA marekani watumia mabavu yao ya kisiasa mpaka kwenye soka,
 
Marekan inavyopenda kuingilia mambo! mda si mrefu watapandikiza chuki! mim nahis hata yake Mapambano ya Mywheather na Pac kama pac angemshinda may huko Ufilipino kingenuka
 
Marekani ndio Baba wa Dunia,akiwa kama Baba lazima ahakikishe kila kitu kinakwenda sawa kwenye familia/Dunia yake. Fifa ni kichaka cha Rushwa na Ufisadi kama ilivyo CAF na TFF. Kwa hiyo ni Marekani pekee anaethubutu kufanya yale Nchi nyingine zinaogopa kufanya. Hongera sana Marekani.
 
Zoezi la kwenda Urusi kwa ajili ya WC ni gumu sana kwa USA na hakika lazima wafanye jambo ngoja tukae tuone hii vita nani atashinda.
 
Kilichopo hapo ni Ugomvi wa US na Rusia,Itakumbukwa kuwa uvamizi wa Urusi kule Ukraine haukumpendeza Mmarekani na washirika wake,mpaka US na wapambe wake wakamuwekea Urusi vikwazo vya kiuchumi.
Sasa US kwa siasa zake amekamata viongozi wakuu wa FIFA wenye ushawishi ndani ya shirikisho kwa tuhuma za "rushwa" maana jamaa waliikataa ushawishi wa US and Co. wa kuiondolea Urusi nafasi ya kuandaa kombe la Dunia 2018 ili nafasi hiyo apewe Uingereza kwa kisingizio kuwa Urusi inakiuka haki za binadamu na hivyo kuwa kinyume pia na falsafa na dhamira ya FIFA duniani
Ni kweli FIFA kuna rushwa,lakini hii sio dhamira ya Marekani
 
Zoezi la kwenda Urusi kwa ajili ya WC ni gumu sana kwa USA na hakika lazima wafanye jambo ngoja tukae tuone hii vita nani atashinda.

Wanataka FIFA aondoe nafasi ya kombe hilo Urusi 2018,maana kupelekwa kwa kombe hilo huko,kutamuongezea Putin umaarufu na kuwasahaurisha watu juu ya machungu ya vikwazo alivyowekewa Urus
Ndio maana leo Vladimir Putin kaibuka na kumpongeza Sepp Blatter

N View attachment 255407
 
Kwa soka la wanawake marekani ndo timu bora duniani. Sijui unaongelea nini hapo
 
USA walisema, kwa sababu FIFA inatumia baadhi ya brand za USA na system zake hivyo lazima waingilie kati.
Na FIFA kwa kweli kama ni matope tu basi imepakwa sana. Blatter akubali kushindwa WC iondoke Russia, Tupewe Tanzania
 
USA walisema, kwa sababu FIFA inatumia baadhi ya brand za USA na system zake hivyo lazima waingilie kati.
Na FIFA kwa kweli kama ni matope tu basi imepakwa sana. Blatter akubali kushindwa WC iondoke Russia, Tupewe Tanzania

Huu ni wivu tu wa US na washirika wake.Huu ni ujanja wa Urusi ya Putin,hakuna dhamira ya kukomesha rushwa,hapa ni vita dhidi ya Urusi
 
NATO ndo polisi wa dunia. Mwenye kubisha aje
 
Nimeona Goal.com
Putin kaongea kuhusu hiyo kitu.
UEFA nao wana mpango wa kuboycot FIFA......
Blatter anasema FIFA haitaingilia uchunguzi wa USA na Swiss, anasema hawezi jiuzulu kwani ni ngumu kumonitor kila mtu.....
Naona Revote kuhusu Host nations inafanyika
 
First things first, Rushwa. Walio-expose huo uozo na kwa malengo yapi ni baada ya. Besides, Marekani ni mwanachama wa FIFA as well.
 
Hzo dili zilifanyika Marekanı na ushahidi upo.Ndo sababu ya Marekani kuingilia.Fifa na Mashirikisho ya soka kote duni ni magenge ya kihuni na wezi.Walimpiga zengwe Binamam wa Qatar,sasa yamewakuta.
 
USA walisema, kwa sababu FIFA inatumia baadhi ya brand za USA na system zake hivyo lazima waingilie kati.
Na FIFA kwa kweli kama ni matope tu basi imepakwa sana. Blatter akubali kushindwa WC iondoke Russia, Tupewe Tanzania

Kwanin iondolewe russia na sio qatar?
 
Back
Top Bottom