Kuna office nimeitembelea leo,office nzima mpaka mkurugenzi hawajui kuongea Kiingereza

Sio kweli.haiwezekani uwe mkurugenzi halafu lugha nyepesi kama kiingereza ikupige chenga.
Ukurugenzi unahusiana nini na Kiingereza?

Neno "Mkurugenzi" lina maana ya mtu anayesimamia au kuongoza taasisi, shirika, kampuni, au idara fulani. Kwa kawaida, mkurugenzi anakuwa na majukumu ya kufanya maamuzi makubwa, kusimamia rasilimali, na kuhakikisha malengo ya taasisi yanafikiwa.

Hakuna sehemu inayotakikana ili uwe mkurugenzi ujue kiingereza.
 
Piga chini wafanya kazi wote wa hapo wapelekwe Veta mpaka na huyo mkurugenzi wao wakasome ufundi
Halafu chukua vijana wasomi waliojaa mitaani wanabeti wape hizo ajira
 
Sio kesi man lugha za watu hizi.Mbona wenyewe hawajui kiswahili?

Ukweli ni kwamba hakuna mtanzania aliyepita mfumo wa formal education atashindwa kujua English ya kujieleza hii ya is and was.Tatizo mnapenda waongee kama watoto wa malkia na wakikosea mnaleta mada kama zote humu.
 
Sawa hata hivyo hao wazungu wanapenda wajifunze kiswahili
 
Sio kweli.haiwezekani uwe mkurugenzi halafu lugha nyepesi kama kiingereza ikupige chenga.
Mkuu mbona Wachina hawajui Kiingereza tena utakuta Mchina ni Engineers kabisa, Au Mtaalamu wa Maswala ya Mafuta na gas lakini Kiingereza hajui, Utakuta anataka kwenda mjini anamwambia Dereva ampeleke mjini sasa lugha ya Kiingereza anayosema inafurahisha, utasikia ana Mwambia dereva Me you to Town( ana maanisha apelekwe mjini).
 
Mkuu mifumo yetu ya kiutendaji ni ya lugha ya Kiingereza ina Maana kama hajui lugha atapata shida kusoma Mikataba au Barua na kujibu Email kutoka nje.
 
Lugha yetu ya taifa ni kiswahili. Kiingereza ni lugha ya biashara ya kimataifa.
Sio lazima kila mtu ajue kiingereza .
Kama swala la wageni sisi tunatembelewa na wageni toka mataifa mbalimbali kama china , ufaransa, Germany, swideni, hispania nk na haiwezekani mtu kujifunza lugha za dunia nzima.
Kuhusu wepesi wa lugha inategemeana na uzoefu kwani waweza kuta kimasai ni lugha nyepesi kuliko kiingereza.
 
Mbona wachina wengi hawajui kingereza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…