Kuna office nimeitembelea leo,office nzima mpaka mkurugenzi hawajui kuongea Kiingereza

Kuna office nimeitembelea leo,office nzima mpaka mkurugenzi hawajui kuongea Kiingereza

Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, Sema kweli Kiingereza Bado ni Baba mkwe kwa graduates wengi wa nchi hii, sijui shida ni nini, hakuna kisingizio sijui lugha ya Taifa imefanyeje, sijui ni lugha tu kama zingine, ingekuwa hivyo basi tungesoma na kufanya research zetu kwa kisukuma au kiha au ku defend hizo thesis mbele za maprofessor kwa kizaramo.

hata kama mtu kasoma shule za Serikali lakini kuanzia kidato cha Kwanza mpaka Doctorate ni kimombo mwanzo mwisho sasa sijui wanashindwa nini, na walifaulu aje hawa watu kama kweli hawajui 🤔🤗

Ni aibu kwa kweli, Bora ambaye hakusoma ana la kujitetea, graduates either from university or college seriously 😳
Kuna nchi nyingi za Ulaya zina lugha zao za taifa tofauti na Kiingereza. Lakini kwa nini wananchi mfano wa Ujerumani au Ufaransa wanaweza kuzungumza Kiingereza vizuri kuliko Watanzania! Ni kwa sababu wapo karibu na jamii za wazungumza Kiingereza huko Ulaya.

Sasa, tukija Tanzania, mtu kweli amesoma sekondari kwa Kiingereza cha kuunga unga, ameajiriwa lakini inapita hata miaka kumi hajawahi kuwasiliana na wateja kwa Kiingereza kwa sababu wateja wake ni Waswahili. Mtu kama huyu uwezo wake wa kuzungumza Kiingereza unadumaa tofauti na yule ambaye labda yupo kwenye kampuni ya utalii.

Suluhisho ni kutumia Kiingereza kuanzia shule ya msingi mpaka vyuoni ili angalau watoto wawe na mazoezi ya kutosha ya Kiingereza.
 
Unajua mtu mpaka anakuwa Mkurugenzi Tanzania minimum education level mara nyingi ni Master's.
Sasa lijitu limekaa darasani linagundishwa kwa KIINGEREZA na kujibu kwa KIINGEREZA zaidi ya miaka 14 halafu halijui kuongea kiingereza.
Huu ni uhuni. Korea, China na wengine husoma kwa lugha zao. Kwahiyo msijitetee nyie mambumbumbu
Mkurugenzi ni cheo, si lazima iwe daraja la usomi. Ni nafasi ya uongozi inayotolewa kwa mtu kutokana na uzoefu, ujuzi, au sifa anazokidhi kwa mujibu wa taasisi au kampuni.

Kwa hivyo, Mkurugenzi ni cheo cha kazi, si daraja la elimu.

Mbumbumbu mwenyewe, kabla sijasahau.
 
Kinachosikitisha ni kwamba hata kiswahili kinatusumbua, sasa tunajua lugha gani kama sio kiswahili wala kingereza tunachojua.
 
Unajua mtu mpaka anakuwa Mkurugenzi Tanzania minimum education level mara nyingi ni Master's.
Sasa lijitu limekaa darasani linagundishwa kwa KIINGEREZA na kujibu kwa KIINGEREZA zaidi ya miaka 14 halafu halijui kuongea kiingereza.
Huu ni uhuni. Korea, China na wengine husoma kwa lugha zao. Kwahiyo msijitetee nyie mambumbumbu

Hakika sisi walinzi tuliosoma human resources tumekuelewa Ila tunabidi kubadilisha Kazi.
 
unashanga mkurugenzi wa ofisi wakati rais wa China taifa kubwa duniani katika kila kitu na yeye pia hajui kingereza
Nyie mambumbumbu acheni kujitetea.
Uchina lugha rasmi ni kichina, lugha ya kusomea darasani ni Kichina.
Tanzania lugha ya kusomea ni KIINGEREZA.
Mkurugenzi minimum education level ni Master's.
Master's kuipata lazima usote darasani miaka kumi na ushehe ukisoma kwa KIINGEREZA, kwanini aogope kuongea kiingereza?
Elimu duni za kuungaunga.
 
Nami nakushangaa kutokutambua hilo mapema kiufupi bongo kama hujasoma english medium primary ni ngumu sana kuwa competent kwenye kingereza maana shule za serikali hazina mfumo mzuri wa kujifunza kiingereza
Naunga mkono hoja.

Sent from my Infinix X669 using JamiiForums mobile app
 
Hii nchi ina vituko sana.

Kuna wageni kutoka marekani wametembelea Tanzania kujifunza mambo flani flani,boss wangu akaniteua mimi na wenzangu wawili tuwaongoze kwenye shughuli zao zilizowaleta.

Cha ajabu kuna office tumeenda leo,office nzima hakuna anayeweza kuongea kiingereza kizuri,hadi mkurugenzi wa office ni zero kwenye kiingereza, eti mkurugenzi akanivuta pembeni akaniambia hayuko vizuri kiafya hivyo anaomba anikabidhi kwa meneja wake ili atusaidie shida yetu,

Meneja nae akazuga eti yuko busy lkn baadae akanivuta pembeni akaniambia huwa anapata shida kuelewa accent ya kimarekani hivyo anaomba niwe namtafsria wanachoongea hawa wageni.
Nimeshangaa sana aisee.
Elimu Bora kutoka CCM
 
Lakini huko uchina hawatumii kingereza popote, sio mtaani wala mashuleni/vyuoni. Sio ajabu kwa mchina, mjerumani, mrusi..nk ila ni ajabu kwa mtanzania kwa sababu ni lugha ameitumia kupata maarifa.
Hadi EU Kuna nchi hawatumii Kiingereza. Ukienda na Kingeregeja unatoka kapa
 
Nami nakushangaa kutokutambua hilo mapema kiufupi bongo kama hujasoma english medium primary ni ngumu sana kuwa competent kwenye kingereza maana shule za serikali hazina mfumo mzuri wa kujifunza kiingereza
 
Hii nchi ina vituko sana.

Kuna wageni kutoka marekani wametembelea Tanzania kujifunza mambo flani flani,boss wangu akaniteua mimi na wenzangu wawili tuwaongoze kwenye shughuli zao zilizowaleta.

Cha ajabu kuna office tumeenda leo,office nzima hakuna anayeweza kuongea kiingereza kizuri,hadi mkurugenzi wa office ni zero kwenye kiingereza, eti mkurugenzi akanivuta pembeni akaniambia hayuko vizuri kiafya hivyo anaomba anikabidhi kwa meneja wake ili atusaidie shida yetu,

Meneja nae akazuga eti yuko busy lkn baadae akanivuta pembeni akaniambia huwa anapata shida kuelewa accent ya kimarekani hivyo anaomba niwe namtafsria wanachoongea hawa wageni.
Nimeshangaa sana aisee.
Kwani kuna shida wapo tanzania na tanzania lugha kuu inajulikana ni kiswahili wewe ndio mwenye shida ulipaswa kuwauliza mapema na uandae mazinga rafiki ili mambo yaende sawa
 
Mbona kawaida tu, baada ya yote kiingereza sio kipimo cha kuwa na akili nyingi. Ni kimatumbi cha wazungu tu.

Kama mpaka wana ofisi ya hadhi ya kutembelewa basi ni wazi kiingereza hakina umuhimu kwao.
Haya bana ndio umekuja kutudhalilisha huku...
 
Hadi EU Kuna nchi hawatumii Kiingereza. Ukienda na Kingeregeja unatoka kapa
Inaeleweka kwao, kwa sababu lugha zao zimejitosheleza kuanzia mtaani hadi kwenye taaluma. Leo hii jaribu kumfundisha mtoto wako somo la kemia au fizikia kwa kiswahili ndio utajua kama kiswahili kinajitosheleza au vipi.
 
We ndio mshamba!

Unaweza kukielewa kiingereza Cha wachina,warusi au wavietnum vizuri!!?

Wamarekani sio waingereza wazuri !wanaongea kwa lafudhi Yao ambayo sio pure English kama Great Britain!!

Kwahiyo lafudhi yao sio lazima mbongo aielewe ipasavyo ndio maana kwenye subtitles Wana option ya lafudhi za England, American na n.k!

Kile Cha wamarekani sio kiingereza halisi kile Bali ni American English!!

Hivyo tu!
 
Back
Top Bottom