Kuna office nimeitembelea leo,office nzima mpaka mkurugenzi hawajui kuongea Kiingereza

Kingereza sio sawa na Kikurya ambacho ni lugha ya kabila moja tu, Kikurya sio sawa hata na Kiswahili. Kiswahili ni zaidi ya Kikurya na Kingereza ni zaidi ya Kiswahili. Kingereza ni lugha ya kimataifa.
 
Kuna jamaa mmoja yeye ni ofisa elimu kata, siku moja mchungaji alimpa kazi ya kutafsiria waumini anachozungumza mgeni anayeongea kiingereza. Kwa tunaojua kiingereza chote cha uingereza na marekani tuliishia kucheka sana kwa jinsi huyo msomi wetu alivyokuwa anatafri sentensi na maneno ya kiingereza cha mgeni wetu. Shati la mikono mirefu lilitafsiriwa long hand badala ya long sleeves.Jamaa kuona tunamcheka akashuka jukwaani na kuanza kujitetea kuwa mzungu anaongea kiingereza kigumu hawezi kutafsiri hiyo kazi apewe mkalimani mwingine anayejua kiingereza vema. Kiufupi ni kwamba kuna mabosi wengi sana hawamudu kuongea kiingereza vema huku wana degree
 
Kinachonishangaza Mimi mbona kuna wakurugenzi wachina, wajapan, warussia, wafrance hawajui kiingereza na hawaoni kuwa ni tatizo?
 
Uongo, hizo nchi zote raia akisoma Kingereza lazima akijue vizuri sana.
Macron anaongea Kingereza kizuri.
Wengi wanababaisha kwani ni lugha ya 3 mpaka ya 4, unakuta mtu anaongea kiingereza chenye rafudhi ya kidutch, french, Spain, hivyo hata kueleweka mtihani, sema walishatuzidi kifikra kuwaona they are right all the time
 
Kinachonishangaza Mimi mbona kuna wakurugenzi wachina, wajapan, warussia, wafrance hawajui kiingereza na hawaoni kuwa ni tatizo?
wale nchi zao ziko mbali sana kiufundi. Mfinyanga vyungu tu ni boss katika kijiwe chake. Sisi hatuthaminiani ufundi wetu. Wenzetu wanathamini sana vipawa na vipaji vya wananchi wao, mchoraji tu utakuta ni milionea na nchi inamtambua na kumthamini
 
Hivi kingereza ni nini!? Zaidi ya kuwasiliana....kutoa ujumbe upande huu na kuufikisha upande ule nini cha mno... Na kama uliowaendea wanazungumza kiswahili na wewe pia, ya nini kuhangaika na lugha yenye changamoto kwao....ni wapi ilipoonekana kuwa kingeleza ndio akili au hela.
Kwangu mie kama ikija nafasi ambayo itanilazimu kutumia lugha ya kigeni na nikajua nnaeongea nae hana uelewa na lugha nnayoiongea hapo nitaunga unga mpaka anielewe ....lakini sio kwa kutaka kujionyesha kuwa mimi ni bora kwa kuongea lugha husika....hii inaturudisha nyuma na kutufanya wajinga zaidi....tunasahau kutafuta maarifa sahihi tunahangaika la lugha....halafu kichwani 0 ukipewa kazi, au mradi zaidi ya hicho kinge.....mambo yanakuwa mengi. Tupunguze mambo na kujipa umuhimu ....wakija wao wakaongea kiswahili kwa kukosea tupo tayari kuwafundisha kwa staha....akikosea mswahili kuongea kingeleza tunamcheka kama hakutakiwa kukosea. Huo nao ni ujinga mkubwa.
 
Wengi wanababaisha kwani ni lugha ya 3 mpaka ya 4, unakuta mtu anaongea kiingereza chenye rafudhi ya kidutch, french, Spain, hivyo hata kueleweka mtihani, sema walishatuzidi kifikra kuwaona they are right all the time
Lafudhi sio tatizo kwenye Lugha, kuna watu wanaongea Kiswahili kwa lafudhi ya Kisukuma au kikurya lakini hakuna mtu anasema hawajui Kiswahili. Tatizo Watanzania wengi waliomaliza hata chuo kikuu hawawezi kabisa kuzungumza Kiingereza kwa zaidi ya dakika moja au mbili mfano katika kujitambulisha, kuelezea jambo, mdahalo n.k yani wana msamiati haba/duni wa kufanya mazungumzo hata ya kawaida tu.
 
Kuna shule au chuo ambacho kinafundisha english masaa 24 cha serikali, pia ukishindwa kumaster lugha utotoni ngumu sana kutoboa
 
Kingereza ni lugha ya kimataifa, kama hao watu wa hiyo taasisi walisoma kwa Kingereza mpaka kidato cha nne, sita au chuo halafu bado hawajui Kingereza hilo ni tatizo. Kama hawajafika angalau kidato cha nne hilo sio tatizo.
 
Uongo, hizo nchi zote raia akisoma Kingereza lazima akijue vizuri sana.
Macron anaongea Kingereza kizuri.

Nchi nilizotaja hapo juu nimekaa huko decades mbili, nawajua hao watu vizuri sana. Paris moja ya jiji kubwa Duniani, ukienda kwenye public office na kiingereza chako kupata huduma ni ngumu.
Unaniita muongo kwasababu umesikia Macron anaongea kiingereza kwa Samia hajui kuongea hiyo lugha?
 
Mgeni anapokuja Bongo mara nyingi anaandaa mkalimani kabisa kwasababu anajua English sio lugha ya Taifa.

Wewe upo Kinondoni Mkwajuni mwaka wa 30 huu unashindwa kutambua jambo dogo kama hilo.

Usikute hata mwenye hiyo kampuni hajui Kingereza na anaimiliki ila wewe unajua Kingereza umeajiriwa. Unaona?
 
Hilo sio suala la msingi, hakuna tatizo kama mtu ambaye Kingereza hakikuwa lugha yake ya kufundishia kutojua Kingereza, ni tatizo kutofahamu Kingereza kama kilikuwa kinatumika kama lugha yako ya kufundishia tena kwa miaka 4, 6 au zaidi na pia kama Kingereza kinatumika katika shughuli rasmi za serikali kama mahakamani.
 
Vipi hao wamarekani kiswahili chao kikoje?
Swali je wanao ende huko marekani ambao hawajui kimombo huwa wanatumia njia gani ya mawasiliano

Nadhani njia hiyo hiyo aliyotumia yeye ya ukalimani Ndiyo inayo tumika duniani kote Tena huko majuu wao wapo watu rasmi wanajulikana kama translator
 
Kingereza ni mojawapo ya lugha za taifa la Tanzania, wewe ndiye hujui.
 
Kuna namna fulani mleta uzi ana hoja ila kashindwa tu kuiwasilisha. Hebu fikiria hiyo ofisi pengine ina mhasibu au HR au hata wafanyakazi wa taaluma fulani fulani kama mtaalamu wa mambo ya maendeleo ya jamii kama ni NGO, kuna waalimu kama ni shule, kuna mkandarasi kama ni kampuni ya ujenzi.

Sasa swali ni hawa watu waliwezaje kufanikiwa kimasomo ikiwa kiingereza wasichokifahamu vyema ndio lugha yetu ya kufundishia?

Kwa mtanzania yoyote mwenye elimu ya kuanzia diploma tunategemea afahamu vyema lugha ya kiingereza sababu ndio lugha aliyofunzwa nayo shuleni.

Ni kweli kiingereza sio kipimo cha akili ila kwa mfumo wetu wa elimu ni moja ya vipimo muhimu.
 
Mwanangu Bado mindset yako imejaa kasumba ya kwamba kujua kiingereza ni swala la maana sana. Nchi kubwa za wenzetu viongozi wao hata wakienda huko Magharibi hawajawahi kuongeza kiingereza . Unajua kwanini ? Ni kwasababu kuongea kwao kiingereza Kuna I praise lugha hiyo na kusahau ya kwao ambao ni utamaduni wao! Kutana na Vladmir Putin huyo mshikaji popote huongea Kirusi. Kuna siku mkutano na waandishi alijaribu kuongea kijerumani ikawa stori kubwa. Kutana Xi Jing Ping vivohivyo ni kichina tu.
Kwahiyo kulikuwa na uwezekano kabisa we unayejua kimombo ukaongea na Wamarekani then unaongea na wa home.
Nb.
Mbona wao wakiongea Kiswahili ovyoovyo tunawachekelea tu hatuwabezi? Au ndo inferiority complex?
 
Mbona wakieenda kwa PUTUN, CHINA, KOREA, JAPANI wao ndyo wanajiandaa kujua ABC ya host language na utamaduni, mila na desturi. Kuongea ngeli kwa ufasaa siyo ujanja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…