Kuna ongezeko kubwa la maambukizi ya VVU kwa wasichana wenye umri wa miaka 15-24 Tanzania

Kuna ongezeko kubwa la maambukizi ya VVU kwa wasichana wenye umri wa miaka 15-24 Tanzania

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
378
Reaction score
766
Maambukizi ya VVU miongoni mwa wasichana wenye umri wa miaka 15-24 yameongezeka kwa kiwango cha kutisha, kwa mujibu wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (Tacaids).

Kulingana na takwimu, maambukizi ya VVU kwa wasichana katika kundi hili la umri yameongezeka kutoka asilimia 14 katika kipindi cha 2016/17 hadi asilimia 30 katika kipindi cha 2022/23.

Kulikuwa na kupungua kwa maambukizi miongoni mwa makundi mengine ya umri isipokuwa kundi la umri wa miaka 15-24, na kwa sasa, Watanzania 1,548,000 wanaishi na VVU.

Kaimu mkurugenzi mtendaji wa Tacaids, Dkt. Jerome Kamwela, alisema wanaume wakubwa, hasa wenye umri kati ya miaka 30 na 60, wamebainika kuwa sababu kuu ya kuongezeka kwa maambukizi miongoni mwa wasichana wadogo.

Alisema kuna haja ya kuzingatia suala hili kwa umakini katika jamii, akibainisha kwamba si wasichana tu bali pia wavulana wa kundi hilo la umri wapo kwenye hatari kubwa kutokana na mazingira yanayohimiza mahusiano ya kingono kati ya watu wa rika tofauti.

====================For English Audience Only=====================
Alarm as HIV prevalence doubles among girls aged 15-24 years in Tanzania

HIV incidences among young girls aged 15-24 years have alarmingly doubled, according to the Tanzania Commission for AIDS (Tacaids).

According to statistics, HIV infections among girls in this age group have increased from 14% in the 2016/17 period to 30% in 2022/23.

There was a decrease across other age groups except the 15-24-year population, and as of now, 1,548,000 Tanzanians are living with HIV.

Tacaids acting executive director, Dr Jerome Kamwela, said older men, specifically between 30 and 60 years, have been identified as a major contributing factor to the rising prevalence among young girls.

He said serious attention is required at the societal level, noting that not only girls but also boys in the same age group pose significant risks due to environmental factors that encourage sexual relationships between individuals of different age groups.
 
Hilo ndilo kundi la wasichana wenye tamaa zaidi, wote wanataka iPhone macho matano na chumba kizuri chenye TV inch 80 wakati hawana kazi. Wababa na wazee wanatumia tamaa hizo kujiokotea.

Vijana wengi wa umri huo nao wanaenda kujichukulia huo ugonjwa kutoka kwa hao mabinti baada ya kuupata kwa hao wababa na wazee.

Kabla ya kufanya ngono, pimeni afya zenu. Tamaa mbele, mauti nyuma!
 
Kwa hiyo midingi iliyoungua ndiyo inayoambukiza moto hao wasichana? Basi hao wasichana tamaa za kukimbilia fedha za hao madingi zitawaponza. Kama wanataka ngono wasubiri waolewe na watu walio salama saizi yao, kwanza wakapime.

Hata hao wasichana kama wana ngoma nao huambikiza madingi wasio na kitu hicho. Kuna midingi wake zao wamezeeka hupenda wasichana kwa kuwa wana hela za kuwahonga hususani wanachuo wana njaa kali sana kutaka pocket money
 
Hilo ndilo kundi la wasichana wenye tamaa zaidi, wote wanataka iPhone macho matano na chumba kizuri chenye TV inch 80 wakati hawana kazi. Wababa na wazee wanatumia tamaa hizo kujiokotea.

Vijana wengi wa umri huo nao wanaenda kujichukulia huo ugonjwa kutoka kwa hao mabinti baada ya kuupata kwa hao wababa na wazee.

Kabla ya kufanya ngono, pimeni afya zenu. Tamaa mbele, mauti nyuma!
Ukimsoma vizuri mtoa mada, inaonekana wanaambukizwa zaidi watoto/mabinti wenye miaka 15-24 na jinsia me wa umri 30-60, watu wenye umri wa kuweza kuwa baba zao 🙂 Tafsiri ya moja kwa moja ni tuna pedophiles wamejaa kurubuni watoto/mabinti
 
Hilo ndilo kundi la wasichana wenye tamaa zaidi, wote wanataka iPhone macho matano na chumba kizuri chenye TV inch 80 wakati hawana kazi. Wababa na wazee wanatumia tamaa hizo kujiokotea.

Vijana wengi wa umri huo nao wanaenda kujichukulia huo ugonjwa kutoka kwa hao mabinti baada ya kuupata kwa hao wababa na wazee.

Kabla ya kufanya ngono, pimeni afya zenu. Tamaa mbele, mauti nyuma!

Na nyie mnaokulana na wafanyakazi wa ndani endeleeni. Mtoto wa 20s kaja kwako kufanya kazi unaanza kumtamani ndani ya nyumba yako na mkeo / partner. Unaanza kumla…….. endeleeni
 
Back
Top Bottom