Kuna picha unaitazama kwa sekunde chache tu, lakini moyo wako unaendelea kuizungumza kwa muda mrefu

Kuna picha unaitazama kwa sekunde chache tu, lakini moyo wako unaendelea kuizungumza kwa muda mrefu

Zack Abdul

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2026
Posts
1,194
Reaction score
911
Hii ni picha yangu bora zaidi kwa miaka yote, si kwa sababu ya uzuri wake bali kwa sababu ya somo kubwa lililofichwa ndani yake.

Sisi binaadamu mara nyingi tunaamini kwamba mtu mwenye hali ya chini ndiye anayepaswa kupewa na yule mwenye nacho. Lakini watoto hawa wametufundisha somo tofauti kabisa.

Mmoja alianza kutoa mia yake ya break, akampa Mhe. Rais. Mwingine akafuata. Mwisho wa yote, Mhe. Rais akajikuta ameondoka na TSh 2,800 fedha ambazo watoto hawa walitoa kutoka kwenye kile kidogo walichokuwa nacho mifukoni.

Hawakuwa na vingi, lakini walitoa kwa moyo.

Wakati mwingine tunasahau kwamba thamani ya kutoa haipimwi kwa kiasi unachotoa, bali kwa moyo uliokufanya utoe.

Watoto hawa wametukumbusha jambo moja kubwa: Wengi wetu tumezoea kufikiria kupokea, lakini si mara zote tunakumbuka kutoa.

Picha hii ibaki kuwa ukumbusho kwamba hata kile kidogo ulicho nacho kinaweza kuwa kikubwa sana kwa mwingine. Kua sababu ya Tabasamu la mtu leo. 📌🇹🇿

Dr.Zack ✍️
IMG-20260926-WA0054.jpg
IMG-20260926-WA0051.jpg
IMG-20260926-WA0055.jpg
IMG-20260926-WA0057.jpg
 
Machoni kama watu-AY ft Lady Jaydee
 
Back
Top Bottom