Kuna raha gani mwanasiasa unakula kushiba ilhali wapiga kura wana shinda njaa?!

Kuna raha gani mwanasiasa unakula kushiba ilhali wapiga kura wana shinda njaa?!

Li ngunda ngali

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2023
Posts
707
Reaction score
2,572
Majimboni kwao wengi wao hali ya wapiga kula ni ya kutisha na ugumu wa maisha unaowasumbua.

Hakika, matumbo ya wakubwa wale ukiyaona yameshiba na huenda yamebeba na hata kipolo cha kesho!

Fikiria mwananchi wa hali ya chini anavyopambana kupiga magoti na kuchuchumaa kwa kila stairi kuchimbua maji makorongoni na bado maji hayapatikani! Ajabu, aliyempigia kura anakula na tumbo kufutuka, hali inayompelekea japo kuchuchumaa ipasavyo anashindwa?!
 
Mwenye shibe hamjui mwenye tatizo
20230429_115906.jpg
 
😀😀😀 Hiyo ndio maana halisi ya siasa! Mwenye njaa humtafutia mwenye njaa mwingine nafasi ya kupata shibe akitegemea nae atapatiamo.

Cha ajabu akishashiba hamkumbuki aliyempa nafasi ya kupata ulaji hadi njaa itakapomuuma tena
 
Mwalimu Nyerere alisikitishwa mno na hili jambo.

Hakupenda kabisa KUONA WATU anaowatawala wanakuwa omba omba.

VIONGOZI WA Leo wanajiona miungu WATU.
 
Aliyeshiba hamkumbuki mwenye njaa, wewe unayeuliza hivyo amini nakwambia ukiingia kwenye siasa utafanya hayo hayo.
 
Back
Top Bottom