Kuna rocket imetumwa huko angani ikagonge mwamba unaohatarisha kugonga dunia

Kuna rocket imetumwa huko angani ikagonge mwamba unaohatarisha kugonga dunia

MakinikiA

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2017
Posts
5,104
Reaction score
6,827

Dart: Mpango wa kulishambulia jiwe kubwa la Dimorphos linalokaribia kugonga dunia wazinduliwa​

23 Novemba 2021
Imeboreshwa 24 Novemba 2021

jiwe kubwa

CHANZO CHA PICHA,NASA / JHUAPL / STEVE GRIBBEN
Chombo cha anga za juu kinachotarajiwa kugonga jiwe moja kubwa linalokaribia dunia kwa kasi kimezinduliwa .

Chombo hicho cha Nasa kwa jina Dart kinataka kubaini ugumu uliopo katika kuzuia jiwe hilo kugongana na dunia.

Chombo hicho kitaligonga jiwe hilo kwa jina Dimorphos ili kujua ni kiwango gani cha kasi yake kinaweza kubadilika.

Iwapo miamba iliopo angani ilio na ukubwa wa mita chache ingegongana na dunia , ingesababisha athari kubwa.

Falcon 9 - roketi inayobeba chombo hicho cha Dart ilipaa mwendo wa saa mbili alfajiri siku ya Jumatano kutoka kambi ya angani ya Vandenberg mjini Carlifonia.

Safari hiyo ya NASA itatathimini pendekezo la muda mrefu la kumaliza mwamba huo ulioko katika anga za mbali unaoelekea kwenye dunia.

Chombo hiki cha anga za mbali kitaanguka kwenye kitu kinachoitwa Dimorphos kuangalia ni kwa kiasi gani kasi na njia yake inaweza kuharibiwa.

Kama kifusi cha cosmic chenye urefu wa mita mia moja kitagongana na sayari yetu, inaweza kusababisha maafa makubwa.

Hili ni jaribio la kwanza la kuzuwia mwamba huu unaozunguka dunia kwa melengo ya kujifunza jinsi ya kuilinda dunia, ingawa aina hii ya mwamba unaolengwa wakati huu sio tisho.

"Dart itakuwa ikibadili kipindi cha uzio(obiti) ya Dimorphos kwa kiasi kidogo.

Na hilo kusema kweli ndio tu linalohitajika katika tukio ambapo mwamba utagundulika kabla ya muda ,"anasema Kelly Fast, kutoka ofisi ya uratibu wa ulinzi wa sayari ya Nasa.
Jumatano, roketi ya Falcon 9 iliyobeba chombo cha anga za mbali cha Dart itapaa kutoka ngome ya anga za mbali ya Vandenberg Space Force Base iliyopo California.

Infographic

Miamba inayozunguka jua ni mabaki yanayosalia katika ujenzi wa mfumo wa jua, huku mingi ikiwa haina tisho lolote la hatari kwa sayari yetu. Lakini wakati njia ya mwamba inapoziba njia inayozingira jua inapita ile ya dunia ili vitu viwili viweze kupita kwa wakati mmoja, na hivyo mgongano wa vitu hivi viwili unaweza kutokea.

Safari ya chombo hicho -Dart inayogarimu dola milioni 325 (£240m) italenga miamba miwili ambayo uzio wake unakaribiana - inayofahamika kama binary.

Mwamba mkubwa zaidi kati ya miamba hiyo miwili, unaitwa Didymos , ukiwa na ukubwa wa karibu mita 780 , huku mdogo zaidi ukiitwa Dimarphos-wenye upana wa mita mita 160.

Ukubwa wa Dimorphos unaweza kulipuka kwa kiwango cha nguvu sawa na bomu la nyuklia mara nyingi, na kusababisha maafa katika eneo linalokaliwa na watu wengi na kuwajeruhi makumi ya maelfu ya watu.

Miamba hii inayozingira dunia, mithili ya sayari ndogo(Asteroids) yenye milimita za ujazo 300 na mikubwa zaidi inaweza kusababisha uharibifu mkubwa katika sayari, huku miamba mikubwa zaidi ya kilomita 1 inaweza kusababisha athari kote duniani.

Roketi

CHANZO CHA PICHA,NASA
Baada ya kusafiri Dart , kwanza kitaepuka sumaku ya dunia, na kufuata uzio wake kulizingira jua.

Halafu kitazuwia binary kitakapokaribia umbali wa katika eneo la maili milioni 6.7 za dunia Septemba 2022.

Dart kitapasua na kuingia ndani ya Dimorphos kwa kasi ya karibu mita 15,000 kwa saa (6.6 kilomita kwa sekunde). Hii inatarajiwa kubadili kasi ya mwamba huo kwa kasi ya milimita moja kwa sekunde-na matokeo yake kuharibu uzio wake unaozingira Didymos.

Ni mabadiliko madogo sana, lakini inaweza kutosha tu kugonga kitu kinachoenda kugongana na dunia.

Infographic

Kuna miamba mingine mingi midogo inayozingira jua kuliko mikubwa na kwa hiyo kuwa na uwezekano wa tisho ambalo tumewahi kukabiliana nalo -kama tutawahi kukabiliana nalo-huenda litakuwa ni kutoka kwa mwamba wenye ukubwa wa aina hii ,"amesema Tom Statler, mwanasayansi anayesimamia safari hii katika Nasa.

Dart kinabeba kamera inayoitwa Draco ambayo itatoa picha za miamba yote inayozingira jua na kusaidia chombo kujiendeleza katika mwelekeo sahihi ili kugongana na Dimorphos.

Takriban siku 10 kabla ya Dart kugonga shabaha yake, chombo cha anga za mbali cha Marekani kitatuma setilaiti ndogo, iliyotengenezwa Italia inayoitwa LiciaCube. Setilaiti hiyo ndogo itatuma duniani picha za tukio, kuondolewa kwa kifusi na shimo lililotokea kutokana na athari ya tukio hilo.

Mabadiliko madogo katika njia ya Dimorphos karibu na Didymos yatapimwa kwa kutumia darubini duniani.

Chombo hicho kina maabara asilia muafaka kwa ajili ya kipimo cha aina hiyo. Kugongwa kwa chombo hicho kutabadili uzio wa Dimorphos uliopo karibu na Didymos kwa takriban 1%, badiliko ambalo linaweza kugunduliwa kwa darubini ya ardhini kwa wiki au miezi kadhaa.

CHANZO CHA PICHA,NASA / JHUAPL / ED WHITMAN
Maelezo ya picha,

Picha ya wakaguzi wamtambo wa miale ya jua wa chombo cha anga za mbali mwezi Agosti
Hatahivyo, iwapo Dart kingejigonga katika mwamba wa wenyewe, muda wake wa uzio unaozunguka Jua ungebadilika kwa karibu 0.000006%, jambo ambalo lingechukua miaka mingi kulipima.

Mwamba wa binary ni mdogo sana kiasi kwamba hata kwa darubini zenye uwezo mkubwa wa kuvuta picha za mbali, huonekana kama nukta ya mwangaza.
 
Waache kujipa kiki hao jamaa!!Dunia italindwa na yule alieitengeneza Dunia ilivyo!!!!Tena wasije wakafanya yao wakidhani wanatengeneza kumbe ndio majanga yakazidi kwa Dunia!!Hekima ya Binadamu ni upumbavu kwake yeye alieitengeneza Dunia!!WATAJUAJE KAMA HILO JIWE NDIO NGUZO YENYE KANI ISABABISHAYO UTULIVU KWA SAYARI ZOTE???
 
waache kujipa kiki hao jamaa!!Dunia italindwa na yule alieitengeneza Dunia ilivyo!!!!Tena wasije wakafanya yao wakidhani wanatengeneza kumbe ndio majanga yakazidi kwa Dunia!!Hekima ya Binadamu ni upumbavu kwake yeye alieitengeneza Dunia!!WATAJUAJE KAMA HILO JIWE NDIO NGUZO YENYE KANI ISABABISHAYO UTULIVU KWA SAYARI ZOTE???
Shkamoo
 
Hili ni dili la kuchota matrillion kwa kutishiana vitu ambavyo havipo, hapa nchi zote tutachangishwa pesa kwa madai wanarusha makombora ya kulipiga hilo jiwe, kumbe wanarusha sattelite zao tu, na mchango tunalipishwa
 
Title yako imekaa kishabiki shabiki na kiumbea umbea mno. Unnecessary sensationalism! (Afadhali mods wameibadilisha!)

Wanasayansi wanaamini kuwa huko nyuma dunia ilishawahi kugongwa na mawe haya makubwa (asteroids) na wana ushahidi huo. Jiwe la mwisho ni hili lililoua viumbe wengi duniani na kuondoa ufalme wa akina dinosaurs; na wanyama wengine lukuki.

Mawe haya yanasafiri kwa kasi ya ajabu na yanapopiga uso wa dunia yanavuvumua vumbi na uchafu mwingi ambao unaweza kubakia angani kwa miaka mingi. Vumbi na uchafu huu huenea dunia nzima na kuziba miali ya jua kabisa kabisa mpaka dunia inaingia katika kile wanachokiita deep freeze. Ina maana dunia inaganda kabisa na kutandwa na barafu kwa vile hakuna mwanga wa jua kwa muda mrefu. Na bila mwanga wa jua ina maana hakuna photosynthesis wala nishati ya aina yo yote. Matokeo yake ni vifo vya jumla kwa viumbe wengi.

Yapo mawe yanayoonyesha kuwa yatakuja kuipiga dunia huko mbele ya safari na NASA wana kitengo maalum kinachoshughulika na tatizo hili na mpaka sasa kuna nadharia tatu zilizopendekezwa kuweza kujiponya siku ikigundulika kuwa kuna jiwe linatujia huko:

1. Kurusha chombo chenye uzito na nishati maalum na kwenda kuligonga hilo jiwe huko angani likiwa mbali na dunia. Lengo hapa siyo kulisambaratisha bali ni kujaribu kulisukuma kidogo (nudge) ili liweze kuacha njia yake ya mzunguko (orbit) na hivyo kuliepusha kugongana na dunia.

2. Kurusha rocket yenye nguvu iliyobeba bomu kubwa la nyuklia na kwenda kulitandika hilo jiwe na kulisambaratisha. Hii hata hivyo inaweza tu kuishia kulimega hilo jiwe katika vipande vingi ambavyo vinaweza kuleta hatari zaidi duniani. Na kukitokea mushkeli wakati wa kurusha hiyo rocket hilo bomu linaweza kuturipukia hapa hapa duniani na kuleta madhara makubwa.

Ili kuepuka kulimega vipande vipande lipo pendekezo la kwenda kulipua bomu hilo karibu na jiwe hilo. Ile nguvu ya mripuko (boom) inaweza kutosha kulisukuma kidogo hilo jiwe likiwa zima na kuliondoa katika orbit yake.

3. Kurusha chombo chenye mionzi mikali ya laser na kwenda kujaribu kulimulika jiwe hilo na mionzi hiyo. Mawe haya mengi yana barafu iliyoganda na likipigwa na mionzi mikali kwa muda barafu inaweza kuyeyuka na hivyo kupunguza uzito wake na hii, wanadai, inaweza kusababisha liondoke kwenye orbit yake inayolifanya ligongane na dunia.

Hata bila kuyeyusha barafu yake, mionzi hii ya laser inaweza kufanya kazi sawa na utando wa buibui na hivyo kulisogeza jiwe hilo polepole nje ya orbit yake na hivyo kuepusha mgongano wake na dunia.

NASA leo wamerusha chombo kujaribu nadharia ya kwanza kama inafanya kazi kwa sababu dunia kupigwa na asteroid nyingine ni suala la muda tu. Elon Musk anarusha maroketi haya kila leo hatusikii cho chote lakini leo umeshusha ushabiki wa kufa mtu eti anga lilibadilika. Lilibadilika wapi? Labda kama ulikwenda kushuhudia wakati roketi hilo likirushwa huko California. Ni wazi hii habari hukuiandika mwenyewe na umefanya plagiarism mahali fulani (BBC Swahili) na sina uhakika kama una ufahamu wa kutosha na habari yenyewe pamoja na implications za kiujumla za kinachozungumziwa.

Wakati tunahangaika na tozo, ufisadi wa kutisha, kutengeneza madawati, kujenga nyumba za walimu, kujenga vyoo vya shimo vya kutosha mashuleni, ushirikina, ukosefu wa umeme na maji, siasa za hovyo za kuoneana hizi, wenzetu huko hawalali wanahangaika na mambo kama haya mazito. Tuombe wafanikiwe kwa sababu siku moja pengine wataweza kuokoa maisha ya viumbe hapa duniani. Hata wakishindwa wao pia wanahangaika kutafuta makazi katika sayari zingine huko wanaweza wakaondoka zao na kutuacha hapa siku mambo yakibumburuka!

N.B: Bajeti ya NASA kwa mwaka huu wa fedha ni dola bilioni 23.3. Bajeti nzima ya nchi yako kwa mwaka huu wa fedha ni kiasi gani?
 
Vijana wa bongu ujuaji [emoji23][emoji23][emoji23][emoji1373] Mnapinga hata tu. Hata hoja kidogo hamna

Tunaifa la hovyo sana
Nakwambia tuna tatizo kubwa. Sijui ni elimu yetu mbovu. Sijui ni kutopenda kusoma soma ili kuwa na uelewa mpana wa mambo. Tunaweza tu kubishana na kuporomosha matusi lakini kujibu kwa hoja hakuna. Mbongo hata kama hana fununu kabisa na mada inayozungumziwa lazima tu atatia neno tena kwa kutumia nguvu nyingi huku mishipa ya shingo imemtoka. Ukijaribu kumwelewesha anaporomosha matusi.

Kilichofanyika leo ni mkakati wa muda mrefu na ni katika kujaribu kuona kama nadharia mojawapo ya kuiepusha dunia isipigwe na asteroid inafanya kazi. Tuwaache tu wazungu wapambane...sisi tuna mambo yetu ya muhimu zaidi....
 
Hili ni dili la kuchota matrillion kwa kutishiana vitu ambavyo havipo, hapa nchi zote tutachangishwa pesa kwa madai wanarusha makombora ya kulipiga hilo jiwe, kumbe wanarusha sattelite zao tu, na mchango tunalipishwa
Kuhusu matofali huko angani yapo kweli..
Dunia NI "kamchanga "kadogo sana ukilinganisha na hyo mitofali
 
Back
Top Bottom