Title yako imekaa kishabiki shabiki na kiumbea umbea mno. Unnecessary sensationalism!
Wanasayansi wanaamini kuwa huko nyuma dunia ilishawahi kugongwa na mawe haya makubwa (asteroids) na wana ushahidi huo. Jiwe la mwisho ni hili lililoua viumbe wengi duniani na kuondoa ufalme wa akina dinosaurs; na wanyama wengine lukuki.
Mawe haya yanasafiri kwa kasi ya ajabu na yanapopiga uso wa dunia yanavuvumua vumbi na uchafu mwingi ambao unaweza kubakia angani kwa miaka mingi. Vumbi na uchafu huu huenea dunia nzima na kuziba miali ya jua kabisa kabisa mpaka dunia inaingia katika kile wanachokiita deep freeze. Ina maana dunia inaganda kabisa na kutandwa na barafu kwa vile hakuna mwanga wa jua kwa muda mrefu. Na bila mwanga wa jua ina maana hakuna photosynthesis wala nishati ya aina yo yote. Matokeo yake ni vifo vya jumla kwa viumbe wengi.
Yapo mawe yanayoonyesha kuwa yatakuja kuipiga dunia huko mbele ya safari na NASA wana kitengo maalum kinachoshughulika na tatizo hili na mpaka sasa kuna nadharia tatu zilizopendekezwa kuweza kujiponya siku ikigundulika kuwa kuna jiwe linatujia huko:
1. Kurusha chombo chenye uzito na nishati maalum na kwenda kuligonga hilo jiwe huko angani likiwa mbali na dunia. Lengo hapa siyo kulisambaratisha bali ni kujaribu kulisukuma kidogo (nudge) ili liweze kuacha njia yake ya mzunguko (orbit) na hivyo kuliepusha kugongana na dunia.
2. Kurusha rocket yenye nguvu iliyobeba bomu kubwa la nyuklia na kwenda kulitandika hilo jiwe na kulisambaratisha. Hii hata hivyo inaweza tu kuishia kulimega hilo jiwe katika vipande vingi ambavyo vinaweza kuleta hatari zaidi duniani. Na kukitokea mushkeli wakati wa kurusha hiyo rocket hilo bomu linaweza kuturipukia hapa hapa duniani na kuleta madhara makubwa.
Ili kuepuka kulimega vipande vipande lipo pendekezo la kwenda kulipua bomu hilo karibu na jiwe hilo. Ile nguvu ya mripuko (boom) inaweza kutosha kulisukuma kidogo likiwa zima na kuliondoa katika orbit yake.
3. Kurusha chombo chenye monzi mikali ya laser na kwenda kujaribu kulimulika jiwe hilo na mionzi hiyo. Mawe haya mengi yana barafu iliyoganda na likipigwa na mionzi mikali kwa muda barafu inaweza kuyeyuka na hivyo kupunguza uzito wake na hii, wanadai, inaweza kusababisha liondoke kwenye orbit yake inayolifanya ligongane na dunia.
Hata bila kuyeyusha barafu yake, mionzi hii ya laser inaweza kufanya kazi sawa na utando wa buibui na hivyo kulisogeza jiwe hilo polepole nje ya orbit yake na hivyo kuepusha mgongano wake na dunia.
NASA leo wamerusha chombo kujaribu nadharia ya kwanza kama inafanya kazi kwa sababu dunia kupigwa na asteroid nyingine ni suala la muda tu. Elon Musk anarusha maroketi haya kila leo hatusikii cho chote lakini leo umeshusha ushabiki wa kufa mtu eti anga lilibadilika. Lilibadilika wapi? Labda kama ulikwenda kushuhudia wakati roketi hilo likirushwa huko California. Ni wazi hii habari hukuiandika mwenyewe na umefanya plagiarism mahali fulani (BBC Swahili) na sina uhakika kama una ufahamu wa kutosha na habari yenyewe pamoja na implications za kiujumla za kinachozungumziwa.
Wakati tunahangaika na tozo, ufisadi wa kutisha, kutengeneza madawati, kujenga nyumba za walimu, kujenga vyoo vya shimo vya kutosha mashuleni, ushirikina, ukosefu wa umeme na maji, siasa za hovyo za kuoneana hizi, wenzetu huko hawalali wanahangaika na mambo kama haya mazito. Tuombe wafanikiwe kwa sababu siku moja pengine wataweza kuokoa maisha ya viumbe hapa duniani. Hata wakishindwa wao pia wanahangaika kutafuta makazi katika sayari zingine huko wanaweza wakaondoka zao na kutuacha hapa siku mambo yakibumburuka!