Kuna rocket imetumwa huko angani ikagonge mwamba unaohatarisha kugonga dunia

Kuna rocket imetumwa huko angani ikagonge mwamba unaohatarisha kugonga dunia

Waache kujipa kiki hao jamaa!!Dunia italindwa na yule alieitengeneza Dunia ilivyo!!!!Tena wasije wakafanya yao wakidhani wanatengeneza kumbe ndio majanga yakazidi kwa Dunia!!Hekima ya Binadamu ni upumbavu kwake yeye alieitengeneza Dunia!!WATAJUAJE KAMA HILO JIWE NDIO NGUZO YENYE KANI ISABABISHAYO UTULIVU KWA SAYARI ZOTE???
Tumtukuze bwana Mungu wetu....
 
Waache kujipa kiki hao jamaa!!Dunia italindwa na yule alieitengeneza Dunia ilivyo!!!!Tena wasije wakafanya yao wakidhani wanatengeneza kumbe ndio majanga yakazidi kwa Dunia!!Hekima ya Binadamu ni upumbavu kwake yeye alieitengeneza Dunia!!WATAJUAJE KAMA HILO JIWE NDIO NGUZO YENYE KANI ISABABISHAYO UTULIVU KWA SAYARI ZOTE???
Asante .
 

Dart: Mpango wa kulishambulia jiwe kubwa la Dimorphos linalokaribia kugonga dunia wazinduliwa​

23 Novemba 2021
Imeboreshwa 24 Novemba 2021

jiwe kubwa

CHANZO CHA PICHA,NASA / JHUAPL / STEVE GRIBBEN
Chombo cha anga za juu kinachotarajiwa kugonga jiwe moja kubwa linalokaribia dunia kwa kasi kimezinduliwa .

Chombo hicho cha Nasa kwa jina Dart kinataka kubaini ugumu uliopo katika kuzuia jiwe hilo kugongana na dunia.

Chombo hicho kitaligonga jiwe hilo kwa jina Dimorphos ili kujua ni kiwango gani cha kasi yake kinaweza kubadilika.

Iwapo miamba iliopo angani ilio na ukubwa wa mita chache ingegongana na dunia , ingesababisha athari kubwa.

Falcon 9 - roketi inayobeba chombo hicho cha Dart ilipaa mwendo wa saa mbili alfajiri siku ya Jumatano kutoka kambi ya angani ya Vandenberg mjini Carlifonia.

Safari hiyo ya NASA itatathimini pendekezo la muda mrefu la kumaliza mwamba huo ulioko katika anga za mbali unaoelekea kwenye dunia.

Chombo hiki cha anga za mbali kitaanguka kwenye kitu kinachoitwa Dimorphos kuangalia ni kwa kiasi gani kasi na njia yake inaweza kuharibiwa.

Kama kifusi cha cosmic chenye urefu wa mita mia moja kitagongana na sayari yetu, inaweza kusababisha maafa makubwa.

Hili ni jaribio la kwanza la kuzuwia mwamba huu unaozunguka dunia kwa melengo ya kujifunza jinsi ya kuilinda dunia, ingawa aina hii ya mwamba unaolengwa wakati huu sio tisho.

"Dart itakuwa ikibadili kipindi cha uzio(obiti) ya Dimorphos kwa kiasi kidogo.

Na hilo kusema kweli ndio tu linalohitajika katika tukio ambapo mwamba utagundulika kabla ya muda ,"anasema Kelly Fast, kutoka ofisi ya uratibu wa ulinzi wa sayari ya Nasa.
Jumatano, roketi ya Falcon 9 iliyobeba chombo cha anga za mbali cha Dart itapaa kutoka ngome ya anga za mbali ya Vandenberg Space Force Base iliyopo California.

Infographic

Miamba inayozunguka jua ni mabaki yanayosalia katika ujenzi wa mfumo wa jua, huku mingi ikiwa haina tisho lolote la hatari kwa sayari yetu. Lakini wakati njia ya mwamba inapoziba njia inayozingira jua inapita ile ya dunia ili vitu viwili viweze kupita kwa wakati mmoja, na hivyo mgongano wa vitu hivi viwili unaweza kutokea.

Safari ya chombo hicho -Dart inayogarimu dola milioni 325 (£240m) italenga miamba miwili ambayo uzio wake unakaribiana - inayofahamika kama binary.

Mwamba mkubwa zaidi kati ya miamba hiyo miwili, unaitwa Didymos , ukiwa na ukubwa wa karibu mita 780 , huku mdogo zaidi ukiitwa Dimarphos-wenye upana wa mita mita 160.

Ukubwa wa Dimorphos unaweza kulipuka kwa kiwango cha nguvu sawa na bomu la nyuklia mara nyingi, na kusababisha maafa katika eneo linalokaliwa na watu wengi na kuwajeruhi makumi ya maelfu ya watu.

Miamba hii inayozingira dunia, mithili ya sayari ndogo(Asteroids) yenye milimita za ujazo 300 na mikubwa zaidi inaweza kusababisha uharibifu mkubwa katika sayari, huku miamba mikubwa zaidi ya kilomita 1 inaweza kusababisha athari kote duniani.

Roketi

CHANZO CHA PICHA,NASA
Baada ya kusafiri Dart , kwanza kitaepuka sumaku ya dunia, na kufuata uzio wake kulizingira jua.

Halafu kitazuwia binary kitakapokaribia umbali wa katika eneo la maili milioni 6.7 za dunia Septemba 2022.

Dart kitapasua na kuingia ndani ya Dimorphos kwa kasi ya karibu mita 15,000 kwa saa (6.6 kilomita kwa sekunde). Hii inatarajiwa kubadili kasi ya mwamba huo kwa kasi ya milimita moja kwa sekunde-na matokeo yake kuharibu uzio wake unaozingira Didymos.

Ni mabadiliko madogo sana, lakini inaweza kutosha tu kugonga kitu kinachoenda kugongana na dunia.

Infographic

Kuna miamba mingine mingi midogo inayozingira jua kuliko mikubwa na kwa hiyo kuwa na uwezekano wa tisho ambalo tumewahi kukabiliana nalo -kama tutawahi kukabiliana nalo-huenda litakuwa ni kutoka kwa mwamba wenye ukubwa wa aina hii ,"amesema Tom Statler, mwanasayansi anayesimamia safari hii katika Nasa.

Dart kinabeba kamera inayoitwa Draco ambayo itatoa picha za miamba yote inayozingira jua na kusaidia chombo kujiendeleza katika mwelekeo sahihi ili kugongana na Dimorphos.

Takriban siku 10 kabla ya Dart kugonga shabaha yake, chombo cha anga za mbali cha Marekani kitatuma setilaiti ndogo, iliyotengenezwa Italia inayoitwa LiciaCube. Setilaiti hiyo ndogo itatuma duniani picha za tukio, kuondolewa kwa kifusi na shimo lililotokea kutokana na athari ya tukio hilo.

Mabadiliko madogo katika njia ya Dimorphos karibu na Didymos yatapimwa kwa kutumia darubini duniani.

Chombo hicho kina maabara asilia muafaka kwa ajili ya kipimo cha aina hiyo. Kugongwa kwa chombo hicho kutabadili uzio wa Dimorphos uliopo karibu na Didymos kwa takriban 1%, badiliko ambalo linaweza kugunduliwa kwa darubini ya ardhini kwa wiki au miezi kadhaa.

CHANZO CHA PICHA,NASA / JHUAPL / ED WHITMAN
Maelezo ya picha,

Picha ya wakaguzi wamtambo wa miale ya jua wa chombo cha anga za mbali mwezi Agosti
Hatahivyo, iwapo Dart kingejigonga katika mwamba wa wenyewe, muda wake wa uzio unaozunguka Jua ungebadilika kwa karibu 0.000006%, jambo ambalo lingechukua miaka mingi kulipima.

Mwamba wa binary ni mdogo sana kiasi kwamba hata kwa darubini zenye uwezo mkubwa wa kuvuta picha za mbali, huonekana kama nukta ya mwangaza.
Hawajaugonga tu?
 
Waache kujipa kiki hao jamaa!!Dunia italindwa na yule alieitengeneza Dunia ilivyo!!!!Tena wasije wakafanya yao wakidhani wanatengeneza kumbe ndio majanga yakazidi kwa Dunia!!Hekima ya Binadamu ni upumbavu kwake yeye alieitengeneza Dunia!!WATAJUAJE KAMA HILO JIWE NDIO NGUZO YENYE KANI ISABABISHAYO UTULIVU KWA SAYARI ZOTE???
Sawa hilo ni kwa upande mmoja.

Ila vipi kuhusu matetemeko ya ardhi, tsunami, Magonjwa n.k, je yule 'aliyeitengeneza Dunia' anakuwa amepitiwa?.

Na je vipi kama kujilinda na kuchukua tahadhari pia ni sehemu ya majukumu aliyowapa waishio Duniani?.

Mimi huwa baada ya kuwaza hivyo ulivyowaza hapo lakini pia huwa najaribu kuwaza na upande wa pili.
 
Walishindwa kupambana na Corona iliyopo Duniani wameleta propaganda ya Jiwe sasa hivi hao NASA ni kutisha tuu kila kukisha bila kufanya tafiti za kujiridhisha lile lingine sijui liliishia wapi...
 
Walishindwa kupambana na Corona iliyopo Duniani wameleta propaganda ya Jiwe sasa hivi hao NASA ni kutisha tuu kila kukisha bila kufanya tafiti za kujiridhisha lile lingine sijui liliishia wapi...
Wakiugonga ukapasuka pasuka vipande vidogo vidogo ndo litakuwa balaa zaidi maana watashindwa kuvicontain
 
You know what they are doing,they are trying to justify safari zao nyingi za kwenda anga za juu kwa visingizio ambavyo sivyo.The truth is, wanatengeneza mazingira ya kumleta their fake Messiah,ambaye wanategemea mimi na wewe tutamwamini,ambaye infact atakuwa ndiye the Antichrist.Brother they are preparing a grand deception and illusion which humanity has never witnessed.Wake up.
Wewe ni mental case...
Na huyu unayemwamini sasa, sio wao waliokuletea ?
 
Wakiugonga ukapasuka pasuka vipande vidogo vidogo ndo litakuwa balaa zaidi maana watashindwa kuvicontain
Ni kweli, ni bora wangetuma Solid Rocket Booster kwenda kulisukuma hadi ahera.
 
Wewe ni mental case...
Na huyu unayemwamini sasa, sio wao waliokuletea ?
Wewe ndiye mental case usiyeweza ku-connect the dots.Na si unajua Rais ameagiza Wizara ya Afya ifanye Utafiti kuhusu Afya yenu ya aKili na ushababi maana hamko vizuri.
 
Back
Top Bottom