Kuna rocket imetumwa huko angani ikagonge mwamba unaohatarisha kugonga dunia

Kuna rocket imetumwa huko angani ikagonge mwamba unaohatarisha kugonga dunia

Sasa sayansi tena leo mnaipiga kiwiko wakati moja ya sifa ambazo mnatumia kuipamba quran ni kuonesha mambo ya sayansi yaliyoelezwa ndani ya hicho kitabu?
Hawa Watu Wana vituko kweli kweli Mkuu,yaani anajua kabisa kitu anakitetea hakina mantiki ila atashupaza shingo kisa hekaya za waarabu zinasema jua huzama kwenye chemchemu za matope,na kama ilivyo ada mambo ya dini ni zaidi ya Opium ya Afganistan Kwa wataliban basi ataamini hivyo hivyo na kusema aamin!
😅😅😅
 
Na sisi Tz/Africa tuunde 'NASA' yetu.
hahahahaah Labda nasa Sio NASA nayoijua Mimi,
Napendekeza makao yake Makuu yawe Gambosh maana badala ya kurusha Falcon X au Apollo
Tutarusha nyungo
Halafu mkurugenzi Mkuu wa nasa ya Gambosh awe Mkuu
#Mshana Jr!
😂😂😂😂
 
Simu ni uhalisia kijana na Sayansi yenye matatizo hasa ni Sayansi ya anga,japo kwa ujumla wake Sayansi inashindwa kwenye hitimisho. Soma nilichokiandika hapo juu.

Naishi katika ulimwengu wa Sayansi na napata ugali kupitia huko ila kuna matatizo na uongo mwingi sana.
Ila we jamaa hiki ulichokiandika ingekua ni mwezi april ningesema unafanya pranking

Unakubaliana na sayansi ya simu ila hukubaliana na sayansi ya anga, sasa hiyo simu ina operate vipi bila kutegemea satelite zilizokua installed angani?

Au satelite nazo kwako ni habari za kutungwa tu zisizo na ukweli?
 
Sasa sayansi tena leo mnaipiga kiwiko wakati moja ya sifa ambazo mnatumia kuipamba quran ni kuonesha mambo ya sayansi yaliyoelezwa ndani ya hicho kitabu?
Nani anasema hizi habari ?
 
Wanaacha kupambana na hali ya joto Duniani wanapambana na vitu vya Mungu
 
Hivi katika hii mada ulivyo isoma hujajiuliza chochote kuhusu ukweli wa mada husika au umependa stori na picha ?

Mimi nilivyo soma hii mada cha kwanza nilianza kuhoji au kujiuliza juu ya picha ukiangalia kwa umakini hizo picha ni picha bunifu hakuja picha hata moja ambayo ni halisi.

Kingine kuhusu vipimo na utoaji wa majina na maelezo ya jambo husika,maelezo yanaonyesha ya kuwa wahusika hawana maarifa sahihi juu ya anga na vilivyomo. Swali la msingi nililo jiuliza ni kuwa wametumia mchakato gani kujia ukubwa wa hilo jiwe ?

Nani wa kwanza kutambua uwepo wa jiwe hilo na ilikuwa lini na alijuaje kuhusu jiwe hilo ?

Ngoja nikuelekeze kisha tusipoelewana utajua mwenyewe.

Nimefuatilia hoja zako za picha na madai ya maigizo na hitimisho langu ni kuwa wewe umejikita kwenye picha ambazo ni za kutengeneza ili kumpa taswira rahisi ya uelewa msomaji asiye mwanasayansi na ukatoa hitimisho kuwa ni maigizo.

Sasa mfano tukiachana na picha ukatumiwa namna wanavyogundua kuwa sayari fulani ina mazingira yanayofanana na dunia ukaletewa zile namba, dots na signals ungeelewa?

Umeshawahi kuona mtu akihojiwa polisi akawa anatoa maelezo ya namna mhalifu alivyo halafu kuna mtu anamchora, kisha baada ya hapo inatoka picha inayofanana na mhalifu jinsi alivyo?
Sasa hizi taarifa zinazotumwa na vyombo vya anga ni mfano wa huyo mtu na kuna wachoraji wanaochora ili taswira ya picha itokee kurahisisha ile taarifa.

Unajua kuwa ubongo wako unatafsiri vipi kuwa huyu ni mtu fulani baada ya kumwangalia?
Bila wewe kujua kwa haraka sana ubongo wako unapima alama za urefu wa pua, upana wa mdomo, umbali kutoka pua na mdomo, upana wa paji la uso, mzunguko wa jicho n.k kisha unatoa hesabu kamili na kutuma taarifa za utambuzi kuwa huyu ni fulani ila wewe unachoona ni taswira ya picha yenye rangi ambayo unatengenezewa na huo huo ubongo ili kukurahisishia huo utambuzi.

Taarifa za hesabu za huyo mtu zinatunzwa kwenye kanzidata yako ya kumbukumbu na kila ukimuona ubongo ukifanya zile hesabu zinafanana na ile kumbukumbu iliyotunzwa na kanzidata yako kisha utambuzi unatokea. Ukipata hitilafu katika eneo la utunzaji huyo mtu akija hutaweza mtambua anakuwa kama mtu mpya.

Rangi unazo wewe sio ile object au mtu unayemuangalia. Ubongo wako kupitia macho yako unageuza namba na taarifa za kitu ili wewe ukitambue kwa mfumo wa rangi na picha au tuseme video. Sasa hichi ndicho wakifanyacho wanasansi mpaka unaziona picha ambazo unahisi ni maigizo.

Usiidharau teknolojia na kuiita maigizo,nilikuwa nafuatilia historia ya ugunduzi wa ndege kuna watu walikuja na theory kuwa binadamu angetakiwa kupaa angezaliwa na mabawa tuache kumkufuru muumba. Leo binadamu wanapaa.
 
Ngoja nikuelekeze kisha tusipoelewana utajua mwenyewe.
Nina kichwa chepesi sana kuelewa na kushika mambo. Hili ondoa shaka.

Tuendelee.
Nimefuatilia hoja zako za picha na madai ya maigizo na hitimisho langu ni kuwa wewe umejikita kwenye picha ambazo ni za kutengeneza ili kumpa taswira rahisi ya uelewa msomaji asiye mwanasayansi na ukatoa hitimisho kuwa ni maigizo.
Safi kabisa nashukuru kwa kukiri kwako ya kuwa hizo ni taswira bunifu.

Kingine sijajikita tu katika picha kama umenisoma vizuri nimejikita kadhalika katika uhalisia.

Hii ni sayansi na ina kanuni na hatua zake zake kufikia hitimisho juu ya jambo fulani.

Kadhia inayo elezewa hapo haina njia nyingine mbadala zaidi ya kufika sehemu husika zaidi ya hapo ni makadirio na ndiyo maigizo yenyewe.

Kama waliweza kutoa hitimisho kwanini waliweka picha bunifu na si picha halisi.
Sasa mfano tukiachana na picha ukatumiwa namna wanavyogundua kuwa sayari fulani ina mazingira yanayofanana na dunia ukaletewa zile namba, dots na signals ungeelewa?
Hoja hii haina haja ya kuletewa dots wala nini ni jambo la kueleweka wazi wala halihitaji signals,ni sawa sawa na wanavyolezea maji kwa mujibu wa kemia jambo ambalo maji ni kitu naarufu na hakihitaji kiarifisho (definition) ya kisayansi ndiyo maana wanakosea.

Swali la msingi kwanini waelezee kwa dots au signals jambo ambalo kama kweli wamelidiriki ni kuthibitisha tu. Ni sawa sawa na wewe useme umemuona Ali,kisha kisha umuelezee kwa mtindo ambao hauna uhusiano na Ali.
Umeshawahi kuona mtu akihojiwa polisi akawa anatoa maelezo ya namna mhalifu alivyo halafu kuna mtu anamchora, kisha baada ya hapo inatoka picha inayofanana na mhalifu jinsi alivyo?
Mfano wako haingii hapa sababu sharti la kwanza ni mtu husika amemdiriki mtu husika na wala hapakuwa na haja ya kumchora mtu huyo. Na ushahidi huu hauna mashiko mpaka muhusika adirikiwa yaani picha hufanana na watu hufanana pia. Kwahiyo akiyemuona fulani lazima akamuonyeshe huyo fulani.

Lakini kinachofanana na fulanindi chenyewe hicho.
Sasa hizi taarifa zinazotumwa na vyombo vya anga ni mfano wa huyo mtu na kuna wachoraji wanaochora ili taswira ya picha itokee kurahisisha ile taarifa.
Ngoja nikusaidie kitu kimoja ushawah kuthibitisha au kuhakiki ya kuwa kuna chombo chochote kimewahi kufika kwenye sayari nyingine ? Au unaweza kuthibtisha juu ya uwepo wa Sayari nyingine zaidi ya Dunia ?

Hujiulizi kwanini watu hawajaenda tena mwezini tangu yale maigizo ya Neil ? Wanasingizia bajeti ni kubwa imeshipatia miaka zaidi ya 30 sasa bado tu hawajajipanga kwenda tena ?

Sasa uhalisia upo na tunaishi nao haya maigizo watawaigizia nyinyi msio fikiri na kuhoji na kuhakiki mambo.
Unajua kuwa ubongo wako unatafsiri vipi kuwa huyu ni mtu fulani baada ya kumwangalia?
Najua.
Bila wewe kujua kwa haraka sana ubongo wako unapima alama za urefu wa pua, upana wa mdomo, umbali kutoka pua na mdomo, upana wa paji la uso, mzunguko wa jicho n.k kisha unatoa hesabu kamili na kutuma taarifa za utambuzi kuwa huyu ni fulani ila wewe unachoona ni taswira ya picha yenye rangi ambayo unatengenezewa na huo huo ubongo ili kukurahisishia huo utambuzi.
Hizi stori achana nazo jikite katika hoja ya msingi.
Rangi unazo wewe sio ile object au mtu unayemuangalia. Ubongo wako kupitia macho yako unageuza namba na taarifa za kitu ili wewe ukitambue kwa mfumo wa rangi na picha au tuseme video. Sasa hichi ndicho wakifanyacho wanasansi mpaka unaziona picha ambazo unahisi ni maigizo.

Usiidharau teknolojia na kuiita maigizo,nilikuwa nafuatilia historia ya ugunduzi wa ndege kuna watu walikuja na theory kuwa binadamu angetakiwa kupaa angezaliwa na mabawa tuache kumkufuru muumba. Leo binadamu wanapaa.
Hizi stori mzee achana nazo jenga hoja na kosoa hoja na hakiki hoja na thibitisha hoja.

Nakuuliza swali dogo ukitaka kupima tungamo ya kitu au kipenyo cha kitu sharti ni lipi au masharti ni yapi ?
 
Kumekucha...

Masihi wanayemwandaa kwa haya masafari yao feki ni mpinga Kristo aliyetabiriwa kwenye Biblia au ndo wanataka kusingizia kuwa Yesu karudi mara ya pili kupitia haya maroketi yao?

Umenifurahisha sana mkuu [emoji16][emoji16][emoji16]
Usilolijua ni usiku was giza.
 
Usilolijua ni usiku was giza.
Usiku wa giza kivipi?

Si ueleze sasa hizo conspiracy zako na jinsi wanavyojipanga kumleta huyo masihi feki uliyemsema kwa kurusha haya maroketi yao? Usipoeleza sasa tutajuaje? Maadam umeweka hapa wazi tuvumilie tu tunapoomba ufafanuzi hata sisi tulio gizani.
 
Waache kujipa kiki hao jamaa!!Dunia italindwa na yule alieitengeneza Dunia ilivyo!!!!Tena wasije wakafanya yao wakidhani wanatengeneza kumbe ndio majanga yakazidi kwa Dunia!!Hekima ya Binadamu ni upumbavu kwake yeye alieitengeneza Dunia!!WATAJUAJE KAMA HILO JIWE NDIO NGUZO YENYE KANI ISABABISHAYO UTULIVU KWA SAYARI ZOTE???
Hao wanaenda kufanya milipuko yao ya kuharibu zaidi Dunia huku wanatudanganya eti wamezuia lijiwe lisigonge Dunia. [emoji1787][emoji23][emoji1787] Kwahiyo wameahirisha mwisho wa dunia[emoji1787][emoji23]. Ndo maana joto linazidi Duniani wakati yuko mkorea akili pua kwenye. Maji wao wanalipua angani. Blood fucken this pipo
 
Kuhusu matofali huko angani yapo kweli..
Dunia NI "kamchanga "kadogo sana ukilinganisha na hyo mitofali
Sasa kama tofali ni kubwa kuliko Dunia. Eti wanatuma kifaa kilichotoka Duniani kikagonge hilo. Lidubwana. [emoji849][emoji1787][emoji848][emoji848]. Si litakivuruga hiko kifaa chenu chenye ukubwa hata hafiki wa nchi moja.... Au wanamabomu mazito ya kuvunja hilo lijiwe ambalo ni kubwa snaaaa kiasi kwamba Dunia ni kama mchanga???
 
hapana.hayo mawe yapo mengi.
Ila lililo tishio kwa Sasa NI hilo.
Kutoka hapa duniani mpaka huko angani Kuna umbali mkubwa Sanaa.
Hicho chombo chenyewe kitachukua miezi 10 kulifikia hilo jiwe
ACHA MUNGU AITWE MUNGU
 
Back
Top Bottom