Kuna Sauti inanijia kwamba huenda wabunge 19 wa CHADEMA wana baraka za Mwenyekiti kwa makubaliano maalumu kutotoboa siri

Nataman itokee siku asiwepo hata mwananchi mmoja atakayejitokeza kwenye mikutano ya chadema tenaaaa ili wajue kuwa wananchi wako dissapointed na upinzani kwa kiwango cha hli ya juu
Wame disappoint nini? Si waliwatimua uanachama tayari so mlitaka wafanyeje zaidi? Toka rufaa ipite hazijapita siku 90 or so, but mpaka sasa wale sio wanachama wa CHADEMA pending appeal!
 
Walikata rufaa ndani ya chama muda mrefu sana, kwanini hiyo rufaa mpaka leo haisikilizwi? Mbona mara nyingi kamati/baraza zilikuwa zinakutana kwa dharura na kutoa maamuzi haraka
Baraza kuu ni kubwa kidogo so mobilization inahitaji muda.... Isistoshe bado wapo ndani ya muda wa kusikiliza rufaa haijazidi siku 60-90 toka appeal ipelekwe.
 
Yani unataka ushahidi wa chadema wakichukua ruzuku?

Kwa akili yako tindo unafikiri Mnyika pale alipo anafanya kazi ya ukatibu mkuu bure kwa kujitolea?
Watu wanaoingia kwenye siasa kwa maslahi huwa sio kusaka pesa bali POWER, Influence, Popularity na serious connections.
Mnyika ameeleza wazi kwenye uchaguzi wa December 2019 kwamba toka aingie CHADEMA hapokei posho wala mshahara sababu alikua mbunge.

Otherwise nafasi nyingi CHADEMA hazina malipo maybe posho tu za mafuta malazi n.k so it's not true mtu anayetaka maslahi adumu CHADEMA.

Mtu aliyekua mbunge na kuwekeza kwenye biashara mbalimbali leo ategemee mshahara wa vilaki?

Mnyika is better than that to be honest.... Hata polepole huwezi sema alienda CCM kisa mshahara but hizo other benefits. Tuwe wakweli tu
 
Nataman itokee siku asiwepo hata mwananchi mmoja atakayejitokeza kwenye mikutano ya chadema tenaaaa ili wajue kuwa wananchi wako dissapointed na upinzani kwa kiwango cha hli ya juu

Kwa cdm haiwezekani, labda ccm maana ndio chama kilichozeeka. Wananchi wanajua na wanaona jinsi Magufuli anavyotumia madaraka yake vibaya kukihujumu. Uzuri ni kuwa Magufuli amaeamua kutumia madaraka yake vibaya dhidi ya cdm, huku wananchi wengi wakiwa wameshaamka,ndio maana analazimisha kuiua cdm, lakini watu bado hawaipendi ccm kwa hiari yao zaidi ya kushurutishwa.
 
Wame disappoint nini? Si waliwatimua uanachama tayari so mlitaka wafanyeje zaidi? Toka rufaa ipite hazijapita siku 90 or so, but mpaka sasa wale sio wanachama wa CHADEMA pending appeal!
Ofcz wengi hisia zetu zinawatilia mashaka wotee..na inakatisha sana tamaa
 
Survivaal of the fittest bwana!
Ikiwa wasafiri ni wengi sana na basi ni moja si ajabu ukaona jitu la miraba minne likimwangusha mtu na kuingia ndani ya basi. Likishaingia linaanza kumkea konda " ruhusu gari liende. "
Haijalishi hali hewa, vizee au vitoto ili mradi yeye kapata.
Lakini tujue mbele pia yaweza kuwepo ajali.
Maskahi! Maslahi, mwenye anataka apishwe, asitishwe maana atanguruma kama simba!
Na wananguruma kweli hasa Afrika wenye nguvu.
 
Kuna Kisauti kinanjia Kuhusu Mbowe kubariki Viti Maalumu hapo awali kwa makubaliano ya kuwa siri na kujifanya hana habari.

Hii yaweza kuwa kwa maslahi mapana ya Chama (Ustawi na kutofutika).

Ni mawazo yangu ila tuwaze nje ya Box.

Britannica
Haya ni mawazo finyu ya uchochezi na ndio za kishetani
 
Ila ukifika uchaguzi mnategemea masanduku. Hzi confidence mngekua nazo msingewahi ogopa tume huru wala mikutano ya siasa na maandamano
Bongo hakuna upinzani...

Rejelea uanzishwaji wa siasa za vyama vingi, haikuwa matakwa ya wananchi bali mabeberu...

Hawa wote unaowaona kama wapinzani ni mbuzi wa bwana Kheri na wapo zizini mwa bwana Kheri...

Ninyi ambao mmeamua kushabikia/kupenda/kufurukutwa na siasa za maigizo CCM vs (CUF,CDM, NCCR, ACT) ndio mnaoamini kuna upinzani...

Siasa za Afrika bado ni kivuli kile kile tu cha Mtwa na Mtwana, mwenye kutawala na mtawaliwa kama tu ilivyokuwa nyakati za koo za kichifu/kitemi...
 

Sio kweli, nchi nyingi tu Afrika vyama tofauti vinakamata madaraka. Achana na hizo sweeping statements.
 
Ni kwel kamanda lakin tukubali tu kwamb kwsas pale nyumban kuna level flan ya transparency and ile sense of accountability ime shuka sana kama siyo kuyeyuka kabisa.Matumain yetu tulio wengi (kama sio tunaojitambua) kwa chama yamegubikwa na hali ya kutowaamin wafanya maamuzi.
Inakatisha tamaa sana.
Na ile hali ya wacheche kuendelea kukiamin chama haihalalishi haya basi tu ni vile hakuna pa kuhamishia matumain yao.Heri chongo kuliko kengeza
 
cdm ni wabishi hawataki kuutambua/kuambiwa ukweli. Wanajidanganya chama kinakubalika wakati ukweli ni kwamba mtaani chama hakina mashiko, hakiaminiki na hakina mapya. Wanajiweka "victim" wa awamu ya tano eti failure yao imesababishwa na serikali (typical mawazo ya hovyo ya kimasikini)

Kwenye uchaguzi walipigwa kihalali kwasababu 2015-20 walishindwa kuwa wabunifu na kuja na siasa mpya ambazo zingeshindana positively na siasa mpya za ccm chini jpm, wao walikuwa wanasubiri ccm ifanye jambo waje kupinga, hawakuwa na alternative solution. Huko bungeni kina mbowe, mdee, msigwa na wengineo wakisimama wanasema ' serikali ije na mpango wa ... ili....'
NB zitto alikuwa peke yake lakini alijitahidi sana kuchambua taarifa mbalimbali (japo tango pori nyingi) na kuzipost hata humu jf kuliko hao 70 wa cdm

Wajiulize ni kwanini karibu kila anayehama anasema 'lengo kuu la chama cha siasa ni kushika dola, nimegundua huko hakuna mpango wa kushika dola'

MWISHO: Ukituliza akili utagundua maamuzi mengi ya cdm yanafanywa na watu wenye siasa za harakati na hiki kikundi ndio chenye nguvu na ukipinga wanayoyataka hata kama hayana maslahi utashughulikiwa
 
Wewe ni mstaarabu sana.

Lakini najua ustaarabu huo umekuja tokana na ukomavu ndani ya Jukwaa hili.

Huyo uliyemjibu alikupa kila aina ya fursa kumshindilia kuonyesha upumbavu alionao.

Kwanza huyo anajulikana kuwa zezeta wa CCM kama walivyowengi hapa, halafu anakupakazia kuwa wewe ndio "uondoe uchama kichwani"!
 
Kuna Kisauti kinanjia Kuhusu Mbowe kubariki Viti Maalumu hapo awali kwa makubaliano ya kuwa siri na kujifanya hana habari.
Mkuu 'Britanicca', kama ni kuzeeka, basi unazeeka vibaya.

Kumbe ulikuwa na maana/lengo maalum ya kuanzisha mada hii, lakini kwa maksudi mazima ukaiweka kama fumbo!

Basi ngoja tuvute subira tuone haya yote yanakowapeleka CHADEMA.
Kama wana uwezo wa kupanga na kutekeleza unayoyawaza, basi huko ndani ya CHADEMA kutakuwepo na watu makini sana.

Tuvute subira. Najua kila kitu kitawekwa wazi. Hakuna anayeweza kuficha matokeo ya mikakati ya namna hiyo, kama kweli ipo.
 
Nilikuwa wa kwanza kuwaza hili na niliandika kwa kirefu kwenye facebook
 
Ngoja nichomekee neti mwanzal
Kwani yule wa ubeligini anasemaje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…