Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 63,730
- 111,542
Hilo la kwamba awamu ya tano inaihujumu cdm hilo halina mjadala na ni kupitia madaraka ya rais. Tumeona chaguzi zote toka awamu hii imeingia madarakani, tume ya uchaguzi na vyombo vya dola vikitii amri ya rais bkwa kupitisha wanaccm bila kujali matokeo ya kura. Hayo tumeona kwa macho yetu, na watu kadhaa wameuwawa na wengine kuachwa na vilema.cdm ni wabishi hawataki kuutambua/kuambiwa ukweli. Wanajidanganya chama kinakubalika wakati ukweli ni kwamba mtaani chama hakina mashiko, hakiaminiki na hakina mapya. Wanajiweka "victim" wa awamu ya tano eti failure yao imesababishwa na serikali (typical mawazo ya hovyo ya kimasikini)
Kwenye uchaguzi walipigwa kihalali kwasababu 2015-20 walishindwa kuwa wabunifu na kuja na siasa mpya ambazo zingeshindana positively na siasa mpya za ccm chini jpm, wao walikuwa wanasubiri ccm ifanye jambo waje kupinga, hawakuwa na alternative solution. Huko bungeni kina mbowe, mdee, msigwa na wengineo wakisimama wanasema ' serikali ije na mpango wa ... ili....'
NB zitto alikuwa peke yake lakini alijitahidi sana kuchambua taarifa mbalimbali (japo tango pori nyingi) na kuzipost hata humu jf kuliko hao 70 wa cdm
Wajiulize ni kwanini karibu kila anayehama anasema 'lengo kuu la chama cha siasa ni kushika dola, nimegundua huko hakuna mpango wa kushika dola'
MWISHO: Ukituliza akili utagundua maamuzi mengi ya cdm yanafanywa na watu wenye siasa za harakati na hiki kikundi ndio chenye nguvu na ukipinga wanayoyataka hata kama hayana maslahi utashughulikiwa
Tumeona kundi la watu wasiojulikana wakiua, wakiteka na kushambulia wapinzani, na amri inafahamika inatoka wapi. Kwa mara ya kwanza tuliona kwa JWTZ lililotengwa na siasa kikatiba kwenye kamisheni ya jeshi ikitumika kupokea wanaccm! Wote walionunuliwa toka upinzani kwenye operation kuunga juhudi, walipewa ubunge na udiwani kwa chaguzi zilizojaa ukatili, uhayawani na ukatili wa wazi. Haya yote yamefanyika mbele ya macho ya wananchi. Hali hii imepelekea kuwa na wapiga kura wachache sana, huku tume ya uchaguzi ikipika data za idadi ya wapiga kura. Kwasasa wananchi ndio hawatajitokeza tena kupiga kura maana wamepuuza rasmi box la kura, hakuna uwezekano wa wapiga kura kufika tena 5m. Katika mazingira haya unawezaje kusema wananchi wamepuuza upinzani wakati watu wamepuuza siasa za kishenzi za chama dola?