Kwenye ulimwengu unaojulikana, zipo sayari nyingi zenye kufanana na Dunia na kama zipo za hvi basi uwezekano wa kuwepo na viumbe hai kama wa hapa duniani hasa hasa intelligent life kama sisi binadamu pia ni mkubwa. Lakini mambo siyo marahisi kihivyo kwasababu,
kama intelligent life ipo basi tungeshapata signal kutoka kwao siku nyingi hasa hasa radio signals. Manake chochote kile kilichopo ulimwenguni kinatoa signals. Hii ni sana sana kwa exo planet ambazo hazina umbali mkubwa (maybe hazizidi 100000 ly).
Kwa zilizopo mbali zaidi (kwanzia million ly) signal zitachukuwa muda mrefu zaidi kutufikia kwa teknolojia tulionayo hivi sasa. Hata tunazozipata kwasasa kutoka kwenye hizo sayari za mbali, ni za zamani sana miaka zaidi ya billioni na hizo dunia zitakuwa zimebadilika sana.
Na kwa jinsi tulivyo kwisha weza ku detect hata zamani hzo kulikuwa hamna intelligent life.
Na hata kwa upande wetu hao viumbe wa sayari za mbali (kama wapo) wanapokea signal za dunia ilivokuwa zamani sana kabla hta viumbe hapa duniani havija evolve. Na hii ni kama teknolojia watakayokuwa wanaitumia inafanana na ya kwetu, ikimaanisha kuwa kimaendeleo watakuwa sawa na sisi au tunafanana kwa kiasi.
Hii pia inamaanisha kuwa, kuna uwezekano mkubwa kuwa kama intelligent life ipo basi itakuwa bado ni primitive au itakuwa imelingana na ya sisi binadamu. Kama kuna ambayo imetuzidi sana uwezekano wa wao kuwepo ni mdogo kwa kuwa kama wangekuwepo wangeshatufikia kwa kuwa teknolojia yao itakuwa kubwa sana.
Hata hivyo kuna uwezekano ya kuwa sisi bado teknolojia yetu ipo primitive na uwezo waku detect hzo signals ni mdogo, mpka labda tutakapo kuwa tumefikia class 1 civilization.
Hivyo basi uwezekano wa intelligent life bado upo 50 50. Kwa hapa bindamu tulipofikia hakuna chochote kinacho prove kuwa kuna intelligent life nje ya dunia.