Kuna sheria yoyote ya Tanzania inayozuia kutamka hadharani kuwa unamchukia Rais wa nchi?

Kuna sheria yoyote ya Tanzania inayozuia kutamka hadharani kuwa unamchukia Rais wa nchi?

kama kumpenda si kosa..hata kumchukia pia sio kosa.
kiukweli huyu jamaa damu zetu haziendani tangu alipo kuwa waziri Wa ujenzi.
alipowaambia watu Wa kigamboni wapige mbizi kama hawana 200.
tangu pale mpaka nakufa.
Muendeeni kwa babu yenu kama mnamchukia sasa hapanafanya nn[emoji23][emoji23]
 
Rais pamoja na Wakuu wake wa Mikoa na Wilaya na wana mamlaka ya kisheria na kikatiba kukuweka ndani kwa muda usiozidi saa 48 'wakihisi' uwepo wako uraiani unahatarisha Amani!

ukijiona kisheria si kosa kutamka unamchukia Rais pia jikumbushe kuwa kisheria si kosa Rais kukuweka ndani akihisi kuna ulazima wa kufanya hivyo

Nyerere hakuwa mtu wa mchezomchezo
Sasa Nyerere hapa anahusikaje?.
 
Naomba nijuzwe,

Je, kuna sheria yoyote inayonikataza kutamka hadharani kuwa namchukia rais wa nchi mfano Rais Magufuli?

Maana sitaki nivunje sheria mimi ni mtiifu kwa Katiba.

Naomba majibu wakuu nina haraka kidogo
wengi wanashitakiwa kwa kutamka maneno ambayo yanaweza kusababisha amani kutoweka. mfano, kama kuna watu wanaompenda magufuli (hata kama wewe humpendi), ukatamka vibaya mbele yao mkarushiana ngumi ndicho kinachozuiwa hapa, hivyo kuwa makini na maneno yako yasiwe ya kuudhi watu wanaokuzunguka amani ikatoweka kwa namna yeyote ile. soma kifungu cha 89(1)(a) cap.16
 
Back
Top Bottom