Kuna shida gani kuweka battery kubwa kwenye gari ndogo?

Kuna shida gani kuweka battery kubwa kwenye gari ndogo?

Konte

Member
Joined
Jul 26, 2017
Posts
86
Reaction score
131
Habari zenu wakuu.

Hizi siku mbili battery ya gari (IST) imenisumbua mno, bila shaka muda wake wa matumizi umekwisha.

Kwa sasa sina pesa ya kununua battery nyingine kureplace hii iliyokufa(N40), uhakika wa kununua battery mpya ni baada ya wiki mbili. Kuna gari nyingine hapa (Verossa) ambayo battery yake (N50) ipo vizuri na gari inatumika mara chache sana hasa siku za weekend tu.

Battery za hizo gari mbili zinatofautiana kuanzia ukubwa wa muonekano bila shaka mpaka umeme unaozalishwa. Nimejaribu kuiweka ya Verrosa kwenye IST imekaa vizuri tu.

Nimewaza kuchukua hiyo battery ya Verossa niitumie kwenye IST mpaka pale nitakaponunua battery mpya ya IST.

Naomba kujuzwa kitaalamu kama ni sawa kufanya hivyo pamoja na matokeo hasi yanayoweza kutokea.

Nawasilisha.
 
Ngoja wataalam waje..ila kama imekaa vzuri na haifik N70 nahisi unaweza kutumia ...
 
Kuna vitu huwa wataalamu wanaangalia, ngoja nitaje taje vichache hapa kifundi maiko.

Battery; kuna CCA, Volts na Ampere
Ni matumaini yangu kuwa battery zote zimeandikwa 12Vdc🙂

Sasa hapo kwenye ampere(Pia Ampere Hour), kama ya verossa ni N70 na IST ni N50, maana yake ni kuwa, alternator ya IST itatumia muda mrefu zaidi kuijaza 70N na hivyo ni kama unaitumikisha zaidi alternator ya IST.

Kama safari ni fupi fupi na umefunga N70 kwenye IST, uwezekano wa kuchajiwa vizuri ni mdogo.

Hiyo CCA, ni uwezo wa battery kuwasha injini katika hali ya ubaridi au jotoridi sawa na mazingira ya nje, mathalani pale unapotaka kuwasha gari asubuhi baada ya kukaa usiku wote bila kutembea wala kuwashwa. Hivyo unaweza kupima volts ukaona inasoma 13Vdc lakini ikashindwa kuzungusha injini.

Kwa dharula, weka tu, si utabadilisha baada ya wiki 2! Ila usije ukanogewa.
 
Nadhani ni vyema uende garage ukaulizie kwa fundi umeme wa magari. Hizo betri kuwekwa namba zake zina maana fulani kwenye gari.
 
Ndio maana unaambiwa N.40 N70 na N 100 hapo unaumiza gari lako maana moto unalisha ni mkubwa kuliko size yake.
Naomba nikuweke sawa bosi, hata ukiweka N200 kwenye IST, kama ni 12Vdc, basi ni hiyo hiyo. Hakuna moto mwingi utakaoenda kwenye gari yako, ila kama utaziunga betri mbili kwa mtindo utakaokupa 24Vdc, hata kama ni N40, zitauwa vifaa vyako.

Kila kifaa kinapakuwa kwa kadiri ya kinavyohitaji na kilivyopangiwa, kikianza kuzidisha, fuse inaungua na kumkatia huo mgawo.

Kwenye umeme wa majumbani unaweza sema hivyo kwa hali fulani.
 
Kwa nini wakakuwekea N40 wasikuwekee N. 100
 
Nitajie sehemu (accessories/parts) ambazo zinaweza kuumia endapo nitatumia N50 badala ya N40.
Wire kutoka kwenye batery kwenda kwenye starter kwanza kuzidiwa wattz rotation ya engne kuongezeka mfumo wa umeme kuongezeka baadhi ya vifaa kwenye contol box kuumia maana moto umevuka watts zinazotakiwa na fuse kuzidiwa pamoja taa zitawaka ila hazitadumu kama inavyotakiwa
 
Naomba nikuweke sawa bosi, hata ukiweka N200 kwenye IST, kama ni 12Vdc, basi ni hiyo hiyo. Hakuna moto mwingi utakaoenda kwenye gari yako, ila kama utaziunga betri mbili kwa mtindo utakaokupa 24Vdc, hata kama ni N40, zitauwa vifaa vyako.

Kila kifaa kinapakuwa kwa kadiri ya kinavyohitaji na kilivyopangiwa, kikianza kuzidisha, fuse inaungua na kumkatia huo mgawo.

Kwenye umeme wa majumbani unaweza sema hivyo kwa hali fulani.
Ndio maana nikamuambia gari litaumia sio kumaanisha kwenye engine ni baadhi ya vifaa ya mfumo wa wire/umeme kama fuse taa au sterter winginv yake maana moto unaoenda ni mkubwa watts kuliko kiwango kilichowekwa
 
Back
Top Bottom