Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Atakata fuse kibao tena baadhi ya dioty au resister na AC kwenye control box kuungua kabisa maana anazidisha wattsTia tu man. Haina noma.
Battery ya babywoka yangu inatabia ya kuweka unga unga mweupe kwenye zile terminals zake. Sijui shida nini.
Hapana mkuu, toka hapo kwenye moto mwingi kwanza ukitaka kuuelewa huo umeme, uking'ang'ania hapo, wengi watakuwa wanakushangaa.Ndio maana nikamuambia gari litaumia sio kumaanisha kwenye engine ni baadhi ya vifaa ya mfumo wa wire/umeme kama fuse taa au sterter winginv yake maana moto unaoenda ni mkubwa watts kuliko kiwango kilichowekwa
Rated output ya alternator wakati huo inasoma ngapi? Tolerance yake ni ipi? Deep cylce?Ishu tu ni kwamba gari ambayo ilikuwa N40 ukaweka N50 battery itakuwa inachelewa kujaa. Na siyo kwamba utaumiza Alternator sababu hakuna muda alternator haifanyi kazi wakati engine inazunguka.
Fungua clamp kwenye terminal husika, safisha hiyo terminal na clamp, funga vizuri clamp kwenye terminal, PAKA GRISI au VASELINE kwenye clamp na terminal.Battery ya babywoka yangu inatabia ya kuweka unga unga mweupe kwenye zile terminals zake. Sijui shida nini.
Rated output ya alternator wakati huo inasoma ngapi? Tolerance yake ni ipi? Deep cylce?
Nikiunga betri 2, ama mfuatano au sambamba, betri moja ikawa mbovu na moja nzima, nini kinatokea hapo?
Betri kubwa ni load kwa alternator ndogo.
Unapokuwa unachaji betri ambayo iko exhausted kwa zaidi ya 40%, charging current inakuwa kubwa, tuseme 40A. Kadiri muda unavyokwenda, betri inakunywa chaji na kuanza kujaa. Inapoelekea kujaa, na charging current inapungua mpaka kufika 0A sio? Kisha battery charger inaanza kufanya tricle charging endapo battery iko connected na load.Mzee kinachomatter ni Cold Cranking Amps
Kama minimum CCA zimekuwa met. Then put any battery. Hakuna shida utapata. Changamoto moja ni kwamba bigger battery haitotosha kwenye space ya kuweka battery hapo kwenye gari yako.
Wewe unaonekana mgeni na mitambo hii. Umeambiwa tatizo pekee litakalokuwepo ni alternator kutochaji betri kwa wakati wa kawaida. Lakini pia Kuna advantage kama gari likifa charging system kwa maana unaweza kuendesha kwa betri na ukafika kwa fundi bila kuzimikiwa. Faida nyingine kwa kuweka betri kubwa ni kuwa unaweza kuongeza vifaa vya umeme kwenye gari kama heavy music system au spot lights. Hakuna kifaa kitakachoharibika.Ndio maana nikamuambia gari litaumia sio kumaanisha kwenye engine ni baadhi ya vifaa ya mfumo wa wire/umeme kama fuse taa au sterter winginv yake maana moto unaoenda ni mkubwa watts kuliko kiwango kilichowekwa
Umenena sawasawa na mawazo yangu.Naomba nikuweke sawa bosi, hata ukiweka N200 kwenye IST, kama ni 12Vdc, basi ni hiyo hiyo. Hakuna moto mwingi utakaoenda kwenye gari yako, ila kama utaziunga betri mbili kwa mtindo utakaokupa 24Vdc, hata kama ni N40, zitauwa vifaa vyako.
Kila kifaa kinapakuwa kwa kadiri ya kinavyohitaji na kilivyopangiwa, kikianza kuzidisha, fuse inaungua na kumkatia huo mgawo.
Kwenye umeme wa majumbani unaweza sema hivyo kwa hali fulani.
Unapokuwa unachaji betri ambayo iko exhausted kwa zaidi ya 40%, charging current inakuwa kubwa, tuseme 40A. Kadiri muda unavyokwenda, betri inakunywa chaji na kuanza kujaa. Inapoelekea kujaa, na charging current inapungua mpaka kufika 0A sio? Kisha battery charger inaanza kufanya tricle charging endapo battery iko connected na load.
Sasa kwa kesi ya gari, wakati gari inatembea, vifaa kama sio vyote basi vingi vinapaswa kulishwa umeme na alternator sio? Wakati huo huo alternator inapaswa kuchaji betri na kuhakikisha betri iko full.
Sasa kama vifaa vyote vya kwenye gari, mathalani ni usiku, vimewashwa na vinachukua 40A, battery kwakuwa ni kubwa au bovu, linataka 40A, uwezo wa alternator ni 60A output, kwa safari ya masaa 12, alternator inatoa 60A yote huku deep cycle yake ikisema pengine ni 0.9 max, hakuna lolote litakalotokea kwenye alternator yako?
Sijawahi kuchunguza hili. Na una-refer gari ipi? IST? Naweza kutafuta clamp meter kucheki hili siku moja.Tusifanye assumptions.
Labda nikuulize wewe swali.
Kwenye full electrical load amps ngapi zinaenda kwenye accessories na ngapi zinaingia kwenye battery?
Sijawahi kuchunguza hili. Na una-refer gari ipi? IST? Naweza kutafuta clamp meter kucheki hili siku moja.
Naanza kukuelewa mkuu, sikuwa na lengo hilo, unisamehe sana!
Hapo sawa, maana nilihofia kuwa naweza kuwa naku-challenge nikaharibu biasharaOkay haina shida mkuu.
Kwa gari yoyote lazima huwa kunakuwa na ratio ya current inayokuja kwenye Acc na inayoenda kwenye battery.
Anyway ngoja kukuche me mwenyewe kuna gari kadhaa nitaangalia alternator zake then tunaweza kuwa na mjadala wenye tija.
Hapo sawa, maana nilihofia kuwa naweza kuwa naku-challenge nikaharibu biashara
Wa stendi, hapo ni kuangali tu uwqezo wa charging alternator..!! Kama output current ya alternator inaweza kuiendesha hiyo battery wala haina shidaNdio maana unaambiwa N.40 N70 na N 100 hapo unaumiza gari lako maana moto unalisha ni mkubwa kuliko size yake.
Yaan wewe ndio kabisa hata maana ya N huijui mkuu, hiyo N siyo size kama unavyo amini N ni Newton ambapo kwa maana nyingine tunaweza sema ni ujazo wa current au kiswahili labda tuseme uzito wa umeme,Umenena sawasawa na mawazo yangu.
Mimi ninachoelewa N40, N50 au N70 ni size ya battery tu, kikubwa ni kutambua gari yako inatumia v12 au 24.
Kitako cha battery kwenye gari lako ndiyo kitaamua ukaaji wa size ya battery iwe ni N40 au N50.
Kweli kabisa inawezekana mimi sijui kitu, lakini naelewa kitu kimoja. Kuna universal language ya size kwenye hii dunia.Yaan wewe ndio kabisa hata maana ya N huijui mkuu, hiyo N siyo size kama unavyo amini N ni Newton ambapo kwa maana nyingine tunaweza sema ni ujazo wa current au kiswahili labda tuseme uzito wa umeme,
Yaan kadri N namba inavyo kuwa kubwa ndivyo battery inaweza kuhimili kuendesha vifaa vingine kwa mda mrefu mfano kama battery ya12VDC N40 inaweza kuwasha mziki kwa volume 70% bila kuzima kwa masaa 6 basi battery ya12VDC N50 itawasha mziki huo huo na kwa volume hiyo hiyo ya 70% ila kwa masaa 8 nadhani hapo utakuwa umeelewa maana ya N.
HAPANA mkuu N ya kwenye battery za gari,solar and co. Haimaanishi product size in terms of dimension ila ina maanisha size in terms of voltage currents. Elewa hivyo na usiwe mbishi kwa hilo.Kweli kabisa inawezekana mimi sijui kitu, lakini naelewa kitu kimoja. Kuna universal language ya size kwenye hii dunia.
Mfano; Size ya battery za remote control zinakuwa determined na letters kuna size za A, AA au AAA. Kwa maana hiyo, kama remote yako ya TV imeandikwa battery size ni AAA, maana yake mimi LAYMAN sio lazima niende na remote dukani ili nitest kama battery zitaenea, bali nahitaji kumwambia mwenye duka anipe battery size ya AAA. Nikichukua size tofauti kwa mfano size AA maana yake hiyo battery haitaenea kwenye remote yangu.
Hii ni universal language ya mtumiaji na ni rahisi kwa watu ambao hawajui kama mimi na kwa maana hiyo sihitaji kupiga hayo mahesabu ya electronics.
Size ya battery ya gari inakuwa determined na hizo N40, N50 na kadhalika. Hii lugha inamsaidia mlaji ambaye hajui kitu kama mimi ili anunue battery sahihi kutokana na specification ya gari. Na mara nyingi, kitako cha battery huwa kinaamua size ipi ununue kwani size ya battery N100 haiwezi ikakaa kwenye kitako cha magari madogo kwa sababu hiyo sio size yake.
Pamoja na elimu yenu ya electronics, viwanda vilirahisisha mlaji ambaye hana elimu anunue size ya ukubwa unaotakiwa badala ya kupiga hesabu zenu za amp na volts.
Kwa maana hiyo, wewe piga hesabu zoote za electronics lakini mimi kama mlaji layman nitaenda kununua battery kutokana na size ya kitako cha gari langu.