Kuna shida Gani kwenye Operation za Uzazi? Hivi vifo ni mimi tu naona?

Kuna shida Gani kwenye Operation za Uzazi? Hivi vifo ni mimi tu naona?

alitaka kuwashtaki naona hosp waliongea nae akaacha lakini ni kweli wa tanzania tunakosa hela kizembe hapo angekomaa nao angepata hela ndefu tatizo ukifika kwa mwanasheria anakwambia kufile kesi ni milioni tatu sasa ni watu wangapi wana hiyo pesa.
Zipo taasisi kibao zinatoa msaada wa kisheria.. hapo akifanya sii kwaajili ya marehemu pekee.. pia itawasaidia wengine watakao fuata.

Pia kuna baraza la madaktari kuna platform ya kushughulikia haya mambo

POLE SANA MKUU
 
Likely kuna tatizo mahali.

Kisayansi kujifungua kwa upasuaji mkubwa alias C-Section inaelezwa kua ndio njia salama zaidi na ya uhakika...taking aside few complications.

Sasa ikitokea inakua tena sio salama vifo vinajitokeza lazima wataalamu watuambie shida iko wapi?

Ni vifaa, vifaa tiba, utaalamu duni, ucheleweshaji au nini hasa...haya yote ni ya kitaalamu na hayahitaji watabiri wa kuupiga mwingi.
Acha uongo....C section comes with greater risks kuliko vaginal delivery.
Standard procedure inakuhitaji uwe na sababu ya msingi ya kufanya C section sababu normal delivery ni priority.
 
wee huko kidogo mama yangu mdogo alale yooo, eti professional doctor 😆 akasahau kushona ngozi ya ndani sijui ila nakumbuka aliteseka sana almost a year.
Sijui kwa sasa...ila kuliko kwenda general au udom I prefer there...
Kwani kusahau kitu kunamuondelea mtu kuwa professional? Sema ni uzembe,maybe ulevi n.k....
 
Inaumiza sana ndugu zangu.
Watu wa 3 ninaowafahamu, wengine wa 3 ni watu wa karibu wa marafiki zangu..
Katika miezi 4 wamepoteza maisha Wote kwa operation ya uzazi, achilia mbali wale ninaosikia mtu pembeni akiongea.

Inauma Sana ndugu zangu,
Mnampeleka mpendwa wenu hospital akiwa mzimaa mpate malaika, mnaambulia Miili miwili isiyotikisikaa... Mbaya zaidi uone kuna hali ya uzembe ilifanyika.
Isikie tuu hii kwa mtu ndugu yangu..

Hiki ni nini? Au ni coincidence tuu kwa bahati mbaya imetokea zaidi kwa watu ninaowafahamu?
Hivi hua hospital wana keep Data? If yes Are they real? Data zinasemaje? Zinafanyiwa kazi? Maana sidhani kama ni kawaida..

Kwa Moyo wa dhati NIIOMBE Serikali kupitia wizara ya Afya Fuatilieni hili Zaidi, kuna uzembe,
Mmoja kati ya hao Pamba ilisahaulika Tumboni Dodoma hapo, mwingine naye mistake katika kutenganisha Kitovu, Mwingine naye kuna sehemu ilikawa vibaya...
Haya ni makosa ya kibinadamu..
Hatuna chance ya makosa ya kibinadamu katika Afya ya mtu jamani..

Wahusika Niwaombe ndugu zetu, nyie ni professional, mmekula viapo, Mnalipwa, Jitoeni katika kazi zenu, Fanya Ukijua uhai wa viumbe hao upo mikononi mwako,
Kueni makini na Afya za Mama zetu, Dada zetu na wote kwa ujumla, mmeaminiwa sanaa..
Itokee kwa mipango ya Mungu ila sio kwa uzembe..

Serikali nawaomba Sana viongozi wangu, Chukueni hili katika positive way ya kuokoa mama na mtoto..
Siandiki hapa kama Niliyepoteza Mke au Ndugu, naandika kama binadamu niliyeumia SANAA kuona ndugu zetu hawa Wanatutoka katika picha kama hizo...

Nawaomba Tena Chukueni hili katiaka Positive way,
Mpo hapo kuokoa jamii kubwa nyuma yenu, Jivunie Kuo mmoja wa waliokoa mamia ya mama zetu na taifa la kesho, Siku Moja utalipwa, this is real sio siasa.
Ni suala la kitaalamu, litatuliwe kitaalamu.

Rai kwa Mama na dada zangu, Mnaopokua wajawazito, Punguzeni Utandawazi, epukeni Uzazi wa operation usio wa lazima kwa kisingizio hutaki uchungu, Jipe mazoezi.

Poleni Sana Wote mlitokwa na Wapendwa Wenu katika picha kama hii..

AMEN.
INAWEZEKANA MADAKTARI WANAFUNZI WANAACHIWA KAZI ZOTE
 
Zipo taasisi kibao zinatoa msaada wa kisheria.. hapo akifanya sii kwaajili ya marehemu pekee.. pia itawasaidia wengine watakao fuata.

Pia kuna baraza la madaktari kuna platform ya kushughulikia haya mambo

POLE SANA MKUU
Naona alianza kumalizana na hosp tuu maana alikuwa na hali mbaya alichokuwa anataka ni kupona tuu
 
Sijui kwa sasa...ila kuliko kwenda general au udom I prefer there...
Kwani kusahau kitu kunamuondelea mtu kuwa professional? Sema ni uzembe,maybe ulevi n.k....
ilikuwa 2016 anaishi dom lakini watoto wake hakuwahi jifungulia dom kwasababu kulikuwa hamna hosp inayoaminika kwenye uzazi ndo ikaja hiyo hosp akasema ngoja ajifungulie hapo anasikia wapo vizuri ndo ikawa hivyo hawakumshona vizuri
 
Poleni poleni mno kwa wote mliokutwa na uzembe huu,na tatizo nothing u can do, yaani Doctors wengi nchi yetu they got away with murder, wakuu tutafuteni hela,pls usicheze kabisa na afya yako na wapendwa wako, peleka Nairobi au Millpark, royal families huwezi kuona ndugu zao wanatibiwa pale magomeni hospital
Well Said !!!
 
Kada imekua Cha wote, Ili mradi wazazi wako Wana Pesa unakua Daktari.


Mitihani yao ya Kidato Cha sita Sasa ,unashika mtihan unajiuliza, Hii ndo Paper 1 na 2 ya Physics ?. wanatungiwa mitihan myepesi sana.

Haya, Private schools nazo zinashindana kufaulisha basi Wizi juu ya wizii ,maswali yanasoviwa chap, wanapewa wanafunzi chap ,wanajibu chapchap wanapiga One.


Hujatulia kidogo... Wazuri wa Elimu anataka kumfurahisha Rais, "Mama Sa100 kafanya watoto wamefaulu sana ". .... Siasaaa siasaa hizi .


Angalieni matokeo ya Kidato Cha sita ya Mwaka 2021 baada ya Rais Sa100 kushuka kijiti..... Ilikua ni miezi miwili ya yeye kua MADARAKANI, ila Sasa , Matokeo yakapikwa pikwaa, kuonyesha kua MIEZI MICHACHE TUU TAYARI KABADILISHA ELIMU, SASA WANAFAULU
We jamaa najua ni Dr na huwa unafanya Cesarean Operation what mistake happened wakati wa hilo zoezi mpaka kupelekea kifo Cha either mama au mtoto?


Isije ikawa tunawalamu bure madatari.
 
Back
Top Bottom