Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 11,550
- 40,697
Hii kitu ni nyeti sana, bahati mbaya sana wengi tunaandika tu hapa, lakini hatujui kitu, tunasukumwa na hisia tu, ukweli hatuufahamu.
Imebidi niingie chimbo kuuliza wataalamu wa afya kuhusiana na hii, na nilichoelezwa kimeniacha mdomo wazi, nimeshangaa mnoo.
Labda niweke facts chache katika hili baada ya kuhoji sana wataalamu kadhaa.
1. Operation yoyote ile ni risk ya mgonjwa kupoteza maisha, na kadri operation itahusisha dawa za nusu kaputi au kupoteza damu nyingu basi risk huwa zaidi ya maradufu. Na operation ya kujifungua ni very risk kwa sababu uhusisha hayo. Ni kufa au kupona.
2. Matokeo ya operation yoyote ile hutegemea maandalizi, vifaa, wataalamu, madawa na uangalizi (monitoring). Kupelea kwa chochote kile katika hivyo kunaweza kupelekea lolote lile kutokea.
3. Kwa mujibu ya wataalamu wa kidunia (WHO?) ili ufanisi wa operation ya kujifungua uwe mzuri, inabidi at least kuwe na timu ya wataalamu wasiopungua 12 standby! Ambao ni:
(i)Daktari mkunga (Obstetrician)
(ii)Daktari msaidizi (medical Doctor)
(iii)Daktari wa dawa za usingizi.(Anasthesiology)
(iv)Daktari msaidizi wa dawa za usingizi. (Anasthestist)
(v)Muuguzi mtaalamu wa operation (theatre nurse)
(vi) Muuguzi mtaalamu msaidizi
(vii) Muuguzi mkunga (Nurse widwifery)
(viii) Daktari wa vichanga (Neonatologist)
(ix)Mtaalamu wa vifaa (Medical equipment technician)
(x) Mfamasia
(xi)Mtaalamu wa maabara.
(xii)Daktari muokozi (Resuscitation Doctor).
4. Kifalsafa katika fani ya utabibu, kila Daktari ni mwanafunzi, tofauti ni ngazi za uanafunzi. Kadri Daktari anavyofanya kazi ya kutibu kwa mtizamo wa kiuanafunzi ndivyo anavyoweza kutengeneza matokeo bora na chanya yakuponyesha and vice versa is true.
5. Kwa kadri operation za kujifungua watoto zinapokuwa nyingi pasipo sababu ya msingi ya ulazima wa moja kwa moja (absolute indication) ndivyo na idadi ya vifo vya wakina mama wanaojifungua kwa operation itazidi kuongezeka.
Mwisho ni scenario ambayo ilinishtua zaidi. Kuna kituo kimoja duni cha afya cha serikali, kipo maeneo ya vijijini, ambacho hakikuwahi kuwa na wataalamu mbali mbali muhimu, hakina Daktari bingwa wa wanawake, wala daktari bingwa wa dawa za usingizi na wataalamu wengine mahususi, wala vifaa vya kisasa sana vya upasuaji, katika mazingira hayo hayo kikafanikiwa bure kuwasaidia wakina mama kujifungua kwa njia ya operation (wastani wa operation moja kwa siku) kwa kipindi cha miaka mitano mfululizo pasipo kuwepo rekodi ya kifo hata kimoja cha mama.