Kuna shida gani Tanzania ikitangaza rasmi kuisaidia Congo kupambana na M23? Tuna Viongozi wa namna gani?

Hakuna kete yoyote, huo mgogoro hauna athari zozote za maana kwa mataifa makubwa yenye nguvu za kuumaliza kwa hiyo hawaupi umuhimu au kipaumbele chochote.
 
Hakuna kitu kama icho! jk alifanyaje 2012?
 
Mna mu underrate yule mtu mrefu ila tambueni kua amekulia polini anajua intelgence ya vita, mnajua kwa nn kapeleka wanajeshi wake kule Mozambique ile ni long term plan sku tukisema vyoko atuzunguke, kaiteka goma ndani ya sku moja tu duh
 
NI kwamba, kwa sababu Rwanda wanawasaidia M23, tukitangaza kuwasaidia DRC maana yake tumetangaza vita na Rwanda.
Ndiyo Kagame aambiwe kabisa aache kuisaidia M23. Na asiposikia wakate mbupu zake. Kwa nini kamtu kamoja kaendelee kusumbua jirani yake kwa muda mrefu namna hii na majirani wengine wapo hawachukui hatua kali dhidi ya jirani mkorofi? Tatizo lipo wapi?
 
M23 Wana drone wewe una jeshi la mkoloni kila kitu manual... Unapasua tofali kwa kichwa, una mavifaru outdated , ndege za vita outdated.....tusi wa underrate Rwanda inaweza kujikuta TUNAOMBA hifadhi sudani kusini,Uganda, Zambia, Malawi na ughaibuni..
Kwa hiyo una maanisha Jeshi letu halina drone?

Acha kutudharau dogo.
 
Ndiyo Kagame aambiwe kabisa aache kuisaidia M23. Na asiposikia wakate mbupu zake. Kwa nini kamtu kamoja kaendelee kusumbua jirani yake kwa muda mrefu namna hii na majirani wengine wapo hawachukui hatua kali dhidi ya jirani mkorofi? Tatizo lipo wapi?
Akikuuliza mambo ya DRC na Rwanda yanakuhusu nini utamjibuje??
 
M23 kama wameteka Goma watangaze Nchi.

Tuwasaidiw DRC Ili tupate nini? Miaka yote tuliowasaidia wametupa nini?
 
Aliyekwambia kuna mambo ya kimya kimya vitani ni nani? Ukiwa ni mtanzania ukaenda kupigana upande mwingine utajulikana tu ni mtanzania.

Watu wanaposema vita ndo iwe suluhu ya mwisho hawajakosea, vita ni kitu kingine kabisa.
 
Ni kweli kabisa
Hii ni kwa wanaoelewa vita kwa manufaa ya nchi
Hata hapo kuna wanaofaidika na wanapigana kwa sababu ya Madini na misitu
Huwezi kupeleka majeshi kama huna maslahi nayo
Au kiswahili chepesi kwenda kuiba rasilimali za wengine

Nakumbuka vita vya Iraq wazungu walivyofaidika
Yaani mpaka Dick Cheney alichukua tenda ya ku supply jeshi la Marekani huko mashariki ya kati na alipiga hela nyingi sana
Imagine VP wa US anapiga dili mpaka toilet paper
 
Kwa hiyo una maanisha Jeshi letu halina drone?

Acha kutudharau dogo.
Mkuu,
Tujibu hoja mambo ya kuitana dogo usipendelee.
Maana tumekuwepo humu kabla yako.
Kuhusu vita usi wa underrate m23 maana mpaka Sasa umeona kinacho endelea mashariki ya Kati.. Israel mpaka Sasa licha ya kua na kila kitu kashindwa kumaliza vita yake the same kwa Russia vs Ukraine

So Sisi ni maskini ndio maana huwa tunapima unga kilo kilo kwa mangi na kila siku tunaacha Kodi ya meza asubuh Ndio tukachokoze vita ya watu WAKATI sisi wenyewe tupo vitani
 
Tanzania ni mwanachama wa SADC hivyo ilishatangazwa tayari kuwa SADC inamsaidia mwanachama wake DRC kupambana na M23. Mkuu wewe unataka lazima TZ nayo itangaze? Au tatizo ni uelewa wa mambo unakupiga chenga?
 
Hizi mada nimekuwa nikifutilia sana hapa jf cha kusitikisha ni baadhi ya comment za wadau ni wazi kuwa hatuna matumaini ya kutoka hapa tulipo na kusonga mbele yaani mtu anasema Tz Ni nchi maskini tena anarudia rudia muulize umaskini wa tz uwapi?

Atakujibu wanafunzi wanakaa chini
Vyoo hamna yaani mifano ya kijinga kijinga tu.

Huyo huyo mdau kasahau nchi yake inanunua v8 ovyo ovyo tu CAG kila mwaka anataja ufisadi wa mabilioni kila idara
Tunasahau jpm hapa tu alituambia nchi yetu ni tajiri na kweli tuliona maendeleo ya kasi sana kwa kipindi kifupi tu leo hii tuna sgr nk!

Mleta uzi maoni yako ni kama yangu mimi niliwaza toka zamani sana ila nikawa nawaza labda kutakuwa vikawazo flani Kimataifa maana naona jeshi letu lipo imara sana kongo wapo tiyari hata kutumegea kipande cha ardhi yao tukafaidika na madini na mistu yao.

Faida ni nyingi sana Pk sio wa kumuogopa kwa upande wa jsehi letu japo ana mapandikizi mengi sana kwenye nchi yetu mbali na haya kaweka kambi yake kule kusini kwa mgongo wa kuisadia nchi flani lakini Target yake ni Tz but na uhakika uwezo huo hana. Hata kama atategemea msaada nje na sisi bado nchi ina mali hatuwezi koswa misaada.

Hii kuogopa ogopa eti tukiingia huko nikutangaza vita na PK kwani yeye nani? yaani afanye anavyotaka na aachwe tu? Ipo siku akimalizana na kongo ataona kupima nguvu na Tz na muda huo atakuwa anajimilikisha nchi ya kongo na mali zake kumpiga itakuwa kazi kubwa mno ......
 
Umaskini wetu ni upi mkuu? Au una maanisha umaskini wa akili au umasikini wa viogozi wenye huruma na mali za uma?
 
Aliyekwambia kuna mambo ya kimya kimya vitani ni nani? Ukiwa ni mtanzania ukaenda kupigana upande mwingine utajulikana tu ni mtanzania.

Watu wanaposema vita ndo iwe suluhu ya mwisho hawajakosea, vita ni kitu kingine kabisa.
Kwa hiyo Tanzania imetoa tangazo rasmi inaenda kusaidia DRC dhidi ya M23?
 
So kwa hoja yako una maanisha Rwanda kashindikana? Na anaweza fanya lolote lile bila kufanywa chochote kile?
Ana wakubwa nyuma yake wenye nguvu duniani.
Ukiona mbuzi juu ya mti ujue kapandishwa na mtu.
Ukiona mtoto mdogo jeuri anakupiga ngumi kibabe ujue Kuna mtu anaye mpa jeuri, mguse upigike.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…