ANAANDIKA Boniface Jacob almaarufu kama Boniyai mwenyekiti CHADEMA Kanda ya Pwani.
Tafakari na Ushuhuda ya Eid Al Uddha.!
Mara zote wakati wa kufunga mkutano unapokaribia huwa tunamaliza kwa kuweka chagizo la fedha maarufu kama Tone Tone.
Makamu Mwenyekiti @HecheJohn
akiwa jukwaani na kapu la chagizo mimi huwa na chukua kikapu kimoja napita nyuma ya mkutano kuchangisha wale wanao ona aibu au kuogopa kwenda mbele ya jukwaa kupeleka michango yao.
Jana tulipokuwa Kilombero kata ya Ruaha nilishuhudia mambo ya ajabu kidogo.
Wakati napita nyuma ya mkutano kuchangisha nilikuwa naitwa na watu kadhaa waliokuwa wamenyanyua fedha zao ishara ya kwamba nipite kuzichukua.
Nikiwa mbali zaidi nilitwa na wakina dada kama wanne waliokuwa nje ya flemu kama saluni.
Nilifika nikanyoosha kikapu ili walioniita wachange kama wenzao,walichanga wawili tshs 2000 kila mmoja na wakaniambia aliyetuambia tukuite yupo ndani.
Alikuwa ni mbaba nadhifu mwenye suti maridadi,kwa sauti ya chini akaniambia "Mimi ni Mtumishi wa Umma ,nisamehe nimekuita huku ili mashushu wasije kuniona nikichangia CHADEMA,tuliitwa hapa kuja kuzuia mkutano wenu,ila nimependa ujumbe wenu wa No Reforms No Election kisha akaingia kwenye koti lake la suti akachanga Tsh 100,000/=
Wakati ninafuraha kikapu changu kinakaribia kujaa
Ghafla kwa mbali aliniita bibi mmoja ambaye alikuwa amekaa chini kwa kunyoosha katika nyasi,nguo zake Kukuu na alikuwa amejitenga sehemu ya peke yake.
Wakati huo tayari ni saa 8 na nusu mchana na tayari msafara ilikuwa umeanza Kutoka uwanjani kuwah mkutano wa saa 10 jioni Morogoro mjini umbali wa kilometa 218.
Roho ilisita sababu ya haraka lakini kwakuwa zoezi la uchangishaji ni la hamasa nikajisemea hata aikichanga tshs 200 inatosha kuwa motisha kwa wengine.
Nikiwa nimemsalimia na kusimama mbele yake huku kapu nimepeleka mbele kusubiri mchango wake.
Bibi alikuwa anafungua pindo la kanga yake kwa tabu sana na muda mrefu huku akirudia neno "msichoke msichoke, mschoke"
Baada ya dakika kadhaa bibi alitoa fundo lake la pesa,ilikuwa ni Tsh elfu 25,akatoa mchango (tonetone) elfu ishirini kisha akasema anabakia na tshs efu tano kwa ajili ya bodaboda ya Kurudi kijijini kwake.
Nilishangaa sanaaaa, bibi kutaka kazi ya kudai mabadiliko ya kisheria na kimfumo ifanyike kwa gharama ya mchango wake.
Hadi leo nimekaa na kutafakari,kama bibi anaimani kubwa kiasi hiki vijana watakuwa na kisingizo gani..?
No reform No election.