Kuna shida yoyote kama efd machine haitumiki kila siku ikiwa TRA wamenikadilia kodi ya kulipa kwa mwaka?

Nyarupala

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2024
Posts
494
Reaction score
856
Ni January inakaribia ndyo nakumbuka kuna kitu kinaitwa efd machine na kutoa risiti kwakweli kwangu ni ngumu,syo makusudi bali ni kusahau tu.

Sikumbuki huu mwaka unaenda kuisha nadhani nimeitumia kama miezi minne tu zikiisha rola ndo kabisa nasahau kila kitu.

Lakini TRA wameniwekea makadilio ya kodi ambayo inalipwa kila baada ya miezi mitatu,yaani mara nne kwa mwaka. Je,kuna shida yoyote hapo? Kwasabab kama kodi nalipa kila kitu ila shida ndyo machine yao kuitumia mtihani.
 
Aisee nchi hii
Uzuri mashine inasoma.jumla ya mauzo kwa mwaka
Unatakiwa utumie mashine wakikukamata utakoma tena usije ukaenda kusema huuutopolo
Sema Tu biashara mbaya.kuna.siku huuzi kabisa
Japo nimeelewa nisamehe wewe ni kiazi mbatata
 
Biashara yako ina fall kwenye category gani, sole proprietorship, (mtu mmoja), partnership (mnashea) ama ni kampuni?

Kwanini ulisajili mfumo wa EFD na hutoi risiti ? Hilo ni kosa kubwa sana na wakikubaini fines & penalty zitakuhusu pasipo kuonewa huruma

Ulifanya makadirio ya Kodi ! Je unaandaa vitabu vya hesabu , nikimaanisha financial statements?

Huoni kutakuwa na tofaut kubwa ya sales za kwenye zreport na ile unayoandika kwenye daftari ama Tally/quick books?

vipi kuhusu manunuzi?

Aseeh jitahidi ku comply na TRA guidelines ili kuepuka further notice of discussion.....

Kila la khery mkuu
 
Anazingua ni kama wale wanaofungua kampuni zinakamilika wanazitelekrza huko

Ndo wanakutana na fines & penalties za SDL, PAYE, hawajafanya estimation, mara WHT, hujatuma financial statements! Kazi kweli kweli
 
Mwisho wa siku waanze kupekua na visivyotakiwa kuonekana tena. Nikiepuka huu msala sitarudia tena.
 
Biashara yako ina fall kwenye category gani, sole proprietorship, (mtu mmoja), partnership (mnashea) ama ni kampuni?

Kwanini ulisajili mfumo wa EFD na hutoi risiti ? Hilo ni kosa kubwa sana na wakikubaini fines & penalty zitakuhusu pasipo kuonewa huruma

Ulifanya makadirio ya Kodi ! Je unaandaa vitabu vya hesabu , nikimaanisha financial statements?

Huoni kutakuwa na tofaut kubwa ya sales za kwenye zreport na ile unayoandika kwenye daftari ama Tally/quick books?

vipi kuhusu manunuzi?

Aseeh jitahidi ku comply na TRA guidelines ili kuepuka further notice of discussion.....

Kila la khery mkuu
Ni mtu mmoja. Nikienda sijui naeleza nini...tena nisimkute yule jamaa tena this time,anaongea sana na hasikilizi kabisa
 
Aisee nchi hii
Uzuri mashine inasoma.jumla ya mauzo kwa mwaka
Unatakiwa utumie mashine wakikukamata utakoma tena usije ukaenda kusema huuutopolo
Sema Tu biashara mbaya.kuna.siku huuzi kabisa
Japo nimeelewa nisamehe wewe ni kiazi mbatata
Asante kwa ushauri japo na matusi juu
 
Mwisho wa siku waanze kupekua na visivyotakiwa kuonekana tena. Nikiepuka huu msala sitarudia tena.
Ok ni sole, una biashara kubwa nadhani mpaka una EFD

Je wakitaka waone mauzo unayo rekodi manual utawapa nini ? Najua unayo sasa hapo tyr Kuna utofauti wa sales in your books and sales ya zreport ambayo zote ni annual

Na tofaut ni kubwa mno kama ulivyo sema hukuwa unatoa risiti!

kingine wanaweza taka kuona manunuzi yako yapoje kwa mwaka husika, ikiambatana na ukaguzi kwenye store kama ipo !

Unahitaji mtu wa tax nkuunganishe naye anaweza kukupa ushauri wa kikodi !
 
Ni mtu mmoja. Nikienda sijui naeleza nini...tena nisimkute yule jamaa tena this time,anaongea sana na hasikilizi kabisa
Acha ufala wewe.ukienda sema biashara mbaya .kuna siku huuzi kabisa.sema mashine unatumia hata Kama umeuza pipi.tena sema unataka kufunga kabisa biashara Hali ni mbaya.wakukadirie Kodi ndogo.
Kama huwezi nitafute twende wote useme Mimi my wife wako unilipe
 
We hamaa unisamehe kwa haya nitakayo kuambia. Wewe ni aina flani hivi ya watu, wajuajijuaji, wanaongea sanaa, unampiga mtu ki saikolojia halafu unamwambia dawa ninayo ili akupe pesa. Kuna watu wanaishi hivyo na inawezekana na wewe ni mmoja wao, hii kitu siipendi kabisa. Tunajua kuwa na taarifa sahihi ni mtaji ila usiutumie kumtisha mtu.
 
Upo sahihi kabisa, lakini mm mwenyewe nimeona watu wanaosumbuliwa na issue kama za huyu lakini mimi sihitaji hata hamsini yake ndo maana sikuweka namba ama mawasiliano mkuu! Ila ni kwenye kumsaidia tuu..... Nipo humbled

Tunatofautiana kwenye namna ya kuelewa vitu mkuu 👊
 
Back
Top Bottom