Mlaleo; soma majina ya askari wa Kawe aliyetajwa kama kawaida kwa jina moja la Glory, je, kuna akina Glory wawili Kawe? Kama ni mmoja mchunguzi makini hawezi kutoa jina moja Mara mbili katika list moja. Huu ni ubabaishaji na ukurupukaji kama siku zote. Jina moja linaanza na WP GLORY lingine Glory moja kwa moja, sijui ni kuongeza idadi?Mimi Nimechoka kusikia Majina ya Polisi yanatajwa kwa jina moja as if Hawajulikani au hawajahakiki TIN zao!
Wale ni wasanii sasa unadhani wangemtumia nani kutumbuiza?Hivi hawa wasanii si ndo walikuwa wapiga debe no.1 wa chama fulani mwaka juzi? Unamtumia mtu mwovu kupata mkate halafu ukishashiba unakuja kututangazia uchafu wake? Kwani wakati unamtumia hukumuona ana uchafu au ndo ya baniani mbaya? Wamesahau kampeni ya "mama mkanye mwanao vinara walikuwa kina nani? Au tuamini na chama nacho kinachunguzwa kwa kushirikiana na madalali wa unga?
Wakuu kwa ninachokiona kwa sasa kwa hili tukio la wasanii kuhusishwa na matumizi ya dawa za kulevya ni kutaka kuondoa attention ya watu kuhusu;
1)matokeo mabovu ya wanafunzi wa kidato cha nne hasa wa dar es salaam
Kwa kuwa si hali ya kawaida kwa kweli
2)kuondoa attention ya watu na kuwasahaulisha kabisa kuhusu sekeseke linaliendelea kwa sasa bungeni
Hii ndio tabia ya viongozi wa nchi wakiona wamebanwa haswaa basi watatengeneza tukio la kisiasa ili kuondoa attention iliyopo katika jamii
Mfano kuhusu ugonjwa wa dengue , kiuhalisia huu ugonjwa haukuwepo ila zimetengenezwa figisu figisu ili kufanya tukio fulani la kisiasa lipite
Hali kadhalika ugonjwa kama ebola haukuwepo nchini ila kwa ajili ya kuondoa attention ya watu waliutangaza kwa nguvu zote ili kupisha upepo wa kisiasa upite
Hivyo basi rai yangu ,
Wananchi msielekeze nguvu zenu kuhusu hawa akina wema na wasanii wengine kesi haitakwenda kokote bali ni kuzubaisha watu wasahau matokeo mabovu ya kidato cha nne na mambo yanayoendelea bungeni
Wewe hujajiuliza kwa nini hili suala limekuja ghafla hivyo? Kwani hapo zamani walikuwa hawajui kuwa wanatumia dawa za kulevya kama vile Chidy benzi kwa nini walikaa kimyaa?
Ukishajiuliza natumai utapata jibu sahihi
Mwenye macho haambiwi tazama wala mwenye maskio haaambiwi sikia
Tchaoooo
Shemeji yenu Petit Man amekamatwa na mzigo kabisa mmeanza kulia-lia,
Pia DJ wenu wa WCB Rommy Jones naye amekamatwa na mzigo ndiyo maana vijana wa WCB mmemchukia Makonda ghafla.
Ukilemaa unaachwa feri.akili kumkichwa mkuu