Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Wakuu, hebu tukae kitako!
Ghafla nimeikumbuka ile kauli maarufu ya Job Ndugai aliposema, "Kuna siku nchi itapigwa mnada" akionya kuhusu mzigo mkubwa wa madeni unaoendelea kukua.
Hebu tuangalie hali mwenendo wa Deni la Taifa:
Deni la Taifa limekuwa likiongezeka mwaka hadi mwaka. Mwaka 2019, wakati Waziri wa Fedha na Mipango akiwa Dkt. Philip Mpango, deni hilo lilikuwa Shilingi Trilioni 51.03, likiwa limeongezeka kutoka TSh. Trilioni 49.86 mwezi Aprili 2018.
Hadi kufikia Aprili 2021, deni hilo lilikuwa TSh. Trilioni 60.9.
Kwa mwaka wa fedha ulioishia tarehe 30 Juni 2023, deni la Serikali lilifikia TSh. Trilioni 82.25, sawa na ongezeko la asilimia 15 kutoka TSh. Trilioni 71.31 mwaka wa fedha 2021/22.
Mwaka uliofuata, hadi kufikia 30 Juni 2024, deni hilo liliongezeka na kufikia TSh. Trilioni 97.35 kutoka TSh. Trilioni 82.25 ya mwaka 2022/23.
Na hadi kufikia Aprili 2025, deni la Serikali limeripotiwa kufikia TSh. Trilioni 107.7 ikiwa ni ongezeko la TSh. Trilioni 10 kutoka TSh. Trilioni 97.35
Haya madeni yote tunayokopa, matokeo yake ni yapi kwa wananchi wa kawaida?
Barabara? Huduma za afya? Ajira? Maji? Elimu bora? Au tunaongeza mzigo kwa vizazi vijavyo?
Pia, Soma

- CAG: Deni la Serikali lafikia TSh. Trilioni 97.35, ongezeko la TSh. Trilioni 15.1
- Serikali: Deni la taifa lafikia Tsh. Trilioni 107 ikiwa ni ongezeko la 14.9%
- Mpina: Ukuaji wa deni la Taifa unatia shaka, Waziri Mwigulu haelezi matumizi ya mikopo, ana-concentrate muda mwingi kutafuta mikopo nje ya nchi
- Professa Tibaijuka ashtushwa na kasi ya ukuaji wa deni la taifa