#COVID19 Kuna siku Watanzania watapanga foleni za kilomita kadhaa ili kuchanja

#COVID19 Kuna siku Watanzania watapanga foleni za kilomita kadhaa ili kuchanja

Nakwambia hivi si ajabu hilo maana watu hawajaanza kufa leo kwa ujinga, huko hospitali kuna watu wamelazwa kwa maradhi ambayo sababu ni ujinga tu. Tunasumbuliwa na maradhi mengi sana na husababisha vifo vingi ila yote hayo sababu ni ujinga tu, kama tungejielewa hayo maradhi tusingapata na tungeepusha vifo.

Sasa mimi nakushangaa wewe unaona ujinga kwenye corona tu!
kwahiyo sababu kufa kwa ujinga ni kawaida, tuendelee kufa hivyo?
 
Variants ni nyingi. Ikitokea variants ambayo haisikii hii chanjo ya J&J ntaenda tena kuchanja. Na ntaendelea kujikinga na Corona sababu kuna variants zingine na chanjo siyo 100%
Asichokijua yeye ni kuwa inawezekana ukachanjwa chanjo hata 10 na kila moja inafanya kazi kivyake, kama ilivyo kwa sasa,ndani ya miili yetu kuna chanjo ya ndui, mabusha, pepo punda, hepatitis, corona n.k, lakini kila moja inafanya kazi kivyake.
 
Sasa kwanini watu wasitake chanjo sasa hivi ili kuepuka hivyo vifo? kwanini unaona baadaye ndio watakimbilia hizo chanjo?
wanaujinga, ila kadri vifo vitavyoendelea watapata akili. jinsi mbinyo wa kuingia viwanjani unavyoendelea watapata akili.
 
kwahiyo sababu kufa kwa ujinga ni kawaida, tuendelee kufa hivyo?
Swali hilo nikuulize wewe ambaye sijaona kupigia kelele vifo vya ujinga vya maradhi mengine ila unakuja kupiga kelele katika vifo vya corona tu? Ina maana hivyo vifo vyengine vya kijinga umeona ni sawa tu ila kasoro corona?
 
Kuna jamaa yangu alikuwa mbishi Sana akawa anasema Corona haipo ni siasa tu so sad tumemzika mwezi uliopita kwasababu ya COVID-19 alikuwa mtu mwema na muhimu Sana kwangu [emoji24][emoji24][emoji24]

Sent from my TECNO B1f using JamiiForums mobile app
 
wewe unaweza kusaidia kupigia kelele vifo vingine vinavyosababishwa na ujinga.
 
wanaujinga, ila kadri vifo vitavyoendelea watapata akili. jinsi mbinyo wa kuingia viwanjani unavyoendelea watapata akili.
Si akili labda uoga ambao utatokana na kutishwa, hata sasa Bongo serikali ingetaka kuwatisha watu basi ingeweza na pengine idadi ya watu kuchanjwa ingeongezeka.

Kwahiyo issue sio kupata akili, ingekuwa kupata akili basi tungeshapata akili kwa haya maradhi mengi yanayosumbua sasa hivi tungeyaepuka ambayo yana sababisha vifo mpaka sasa kuliko hata corona.
 
Kuna jamaa yangu alikuwa mbishi Sana akawa anasema Corona haipo ni siasa tu so sad tumemzika mwezi uliopita kwasababu ya COVID-19 alikuwa mtu mwema na muhimu Sana kwangu [emoji24][emoji24][emoji24]

Sent from my TECNO B1f using JamiiForums mobile app
Ni hatari sana. Zamani nilifikiri peer pressure (shinikizo rika) lipo kwa teenegers tu, hata kwa watu wazima kumbe. Watu wazima wanafuatana, hawana sababu za msingi ila wanafuata wenzao. Wenzao wakisema chanjo haifai nao wanafuata, hawajui kwanini haifai. Pole sana kwa msiba.
 
Kwa Tanzania hii Shujaa pekee ndo angeweza kutupangisha foleni ya chanjo.

Nikikumbuka zama za level seat kwenye daladala siamini Tanzania tuliweza kuwa wastaarabu kwa asilimia 90

Mifuko ya plastic ilipotelea mbali kwa hofu ya shujaa

#mwagapovuatyourownrisk
 
Wazungu wenyewe hawataki chanjo na hata hivyo wazungu walisema tutaokota mizoga barabarani lakini wapi, wanakufa wao kama kuku huku afrika watu wanadunda.

Wewe jiandae kuchomwa dozi nyingine ya booster kama kuku anaeumwa kideri.

Kuna lambda variant haisikii chanjo, utachanjwa tena na tena kila variant ikija kama kuku.

Hapangi mtu foleni hapa.
 
Si akili labda uoga ambao utatokana na kutishwa, hata sasa Bongo serikali ingetaka kuwatisha watu basi ingeweza na pengine idadi ya watu kuchanjwa ingeongezeka.
Kwahiyo issue sio kupata akili, ingekuwa kupata akili basi tungeshapata akili kwa haya maradhi mengi yanayosumbua sasa hivi tungeyaepuka ambayo yana sababisha vifo mpaka sasa kuliko hata corona.
Korona inaweza usiuue kama Malaria na UKIMWI, lakini Ogopa sana airborne diseases. hizi ni tofauti na malaria na ukimwi. Plague ya miaka ya 1300(black death) na Spanish Influenza zote ni Airborne. Ziliuwa kwa kutisha. mwanzoni hii black death ilikuwa inaambukizwa kwa kung'atwa na viroboto wa 'panya' ambao walikuwa wanakudunga bakteria Yersinia Pestis.

Sasa huyu mdudu akajigeuza, akaingia kwenye mapafu na kuweza kuambukizwa kwa njia ya hewa. hapo ndipo mamilioni ya watu wakaanza kufa. usifananishe aiborne diseases na vitu kama Malaria. huu ugonjwa unapotential ya kuua watu wengi kuliko UKIMWI na Malaria. au tuseme magonjwa yote yakiwekwa pamoja.
 
Hivi naulizia wanaokufa kwa CORONA waliishachanja chanjo ya J&J au nyingine au walikuwa bado kuchanja?. Ili ni swali fikirishi sana.
 
Ni hatari sana. Zamani nilifikiri peer pressure(shinikizo rika) lipo kwa teenegers tu, hata kwa watu wazima kumbe. Watu wazima wanafuatana, hawana sababu za msingi ila wanafuata wenzao. Wenzao wakisema chanjo haifai nao wanafuata, hawajui kwanini haifai!! pole sana kwa msiba.
Mbona hata huko hospitali tunafuata tu kila tunachoambiwa na daktari huku tukiamini yeye anajua kila kitu kwa sababu kasoma ni daktari, lakini uhalisia haupo hivyo.

Hata hao waliyochanja si kwamba wote wamepata elimu ya chanjo ila wengi ni mkumbo tu, mtu kakaa kijiweni kaona wenzie wamechanja na yeye akaenda kuchanja wengine toka utu uzima hajachanja chanjo yeyote basi ushamba tu akaona nae kujaribu basi hawana elimu yeyote kuhusu huu ugonjwa wala hizo chanjo.
 
Back
Top Bottom